Mbona Rais Samia anaturudisha Dar es Salaam wakati Makao Makuu ni Dodoma?

Kifo cha Magu kimeonyesha unafiki ulivyowajaa Watanzania. Magu alihamishia shughuli za serikali kijijini kwake, mkaja hapa kusema "Ikulu ni popote alipo Rais". Sasa mtulie, hata akienda kupokea hati huko kwa MchambaWima muwe wapole tu.
 
JK aliwashtua watu wakati alipoonesha wapwani hawakupendelea mji mkuu kuhamia Dodoma. Awamu yake ya urais suala la kuhamia Dodoma halikuwekwa kabisa kwenye ajenda.

Sasa tuna Rais mwanamama mpwani. Tangu ameshika Urais inaonekana kama tumerudi Dar kwani kila kitu yuko hapa Dar.

Amehutubia wazee wa Dar juzi, amepokea hati za mabalozi Dar, Jumatano anaapisha wakuu wa mikoa Dar. Mwendazake shughuli Dodoma zilifanyika ikibidi kwenye mahema. Sasa hii trend ya kurudi Dar mbona inapata kasi sasa wakati hadi sheria ishasema Dodoma ndio mji mkuu?.

Tunamuomba Rais Samia awe na moyo na ujasiri kusimamia sera na utendaji kama Hayati Magufuli.

Wananchi walimpigia kura Magufuli kwa wingi watafarijika sana kuona misimamo yake inaendelezwa.
Nyie Sukuma Gang acheni manenomaneno, mfano ulitaka wazee wa Dar akawahutubiwe Chato?
 
Tuwe na msimamo kama Dodoma ndo makao makuu au irudi Dar, tatizo watu wa pwani hawaijui Tanzania ndo mana wanakimbilia Dsm
 
Shida kubwa ni ushabiki usio kuwa na maana. Huenda kuna watu wengi hawakupenda serikali kuhamia Dodoma. Na wengine ni viongozi wakubwa. Hivyo kuona mwendazake amenyamaza milele usistaajabu yanayotokea. Lakini muda ni mwalimu mzuri.
 
Mbona tulipelekwa Chato hukuuliza? Kabla hujaanzisha thread fukiria kwanza maana Hapa jukwaani kuna watu ni great thinkers hawafuati upepo.
 
JK aliwashtua watu wakati alipoonesha wapwani hawakupendelea mji mkuu kuhamia Dodoma. Awamu yake ya urais suala la kuhamia Dodoma halikuwekwa kabisa kwenye ajenda.

Sasa tuna Rais mwanamama mpwani. Tangu ameshika Urais inaonekana kama tumerudi Dar kwani kila kitu yuko hapa Dar.

Amehutubia wazee wa Dar juzi, amepokea hati za mabalozi Dar, Jumatano anaapisha wakuu wa mikoa Dar. Mwendazake shughuli Dodoma zilifanyika ikibidi kwenye mahema. Sasa hii trend ya kurudi Dar mbona inapata kasi sasa wakati hadi sheria ishasema Dodoma ndio mji mkuu?.

Tunamuomba Rais Samia awe na moyo na ujasiri kusimamia sera na utendaji kama Hayati Magufuli.

Wananchi walimpigia kura Magufuli kwa wingi watafarijika sana kuona misimamo yake inaendelezwa.
Unataka aende kwenye ikulu ya Chato?
 
Shida kubwa ni ushabiki usio kuwa na maana. Huenda kuna watu wengi hawakupenda serikali kuhamia Dodoma. Na wengine ni viongozi wakubwa. Hivyo kuona mwendazake amenyamaza milele usistaajabu yanayotokea. Lakini muda ni mwalimu mzuri.

..kwa maoni yangu, GHARAMA za kuhamia Dodoma ni kubwa kuliko faida.

..fedha zilizotumika zingeweza kugharamia mahitaji mengi ya msingi, yanayogusa wananchi wengi kuliko walioguswa na zoezi la serikali kuhamia Dodoma.
 
JK aliwashtua watu wakati alipoonesha wapwani hawakupendelea mji mkuu kuhamia Dodoma. Awamu yake ya urais suala la kuhamia Dodoma halikuwekwa kabisa kwenye ajenda.

Sasa tuna Rais mwanamama mpwani. Tangu ameshika Urais inaonekana kama tumerudi Dar kwani kila kitu yuko hapa Dar.

Amehutubia wazee wa Dar juzi, amepokea hati za mabalozi Dar, Jumatano anaapisha wakuu wa mikoa Dar. Mwendazake shughuli Dodoma zilifanyika ikibidi kwenye mahema. Sasa hii trend ya kurudi Dar mbona inapata kasi sasa wakati hadi sheria ishasema Dodoma ndio mji mkuu?.

Tunamuomba Rais Samia awe na moyo na ujasiri kusimamia sera na utendaji kama Hayati Magufuli.

Wananchi walimpigia kura Magufuli kwa wingi watafarijika sana kuona misimamo yake inaendelezwa.
Tunataka Samia ahamie Chato kabisa
 
Hatumkatazi, atangaze tu yeye makao yake ni Dsm, aache unafiki na itupunguza gharama ya viongozi wote kuishi Dodoma wakati yeye yupo Dsm.
Unafiki ni kufanyia shughuli za serikali ikulu ya Dar es Salaam au nyumbani kwa mama Chato?
 
Back
Top Bottom