Nashengena
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 2,913
- 5,318
Hahahh, kuna ndugu zangu walikuwa wanamsakama mdogo wangu unaoa lini, kila kikao au shughuli wanamuuliza.Naendelea kukusanya data kila siku.
Ukikaa na wanaume huwezi ukasikia wakimshauri mwanaume mwenzake kuoa mara kwa mara lakini kinyume chake
wanawake wamekuwa washauri wakuu wa vijana waliofikia umri wa kuoa kwamba oa oa ♫︎♫︎♫︎♫︎ kama wimbo sasa sijui kwa nn wao ndio washauri wakuu siku hizi.
Utaskia wanasema oa kijana umri unaenda.
Oa maisha ni hayahaya.
Oa utakuja kuitwa babu na watoto wako.
Oa utakuja kuzaa watoto wasiokuwa kuwa na akili.
Oa utakuja kusomesha uzeeni
Oa watukuja kukugongea mke wako.
Oa utakufa uache watoto wadogo.
Oa uendeleze kizazi eti kitapotea.
Utaishije mwenyewe huo ni uchoyo.
Oa ukifa upate wa kukulilia
Mbona wanakuja kwa kasi sana.
Ukijipenda mwenyewe watu wanaonaje sijui.
Jitathmini mwenyewe kwanza ewe kijana.
Siku moja akawatolea uvivu, hivi nikioa mtafaidika nini?
Toka siku hiyo hawakumuuliza tena. Kipindi hicho alikuwa na vikazi vya kuungaunga na hata kodi ya nyumba ilikuwa inasumbua kulipa.
Wabongo ni shida sana. Kuna ndugu yangu eti mtoto wa sijui elfu 2000 wamemupzesha na hana kazi. Sasa hivi mama yake kastaafu analea mtoto, mkwe , mjukuuu, analalamika maisha magumu.
Nawaangalia tu wapambane na hali zao.