Mbowe alianzisha CHADEMA akiwa kijana, Lissu alianzisha nini akiwa kijana?

Mbowe alianzisha CHADEMA akiwa kijana, Lissu alianzisha nini akiwa kijana?

Si mali yake? unajua alitumia fedha kiasi gani kuanzisha chama? kama ni rahisi si muanzishe chenu? Hivi vyama vilianzishwa kama saccos za watu. Hashimu Rungwe alianzisha chake, Cheyo alianzisha chake, Mtikila alianzisha chake, Dovutwa alianzisha chake, Prof. KIGOMA Malima nae alikuwa na chake, Mapalala na Hamadi nae alikuwa na chake, Lyatonga alikuwa na chake, Zito ana chake, Mbowe na Mtei nao wana chao, na wengine wengi. Chadema ni mali ya familia kwa mtaji ya familia. Wapuuzi wanadhani chadema ni mali ya umma wanayoweza kuitolea macho. Chadema kilikupatia ubunge, magari, majumba na ada ya wanao, Kama kimekushinda ondoka katafute kingine. Huwezi kuwa mlevi ukanywa na kulewa bangi na kumwambia Hashim Rungwe ondoka kwenye chama chako cha UMMA party kwakuwa umekaa sana na umezeeka, utakuwa mpuuzi kwelikweli.

HAWA BAVICHA lazima wafundishwe historia ya chama wanachokipigania kabla hawajaropoka.
Wewe tuondolee upuuzi wako kama hujui historia ya Chadema kaa kimya. Eti unabana pua kabisa Mbowe alianzisha Chadema akiwa kijana,wadanganye walugaluga wenzako huko CCM.
 
Lissu kaanzisha majungu.

Watu wengi hasa vijana hawajui kwamba CDM muasisi wake ni Freeman Alkael Mbowe the Great.

Yaani kwa CDM fanya siasa zako zoote ila ukimdharau Mbowe we ni dog tu.
Ila kuendekeza utumwa kwa Samiah na Abdul ni sahihi?
 
Mtoa mada kama hujui historia ya chama kakaa kimyaa..usituletee mambo ya bichwa biringanya.
 
Chama cha CDM kilianzishwa na waasisi 10 kasome documents na katika watu hao Mwamba Alkael Mbowe akiwa na miaka 30 tu alikuwa among them.

Hapendi kusema sema saana uasisi wake ila watu makini sisi tunajua.

Huyu jamaa ropo mpaka leo hana hata ka kampuni kadogo ka uwakili.

Tunasema Lissu bila Mbowe ni debe tupu
Fuso nilikupenda sana tena sana ila kwa hili hapana siasa za kum attack mtu na kumshushia utu wake hazifai hata kama anakukwaza.
 
Wewe umeanzisha nini?
Jitokeze tujue na si kujificha kwa I'd bandia hapa jf
mimi sigombei, ninaongea facts tu. Uonozi sio ulopolopo wa kuongea chochote kinachokujia kichwani na moyoni. Kiongozi bora ni yule anaeheshimu katiba kama ilivyo na kazi za viongozi wa nchi kwa mujibu wa katiba, kisha anaongea na kutenda bila kuathili kesho yake, ya wezake na taifa lake.

Ogopa kuchagua kiongozi asiyekuwa na sera. Trump alimshinda Biden kwa sera zake juu ya Ukraine, wahamiaji, uchumi (kodi, tozo) na namna atakavyoshusha mfumko wa bei. Mgombea wetu yeye sera yake ni wamasai wasihame wazae na wanyama, bandari iendelee na status quo. Hatuambii wapi mazo yetu yataenda kwenye masoko ya wazungu bila ubaguzi, hasemi madini yetu tutayachimbaje wenyewe na masoko ya kuyauza, hasemi kwenye kilimo atafanye. Anachotaka ni kuifulusha CCM madarakani tu na kwenda yeye kukaa Ikulu kama alivyofanya Tshishiked na willium Ruto. Kabila alishindwa na yeye anashindwa, Kenyatta alishindwa na Ruto anashindwa vilevile kuwasogeza wananchi.
 
Fuso nilikupenda sana tena sana ila kwa hili hapana siasa za kum attack mtu na kumshushia utu wake hazifai hata kama anakukwaza.
Amekosea wapi hapo, unataka kupingana na fact? Kwanini ilikuwa rahisi Mtei kumwachia kijiti Bob Makani na kwanini ilikuwa rahisi baada ya Bob Makani akaachiwa Mbowe? Na mbowe ana maagizo juu ya mwenyekiti ajae; kama hupendi hivyo nenda kaanzishe chako ili roporopo itamalaki bila kuhojiwa. They can not let their party (investment) go to the dogs. Ndio maana Mbowe anasema bado ana ndoto ambayo haijatimia bado. Na ndoto ndio inayoongoza kwenye kuanzisha taasisi yoyote ile duniani. Lissu inaifahamu hiyo ndoto iliyokianzisha cdm? Huwezi kupata uwenyekiti kwa harakati kama anavyotaka kufanya Lissu. Lazima foundation ya chadema imkabidhi mtu atakaendeleza pale alipoachia Mtei, Makani na Mbowe kwa mujibu wa Vision ya kweli ya chama. Chadema, TLP, NCCR, Dovutwa na vingine havikuwa vyama vya kwenda Ikulu bali kutimiza matakwa ya vyama vingi na kuipasha joto CCM isipoe katika kuwahudumia watanzania. Ndiyo maana Mwl. Nyerere alikitaka cdm kuweka nguvu zake kwenye kupata idadi kubwa ya wabunge bungeni kuliko kwenda Ikulu.
 
Nyie UWT mapenzi yameanza lini kwa Mbowe?
Mtei, Makini na Mbowe hawajawazi kuitukana CCM wala kukashifu viongozi wakuu wa nchi. Dr. Slaa ni CCM kindakindaki, Mtei ni CCM kindakindaki. Haitakubalika cdm iangukie mikononi mwa Lissu ili kivunjike. Hana uzoefu wa skills za kuongoza taasisi hata ndogo tu sembuse chadema. Wanaomuunga mkono Lissu hata wao wanafanya hivyo kwa mihemko tu na kutokujua siasa ni nini. Kwenye siasa hakuna adui na rafiki wa kudumu, lakini Lissu na uadui wa kudumu moyoni na kichwani. hakuna siasa za hivyo duniani.
 
Tuongee kwa mifano, wewe ulianzisha nini kama hao uliowataja ili tuige?

View attachment 3200866
Mbowe alianzisha chadema! chadema ilianzishwa na Mzee Mtei sasa hv ana miaka 90+?
Ukisema vitu kuangslia umri,Nyerere alianzisha ccm akiwa na miaka 32! Wewe umeanzisha nini? We ulikuwepo wakati nyerere anaanzisha chama! Sio kila mtu lazima aanzishe vysma, vipo vitu vingi tu vya kufanya, haya tuambie Eron musk, Mark Zuckerberg, Walianzisha vysma gani? Je wazee kina Washington, Jimmy Carter walikuwa Bora ujanani kwao kuliko ko vijsna hawa wa sasa! Tumia bongo kuwa za kwa mapana, usiende kwa upepo
 
Wewe tuondolee upuuzi wako kama hujui historia ya Chadema kaa kimya. Eti unabana pua kabisa Mbowe alianzisha Chadema akiwa kijana,wadanganye walugaluga wenzako huko CCM.
Mzee Mtei yungali hai, nendeni mkapate maoni yake.
 
Chama kipi kakianzisha Mbowe? CHADEMA ilioanzishwa na Akina BOB MAKANI na EDWIN MTEI. Mzee Bob Makani akiwa Mwenyekiti wa pili ya CHDEMA. Mbowe karithishwa chama baada ya kuoa kwa Edwin Mtei kama Mkwe.
Ona sasa hata wewe unathibitisha kuwa cdm ni taasisi ya kifamilia; mwambie Lissu nae akaoe mjukuu wa Edwin Mtei kwanza. Kwanini hakurithishwa Lissu au kaka yake Lissu? Kwanini Mtei hampokonyi Mbowe uwenyekiti baada ya kukaa miaka 21? Kama umeichoka cdm na mambo yake toka nenda chama kingine au anzisha chako na mkweo.
 
Watu wamesikia Mbowe kadakishwa b12 basi kila mtu anaandika kumpamba kwa matumaini ya kurushiwa chochote.
 
Nenda wewe ambaye hujui ukweli
Kanuni iko hivi; kama wewe uko chadema na unaiunga mkono chadema malipo yako pekee ni kuwa cdm itakusaidia kupata ubunge, udiwani, uwenyekiti wa serikali za mitaa au Urais kama ikibidi kwakuwa huwezi kuvipata hivyo bila kupitia chama cha siasa, na wengi wamefaidika kuyapata hayo, lakini hakuna kingine. Kama ukichoka na taratibu za cdm toka uende kwingine lakini sio kuitamani cdm iwe yako. Huu ni uwekezaji sawa na uwekezaji mwingine. Hata Zuberi Kabwe atamwachia uwenyekiti mtu anaemwamini sawasawa, sio kila mtu. Ndiyo maana hata CCM walikuwa wakisemaga kuwa CCM ina wenyewe, na cdm ina wenyewe vilevile.
 
Kanuni iko hivi; kama wewe uko chadema na unaiunga mkono chadema malipo yako pekee ni kuwa cdm itakusaidia kupata ubunge, udiwani, uwenyekiti wa serikali za mitaa au Urais kama ikibidi kwakuwa huwezi kuvipata hivyo bila kupitia chama cha siasa, na wengi wamefaidika kuyapata hayo, lakini hakuna kingine. Kama ukichoka na taratibu za cdm toka uende kwingine lakini sio kuitamani cdm iwe yako. Huu ni uwekezaji sawa na uwekezaji mwingine. Hata Zuberi Kabwe atamwachia uwenyekiti mtu anaemwamini sawasawa, sio kila mtu.
Huu ni utopia tu unaongea naamua kukupuuza. Ila kwa uhakika kabisa Sultan wenu anakwenda na maji.
 
Watu wamesikia Mbowe kadakishwa b12 basi kila mtu anaandika kumpamba kwa matumaini ya kurushiwa chochote.
cdm ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine. Ni sawa na kusikia Azam kapata faida ya 1Trilion, halafu mfanyakazi kama Hashim Ibwe aseme mzee Bakhresa aondoke ni mzee ili nao wao wafaidi kidogo hiyo pesa. Mzee Lyatonga alikuwa akiifaidi saccos yake ya TLP, why not Mzee Mtei, Makani na Mbowe? unajua kuwa mzee Mtei anapatiwa gawio la sh. ngapi kutokana na uwekezaji wake huu wa cdm?
 
Huu ni utopia tu unaongea naamua kukupuuza. Ila kwa uhakika kabisa Sultan wenu anakwenda na maji.
Ni heri chama kife kuliko Lissu kuwa mwenyekiti, we unacheza nini. Nani mjinga aanzishe taasisi yake halafu ichukuliwe kiboya kwa kejeli na matusi.
 
Back
Top Bottom