Mbona ulaya hawalalamikii hizi Pitch feeling

Mbona ulaya hawalalamikii hizi Pitch feeling

Thibitisha kama walifanya mazoezi. Hilo ni takwa la kikanuni, ina maana waliyoiweka hawakujua faida yake sio?

Last match, Yanga walifanya pitch visiting. Na hakukuwa na bugdha na unaweza hata wewe ulikuwa hujui kwasababu Simba haikutaka kutengeneza 'Tension' hiyo.

Kwanini sasa?
TAARIFA RASMI KUTOKA MENEJA WA UWANJA
Meneja wa uwanja alikuwa tayari kuwaruhusu na kuwafungulia geti Simba SC ili wakafanye mazoezi kwamujibu wa kanuni ila aliposika sauti ya mbuzi kutoka ndani ya moja basi akakataa kuwafungulia kwa masharti ya kuomba kushushwa wale mbuzi na waganga ambao inasemekana walikuwa wanapelekwa kuchinjwa kwa ajili ya kuendesha ibada kuelekea mechi husika ikiambatana na uchinjwaji wa hao mbuzi.

Sera ya LATRA inasemaje katika ubebaji wa wanyama?

Mvutano ulianzia pale klabu ya Simba haikuwa tayari kushusha wale mbuzi na waganga na zaidi kukataa kuingia wachezaji peke yake.

Gordon Mahona: Meneja wa Uwanja
 
Mzee Nguya kutoka hapa mikindani alikuwepo kwenye basi mojawapo la simba wanae wanampigia Simu kumuulizia kama yupo salama bahati mzuri mzee wetu kajibu yupo vyema hajajeruhiwa popote pale wala hakuguswa...wenyeji wa mikindani bila shaka munamjua huyu mzee
 
Unaweza kuiona ya 'Kipuuzi'. Una haki hiyo.

Mechi iliyopita hiyo sababu ya 'kipuuzi', mliitaka na Simba ikaruhusu.

Kwanini upande wenu unakataa kwa kufikiri ni "Upuuzi'?
Ni Upuuzi kwa simba kugomea mechi ati kwa ajili ya kukataliwa pitch feeling.kwani huo uwanja imeshushwa leo au ni uwanja mgeni kwao?mbona kila kukicha wanajinasibu kuwa kwa makala hatoki mtu sasa leo imekuwaje?waache imani za kishirikina ni aibu kwao.
 
Yanga waligomaje na wakati walienda uwanjani kwa muda sahihi waliopangiwa kwenye ratiba! Wasingefika ndiyo ungesema wamegoma/wamesusa.
Waliopanga muda ndio waliobadilisha muda. Sasa iweje usitii mamlaka?
 
Miaka yote ya mechi za watani,mwenyeji anakabidhiwa uwanja,mgeni anaingia uwanjani siku ya mechi akitokea mahali alipoweka kambi sababu ni culture waliyo jiwekea wenyewe watani.Ndio maana hata meneja hakuwa na taarifa za wao kuja uwanjani. Hata Yanga hii nafasi ya kutumia huu uwanja kabla ya mechi round ya kwanza hakupewa, je hizo kanuni hazikuwepo, maana aliingia uwanjani akitokea Avic Town na mechi alicheza.
Umeandika vinini wewe? Ulizani simba watalala humohumo hadi saa ya game?
 
Ni Upuuzi kwa simba kugomea mechi ati kwa ajili ya kukataliwa pitch feeling.kwani huo uwanja imeshushwa leo au ni uwanja mgeni kwao?mbona kila kukicha wanajinasibu kuwa kwa makala hatoki mtu sasa leo imekuwaje?waache imani za kishirikina ni aibu kwao.
Simba hawajawahi kuzungumzia kwa MAKALA, Wao wanasema kwa MKAPA
 
Umeandika vinini wewe? Ulizani simba watalala humohumo hadi saa ya game?
Hilo jibu mngempa mwenye funguo za uwanja ambaye ni meneja,ambaye nyie wenyewe kwenye barua yenu mmekubali kwamba meneja hakuwa na taarifa.
 
Hapa kuna harufu ya kuwahi kufanyiana mambo ya kishirikina kwenye uwanja na wala siyo jengine.
 
Back
Top Bottom