Tuwe wakweli tu, chadema ni mali ya watu kama ilivyokuwa TANU, CCM, TLP, DP, NLD, NCCR, CUF, nk. Hakuna mtu alimtoa Mwl Nyerere kwenye uwenyekiti hadi pale alipoamua mwenyewe kujitoa na kumpa aliyemuona ataendeleza malengo ya TANU/CCM. Hata mzee Mtei hakuna mtu aliyemshinikiza kutoka uwenyekiti bali alitoka mwenyewe na kumkabidhi Makani, na Makani hivyohivyo alimpa Mbowe kwa hiari yake kwa kumkabidhi mtu aliyedhani anafaa kutimiza malengo. Mbowe nae bila shaka atafanya hivyohivyo kwa mwenyekiti ajae anaemuona ataweza kuendeleza ndoto na malengo ya chama. Hii ya Lissu kutaka kumtoa Mbowe kwa nguvu, matusi na kejeli Mbowe haiwezekani ikawa hivyo. Labda apate baraka za Mzee Edwin Mtei na wanzake waliowekeza mitaji yao hapo. Akina Lissu, Heche, Lema, Mdee, Sugu, Prof Jay na wengine wengi wa aina hiyo tayari wameshafaidika na chadema ya Mtei, hawana lao zaidi ya kuendelea kugombea nafasi za ubunge na Urais kama watateuliwa na kupigiwa kura zitakazotosha.
Huu ndio ukweli mchungu ambao kila mtu lazima aujue. Chadema sio taasisi ya umma kama wanavyotaka kudhani, ina wenyewe na wenyewe hao Lissu hayumo, alikaribishwa tu sana na mwl anavyoweza kukaribishwa kuwa Mkuu wa shule ya mtu binafsi..