Mmezoea viongozi ambao wanaogopa kusema ukweli na kutoa majibu. Unachotaka kujua ni;
Mbowe Hotel Limite (sio Freeman Mbowe) ilikopa kutoka NSSF shilingi milioni 15 mwaka 1990. Dhamana ya mkopo huo ilikuwa ni nyumba.
Kutokana na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi na ukiritimba wa kununua fedha za kigeni kipindi hicho Mbowe Hotel Ltd ilishindwa kufanikisha mradi iliyoombea mkopo. NSSF walikataa kuisaidia Mbowe Hotel Limited kwa sababu wanazozijua wao badala yake wakaenda mahakamani na kupata hukumu ya upande mmoja ili walipwe. Katika kumkomoa Mh. Freeman Mbowe, Mbunge walidiriki hata kupindisha sheria ili afungwe huku wakijua kabisa si yeye aliyekopa (muulize mwanasheria wenu wa chama kuhusu tofauti ya kampuni na mtu binafsi). Hilo halikufanikiwa.
Kwa kuamini kwamba watamkomoa Mh. Mbowe deni hilo likaachwa likue ili eti wapate hela nyingi au lishindwe kulipika liwe mtaji wa kisiasa.
Mbowe Hotel Limited mpaka sasa imelipa sh. Mil 80 ikiwa ni deni na riba lakini bado NSSF wanataka walipwe zaidi.
Kilichopo ni pande zote mbili kukubaliana sheria inasema nini na nini kifanyike. Hili suala liko wazi na hakuna cha kuficha. Mh. Freeman Mbowe hana anachoficha na hakuna mnachoita dhuluma, ufisadi wala wizi.
Karibu.