Najua tena Nakiri kuwa Uti Mgongo wa Media yoyote ile ni Matangazo na yakiwa mengi zaidi ndiyo Afya kwa Ustawi wa Kimapato kwa Media husika na Mishahara mikubwa na ya uhakika kwa Wafanyakazi (Watumishi) wake.
Ila hili la Kipindi cha Michezo cha Sports Headquarters cha EFM ambacho huwa kinaanza Saa 3 Kamili Asubuhi hadi Saa 6 Kamili Mchana kimetawaliwa na Matangazo mengi kuliko Contents za Michezo.
Kwa mfano Kinachowakera Wasikilizaji wengi ni pale Kipindi hiki cha Michezo kinaachoanza Saa 3 Kamili kuanza Kulundikwa na Matangazo ya Bandika Bandua na Taarifa za Habari kuanza ama Saa 3 na dakika 25 au na dakika 30 kitu ambacho Kinawakwaza Wasikilizaji (Audiences) wengi na kujikuta Wakihamia Kusikiliza Redio zingine kama Clouds FM, Uhai FM, Wasafi FM na hata Magic FM.
Tafadhali sana Boss Dizzo (Dickson Mwaimu) lichukue na lifanyie hili Kazi kwani linawakera Wasikilizaji wenu na sasa Wengi wao wameanza Kuwahama na msipoangalia na kubadilika mnaweza kujikuta mkawa Mnatangaza hapo Studioni mkidhani mnasikilizwa na Wengi kumbe mkawa mnasikilizwa na Wanafamilia wenu pamoja na Mahawara zenu ila Wenye Akili wameshawahama Kitambo tu.