Yani siku hizi mtu kutekwa na kuuwawa au kupotezwa imekuwa kitu cha kawaida. Watanzania wanajazana kwenye comment section kutiana mwoga na kushangaa tu. Hii inadhihirisha hile kauli ya "Tutakupoteza na Watanzania watapiga kelele siku 2 kisha watakusahau".
Kila mtu sasa hivi Tanzania ni victim wa kutekwa, ni suala la muda tu... na wengine tunachukulia poa kwa sababu aliyetekwa sio wewe, wala si ndugu yako, wala si mtu wako wa karibu. Lakini amini kwamba tusipoangalia kila mtu anaweza kuwa mhanga wa utekwaji au kuuwawa.
Mtu kavunja sheria, basi miongozo ya sheria ifuatwe... mtu akamatwe kisha apelekwe mahakamani. Lakini gafla tu mtu anapotea mara ajulikani halipo mara kauwawa...