Kila ukifungulia Redio karibia kila stesheni ni kamari tu, kucheze kubahatisha na mapesa kutolewa, watu wanapokea mamilioni, matv, na mambo kede kede kwa kuchangiana kucheza kamari buku buku kwenye maredio.
Hapo bado kamari za kwenye mitandao ya simu, na kwenye mipira, wazee wa mikeka, na wazee wa makasino, kwezi Tanzania pesa ipo. Mfano kuna redio kila baada ya nusu saa, au lisaa yanatoka mamilioni, sasa unashangaa wanaojichangisha huko hewani mpaka mshindi achukue laki 5 mpaka 10M ni wangapi?
Kuna mmoja akanishangaza kuwa ana line tatu, zote alikua anazichezea kuona ipi itashinda au ipi yenye bahati, kweli tuna pesa.
Kuna mwana JF yoyote aliewahi kushinda kweye hizi za redio za kila baada ya nusu saa atupe mrejesho?
Mwaka flani nilifanya kazi kama customer care agent kampuni flani ya simu, kulikua na kamari flani ya kushindania magari, nadhani lilifanyika miezi kadhaa.
Siku niko kwenye majukumu yangu ya kupokea simu akapiga mteja analalamika kacheza miezi yote hashindi, kuchek kweli kacheza inakaribia 3M, nikamshauri akomae siku yake inakuja, ila nilimuhurumia.
Sasa hivi ni kwenye maredio imeshika kasi, ni mipesa tu inatolewa, alafu tunalalamika tozo.
Ngoja tuendelee kukamuliwa mpaka maji tuite mma.