Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Kila mtu mwenye akili timamu anajua ni jitihada za Tundu Lisu.
 
yeah, yamekugusa eee !!

Sasa ifike pahala kudai katiba mpya isiwe kosa la jinai - nafikiri ujumbe huu uwafikie wana Lumumba wote.
Mimi sio lumumba buku7 wala ufipa buku2
 
Hii ina maana gani kisheria? Jaji anasema kuna kesi ya kujibu na DPP anasema hakuna kesi ya kujibu? Nani ni msomi wa sheria na nani ni KIHIYO kati ya hao wawili?
 
Afadhali . Sasa tufuatilie yanayojiri Russia Ukraine vizuri
 
Tulishasema Mbowe ni mwamba, mlikaza fuvu…. ona sasa.!
 
Mimi sio lumumba buku7 wala ufipa buku2
sawa, sasa unafikiri hiyo kesi ilikuwa na uhai kwa taifa letu? wote sisi tumefurahi sababau kesi kwanza ilikuwa inatuabisha kama taifa.

Tufike pahala watanzania tuwe serious na mambo ya msingi na tuachane na mambo haya ya kukomoana yanayotupotezea muda na heshima kama taifa,
 
Mimi kwangu nitaikumbuka kesi hii kwa jinsi ilivyovutia,sidhani kama kuna kesi nyingine ambayo iliwahi kusikilizwa hadharani na kwa uwazi namna ile katika nchi yetu!
Tumeshuhudia jinsi Mawakili walivyochuana,tumeshuhudia jinsi waendesha mashitaki,wapelelezi wa serikali walivyokuwa wanajikanyagakanya na hata kutufanya tujue udhaifu wao.Tumeshuhudia baadhi ya Majaji walivyoikimbia kesi.
Katika hili nilikuwa naomba kesi zote ziwe zinasikilizwa kwa uwazi namna ile ili tujifunze mambo mengi yanayohusu Sheria.
Pongezi zangu ziwaendee Kibatala na Jopo lake!
 
Afadhali . Sasa tufuatilie yanayojiri Russia Ukraine vizuri
Putin kalalamika kasema si vizuri kuendelea kumuwekea vikwazo vya kiuchumi - yeye ana nia njema na Taifa la Ukraine.

Vita baridi achana nayo, tayari imeshaanza kumwingia.
 

Unateseka sana.”
 
Mimi nitapamisi sana pale RAU Madukani kwa Mama P. - pia Mo energy kwa mishikaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…