Mbona Rais Samia anaturudisha Dar es Salaam wakati Makao Makuu ni Dodoma?

Kama ameamua kurudisha makao makuu ya nchi kuwa Dsm aseme wazi tu, SSH ana ka unafiki fulani, anafanya maamuzi ili ku please watu tu, ni kheri aseme wazi waache kujenga Dodoma kuliko huo unafiki anaotaka kujaribu kufanya.
Dodoma kuna hospitali ya vichaa... Mama arudi Dar asije akacharazwa bakora na yule kichaa wa bungeni...
 
JK aliwashtua watu wakati alipoonesha wapwani hawakupendelea mji mkuu kuhamia Dodoma. Awamu yake ya urais suala la kuhamia Dodoma halikuwekwa kabisa kwenye ajenda.

Sasa tuna Rais mwanamama mpwani. Tangu ameshika Urais inaonekana kama tumerudi Dar kwani kila kitu yuko hapa Dar.

Amehutubia wazee wa Dar juzi, amepokea hati za mabalozi Dar, Jumatano anaapisha wakuu wa mikoa Dar. Mwendazake shughuli Dodoma zilifanyika ikibidi kwenye mahema. Sasa hii trend ya kurudi Dar mbona inapata kasi sasa wakati hadi sheria ishasema Dodoma ndio mji mkuu?.

Tunamuomba Rais Samia awe na moyo na ujasiri kusimamia sera na utendaji kama Hayati Magufuli.

Wananchi walimpigia kura Magufuli kwa wingi watafarijika sana kuona misimamo yake inaendelezwa.
Anasubiri kuhamishwa kwa Bandari Dodoma kwanza.
 
Mleta mada tafuta wimbo wa Komando Hamza Kalala. Mambo yote yapo Darbrs Salaam. Dodoma wanakwenda n.a. kurudi.
 
Ikulu ya daslam haijafungwa....bado inatumika pia....mbona majuzi kuna matukio alikuwa akifanyia Dom, lakin Hata akienda kufanyia Kagera yoote ni Tanzania...mangapi yalifanyikia Chato tena nyumbani kwa mtu....
 
Mji mkuu Dar es salaam upo naturally umejiweka wenyewe kwa biashara.

Watu ambao uchumi wao mdogo, bajeti yao ina mambo mengi, wanajiongezea anasa ya kuhamisha makao makuu ya serikali.

Matokeo nchi ina miji mikuu miwili na wa tatu ni barabara inayounganisha miji hii.

Ni mambo ya ajabu sana.
 
Mbona Mwendazake alikuwa akiapisha Mawaziri Chato na hamkusema, cha ajabu kipi SSH (Sasha) kuapisha Mawaziri Dar??

Kwani imeandikwa wapi kwamba shughuli za uapishaji ni lazima zifanyiwe Dodoma ???
Dodoma wamuachie ******* aapishe watu garage
 
Ikulu ya daslam haijafungwa....bado inatumika pia....mbona majuzi kuna matukio alikuwa akifanyia Dom, lakin Hata akienda kufanyia Kagera yoote ni Tanzania...mangapi yalifanyikia Chato tena nyumbani kwa mtu....
mleta uzi anapata mashaka kuwa, mbona kama vile makao makuu hayapewi hadhi yake inayo stahili?!!

kwa mkeka huu mkubwa ni aghalabu tukio kufanyikia Dar. wengi walitegemea tukio kufanyikia Makao makuu ya nchi.
 
Angehamishia zenji hapo ungekua na haki ya kulalamika ila dar ni sawa kabisa na ndipo penye pilika pilika nyingi na amepazoea
Mimi binafsi, mradi wa makao makuu Dodoma ni mzigo kwa Taifa. Ni mzigo kwa sababu, miaka ya nyuma Serikali imewekeza sana Dar kwa kujenga majengo ya wizara na idara mbalimbali kuwa ya kisasa pamoja na miundombinu ili kukidhi mahitaji ya kileo. Ghafla tukaamia Dodoma na uamuzi wa Dodoma. Tukaanza ujenzi upya. Tumejenga flyover Tazara na Ubungo ili kuondoa jam wakati wa wafanyakazi kuja na kutoka kazini. Ghafla tukaamia Dodoma. Ghafla tukaamishia stend ya mkoani Mbezi. Tumejenga terminal 3, sasa akili zote ziko uwanja wa Msalato. Maamuzi haya yote ni gharama kubwa kwa Taifa. Je wananchi watarndelea kubeba taabu hizi hadi lini?
 
Mbona makao makuu ni Dodoma ila Balozi wa China, Museveni na Rais wa Malawi waliwahi kutua Chato?
Ofisi ya Rais ikulu ya Dodoma iko katika hatuza mwisho kukamilika no ofisi kubwa sana nadhani wakati katika hatuza za mwisho finishing sio kazi ndogo ile ikiisha mambo mengi yatafanyika, ila mwisho wa siku anaweza kufanya shughuli siku hata Zanzibar maana kila mkoa kuna ikulu ndogo hakuna shida.
 
Mimi binafsi, mradi wa makao makuu Dodoma ni mzigo kwa Taifa. Ni mzigo kwa sababu, miaka ya nyuma Serikali imewekeza sana Dar kwa kujenga majengo ya wizara na idara mbalimbali kuwa ya kisasa pamoja na miundombinu ili kukidhi mahitaji ya kileo. Ghafla tukaamia Dodoma na uamuzi wa Dodoma. Tukaanza ujenzi upya. Tumejenga flyover Tazara na Ubungo ili kuondoa jam wakati wa wafanyakazi kuja na kutoka kazini. Ghafla tukaamia Dodoma. Ghafla tukaamishia stend ya mkoani Mbezi. Tumejenga terminal 3, sasa akili zote ziko uwanja wa Msalato. Maamuzi haya yote ni gharama kubwa kwa Taifa. Je wananchi watarndelea kubeba taabu hizi hadi lini?
Dar es salaam mji uachwe kwa biashara tu ni muhimu sana viongozi wa serikali Dodoma na maendeleo kwenda sehemu zingine ni vizuri kuwa na Airport 3 international Tanzania ni jambo zuri. Siasa Dodoma, Biashara Dar foleni Dar bado zinapunguza kasi ya kukuwa kiuchumi. Mji wa serikali umeshajengwa Dodoma shughuli za bunge kule na hii ni sera ya CCM wameitekeleza.
 
Dodoma kuna hospitali ya vichaa... Mama arudi Dar asije akacharazwa bakora na yule kichaa wa bungeni...
Hatumkatazi, atangaze tu yeye makao yake ni Dsm, aache unafiki na itupunguza gharama ya viongozi wote kuishi Dodoma wakati yeye yupo Dsm.
 
Dar es salaam mji uachwe kwa biashara tu ni muhimu sana viongozi wa serikali Dodoma na maendeleo kwenda sehemu zingine ni vizuri kuwa na Airport 3 international Tanzania ni jambo zuri. Siasa Dodoma, Biashara Dar foleni Dar bado zinapunguza kasi ya kukuwa kiuchumi. Mji wa serikali umeshajengwa Dodoma shughuli za bunge kule na hii ni sera ya CCM wameitekeleza.
Foleni Dar haitaisha, Siku ukikuta imeisha kimbia ujifiche maana kuna shida mahali
 
Kwanza Dar ni katikati ya Tanganyika na Unguja. Bora angekaa Dar moja kwa moja tu!!
Alishasema bila kumungunya maneno kuwa Dodoma ipandwe miti ya kutosha,na istawi. Pia upungufu wa maji salama.Airport nayo ni kitendawili kwa midege mikubwa.
Hata mabalozi wa nchi za nje wapo Dar
Lakini pia hawezi kutumbukiza pesa nyingi za walipa kodi kwenye ujenzi wa Dodoma wakati kasema tumeshuka kiuchumi,itabidi kwanza atumie pesa chache tuliyonayo kwa miradi mikubwa ya mkakati kama Bwawa la Nyerere n.k
 
Mimi binafsi, mradi wa makao makuu Dodoma ni mzigo kwa Taifa. Ni mzigo kwa sababu, miaka ya nyuma Serikali imewekeza sana Dar kwa kujenga majengo ya wizara na idara mbalimbali kuwa ya kisasa pamoja na miundombinu ili kukidhi mahitaji ya kileo. Ghafla tukaamia Dodoma na uamuzi wa Dodoma. Tukaanza ujenzi upya. Tumejenga flyover Tazara na Ubungo ili kuondoa jam wakati wa wafanyakazi kuja na kutoka kazini. Ghafla tukaamia Dodoma. Ghafla tukaamishia stend ya mkoani Mbezi. Tumejenga terminal 3, sasa akili zote ziko uwanja wa Msalato. Maamuzi haya yote ni gharama kubwa kwa Taifa. Je wananchi watarndelea kubeba taabu hizi hadi lini?
Mwendazake aliwaogopa na kuwachukia matajiri hivyo akaona awahame kabisa
 
Back
Top Bottom