Mbona wanawake ndio wanaongoza kwa kushauri wanaume kuoa?

Hahahh, kuna ndugu zangu walikuwa wanamsakama mdogo wangu unaoa lini, kila kikao au shughuli wanamuuliza.
Siku moja akawatolea uvivu, hivi nikioa mtafaidika nini?
Toka siku hiyo hawakumuuliza tena. Kipindi hicho alikuwa na vikazi vya kuungaunga na hata kodi ya nyumba ilikuwa inasumbua kulipa.
Wabongo ni shida sana. Kuna ndugu yangu eti mtoto wa sijui elfu 2000 wamemupzesha na hana kazi. Sasa hivi mama yake kastaafu analea mtoto, mkwe , mjukuuu, analalamika maisha magumu.
Nawaangalia tu wapambane na hali zao.
 
mbona kama falsafa ......fafanua tena kidoogo japo anayefaidi ni mwanamke na mwanaume hana maana.
 
Ndoa ni ajira ya kudumu kwa mwanamke. Endapo mwanamke maisha yakimpiga knock out basi ndoa inaweza kuwa kimbilio lake. 100% 𝐰𝐞𝐧𝐠𝐢 𝐰𝐚𝐤𝐢𝐨𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐦𝐞𝐬𝐡𝐢𝐧𝐝𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐜𝐡𝐨𝐡𝐢𝐭𝐚𝐣𝐢 𝐡𝐮𝐭𝐚𝐟𝐮𝐭𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐮𝐦𝐞 𝐰𝐚 𝐤𝐮𝐰𝐚𝐧𝐲𝐚𝐧𝐲𝐚𝐬𝐚.
 
naamini na kuhisi tunaitaji zaidi wanawake ambao ndoa kwao is not about identity au wenye kufikiria kuwa nikiwa 'mke wa mtu' ndiyo nakuwa na heshima kwenye jamii;

kwa mawazo ayo ndiyo inapelekea wengi kuona ndoa kama jau, just imagine unaona mwanamke ambaye anaingia kwenye ndoa kwasababu tu anataka ndoa as identity au kuitwa mke wa mtu;

sikatazi watu kuoa ila usioe mtu ambaye kwake ndoa ni kama kivuli cha identity yake au anatamani tu kuitwa mke WA MTU.....
 
Unaheshimika bwana ukiwa umeoa, unaacha kuonekana muhuni. Unaonekana unajua wajibu. Huulizi kwanini kuna nafasi huwezi kupata kama hujaoa?
hapa ndiyo panapo tuumiza yaani ni kama tunafanya vitu kwa kuhofia watu watanionaje;

Oa lakini ndoa isiwe kitu cha kufanya kisa tu ooh! ntaonekana muhuni, nisipo oa ntaonekana sijui wajibu wangu;
 
Wewe jamaa unajua sana.
 
Ukiondoa sababu za kiimani( kwa waamini).....mkataba wa ndoa una manufaa makubwa kwa mwanamke kuliko kwa mwanamume........ mwanamke akishaingia kwenye ndoa anakuwa amesha tatua robo tatu ya matatizo yake maishani mwake......... mwanamke mwenye ufahamu lazima alilie kwa kuwa ndani yake kuna manufaa mengi......
 
hapa ndiyo panapo tuumiza yaani ni kama tunafanya vitu kwa kuhofia watu watanionaje;

Oa lakini ndoa isiwe kitu cha kufanya kisa tu ooh! ntaonekana muhuni, nisipo oa ntaonekana sijui wajibu wangu;
Sio kwamba unaonekanaje, wapo watu ambao hawajaoa na haina shida

Ni kwamba tu ukiipatia ndoa, faida yake ni maradufu. Watu hapa hawasemi, ila bila wake zao wasingekuwa walipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…