Au ndo Maana anachimba Mkwara mzito ili waogope Kumdai?
Mbona hatujapata jawabu? Au ndio kukubali kikubwa?
Si ungeuliza hapo barazani? Au wambea wako waliondoka ghafla ulivyotokea.
Sasa kama ameshindwa kulipa mbona huyo anayemdai asichukue hatua dhidi yake? Au mnamuogopa?
Na zaidi, ilikuwaje mpaka aliyetoa mkopo akubali kuchukua dhamana ambayo haitoshi kulipa deni na riba? Tunashukuru kwa taarifa hii kwa sababu uozo na uzembe kama huo ndio umetufikisha hapa.
Kitendo cha mtu kutoa hela halafu anashindwa kuzidai na pia anachukua dhamana ambayo haitoshelezi hakivumiliki. Lazima ashughulikiwe mara moja.
Hakuna mchezo aliocheza Mh. Mbowe. Ungekuwepo mngemchafua na kumuaibisha. Zimebaki story za barazani!
Kwanza hakuna mtu anaitwa Mbowe Jr. Mwenyekiti wa Chadema ni Freeman Mbowe na si Mbowe Jr.
Kamwulize aliyeanzisha mjadala.Uchakachuaji wa Taarifa. Tunachotaka kujua ni kweli au la?
Mbona una-chakachuwa saana, kweli si kweli?
Kama waliokwambia habari hizo hawakukupa jawabu unategemea nini kutoka hapa?
- Kama amekopa ni ishus za benki aliyokopa, sasa huku kwenye siasa yamekujaje? au?
FMeS!
Why not ask yourself?Na kama tayari umesha-conclude kuwa ulichoambiwa ni ukweli,what's your point in asking the question in the first place?
Nimesikia kibarazani kuwa Mbowe Jr., Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania, alikopa fedha nyingi huko akiba ya uzeeni na sasa kashindwa kuzilipa na mali alizoweka dhamana hazitoshi kulipa deni hilo na riba yake? Naomba wajuzi mtujuze, ni kweli hii?
Au wanamzulia? au kuna ka-mchezo alicheza?
Sasa kama una ushahidi kuwa Mbowe ana deni la kibiashara aliloshindwa kulipa uweke hapa. Au bora zaidi upeleke kwenye magazeti ya Rostum. Nina hakika watafurahi kuiweka habari hiyo front page. Siyo kuingia JF na kufanya character assassination by innuendo.Kumbuka huyo ni public figure, na ni dhahiri anafaa awe mfano wa kuigwa, sasa kama kweli ka deni ka biashara kanamshinda kulipa haka ka nchi si atakaweka rehani pindi atapoupata u Rais (wishful thinking).
Unaishi nchi gani?Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema 2010 alikuwa Mbowe?Katika kutapatapa kwenu mjigeuza Sheikh Yahya kutabiri kuwa Mbowe atagombea urais mwaka 2015.
Na kinachowawasha ni kipi hasa?The alleged creditors hawajasema lolote,na mnafahamu fika kuwa hiyo ingekuwa kete turufu kwa watu kama Makamba na Tambwe Hiza...nyie vimbelembele mnakuja na crazy assessments zenu!
Sasa kama una ushahidi kuwa Mbowe ana deni la kibiashara aliloshindwa kulipa uweke hapa. Au bora zaidi upeleke kwenye magazeti ya Rostum. Nina hakika watafurahi kuiweka habari hiyo front page. Siyo kuingia JF na kufanya character assassination by innuendo.
Ungewauliza huko huko kibarazani wakupe ripoti kamili kabla ya kukimbilia hapa JF.Nimeuliza swali, jibu swali!
Mmezoea viongozi ambao wanaogopa kusema ukweli na kutoa majibu. Unachotaka kujua ni;
Mbowe Hotel Limite (sio Freeman Mbowe) ilikopa kutoka NSSF shilingi milioni 15 mwaka 1990. Dhamana ya mkopo huo ilikuwa ni nyumba.
Kutokana na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi na ukiritimba wa kununua fedha za kigeni kipindi hicho Mbowe Hotel Ltd ilishindwa kufanikisha mradi iliyoombea mkopo. NSSF walikataa kuisaidia Mbowe Hotel Limited kwa sababu wanazozijua wao badala yake wakaenda mahakamani na kupata hukumu ya upande mmoja ili walipwe. Katika kumkomoa Mh. Freeman Mbowe, Mbunge walidiriki hata kupindisha sheria ili afungwe huku wakijua kabisa si yeye aliyekopa (muulize mwanasheria wenu wa chama kuhusu tofauti ya kampuni na mtu binafsi). Hilo halikufanikiwa.
Kwa kuamini kwamba watamkomoa Mh. Mbowe deni hilo likaachwa likue ili eti wapate hela nyingi au lishindwe kulipika liwe mtaji wa kisiasa.
Mbowe Hotel Limited mpaka sasa imelipa sh. Mil 80 ikiwa ni deni na riba lakini bado NSSF wanataka walipwe zaidi.
Kilichopo ni pande zote mbili kukubaliana sheria inasema nini na nini kifanyike. Hili suala liko wazi na hakuna cha kuficha. Mh. Freeman Mbowe hana anachoficha na hakuna mnachoita dhuluma, ufisadi wala wizi.
Karibu.