Mbowe aliiweka Chadema rehani kwa Samia. Sisi tulimuuliza kwani kuna shida gani mzee? Mbona uwezo tunao huku ukituweka rehani?

Ndio maana wapambe na chawa wake wanahaha
Kuna 12b wametengewa wakiweza kumuondoa Lissu kwenye siasa kabisa,yaani asiwe mwenyekiti na asipewe nafasi ya kugombea urais. Hiyo 12b imewatoa ufahamu wengi sana ndiyo maana threads za kumponda Lissu hazikauki kila baada ya dakika tano zinazalishwa .
 
Muarobaini wa matatizo katika vyama vya siasa ni Kuruhusu Mgombea huru
 
Hakika wewe umeongea. Anachokifanya Lisu na wafuasi wake ni kuiua Chadema na wala si kampeni kwa nia ya uchaguzi uliosafi. Hata Lisu akishinda uchaguzi huu, hakika Chadema haiwezi kuwa moja tena kutokana na majeraha wanayosababisha. Lisu namfananisha na Mabere Marando wa enzi za NCCR. Ameamua kupasua Chama kwa maslahi binafsi au Ego yake tu.
 
Huo uwezo mbona hatujauona kwenye uchavuzi wa serikali za mitaa?
 
GSam, hakika wewe ni mtu niliyekuheshimu sana hapa jukwaani kwa hoja zako Murua. Ila kwa hili naona kama unapotoka vile. Mbowe asichukuliwe kama Mungu bali binadamu ambaye anakosea na kuweza kukosolewa kupitia machineries za chama. Nionacho hapa ni utovu wa nidhamu kwa wote wanaomfanyia kampeni Lisu wakiongozwa na yeye mwenyewe. Wanachokifanya hakina tofauti na Mabere Marando wa NCCR miaka ile. Nadhani wewe ulikuwa kijana mdogo sana kuweza kushuhudia ile minyukano. Kwa mantiki hiyo usitegemee Chadema iliyomoja chini ya Uenyekiti wa Lisu. Lisu ni mtu egoistic sana kiasi kwamba yuko tayari kuanika mambo ya ndani ya Chama kwa maslahi yake binafsi. Namuona kama mtu aliyeamua kugawana fito za nyumba na si vinginevyo. Na huo ndio utakuwa mwisho wa Chadema, belieave me or not.
 
Lissu akiwa mwenyekiti wala rushwa watamuogopa ,wakimwita gizani kuteta naye kumrubuni,asubuhi peupe anaongea yote kinagaubaga. LISSU OYEEEE...
 
Inasikitisha sana
 
Ndugu yangu napenda kukupa Taarifa Kwamba, Kesi ya Ugaidi ya Mbowe ilikuwa na ushaidi mwingi sana. Ndiyo Sababu Mbowe anamshukuru sana Samia Kwa Msamaha wake!
Kuna siku Mama Samia alisema maneno kuhisi hiyo case watu wanalalamika kaonewa ooh ni siasa akasema subilini muone mahakama si zipo so evidence against him kwenye case ya ugaidi was seem/ deemed strong kiasi Mbowe angekutwa na hatia so analipa fadhila
 
Mlipoambiwa Mbowe kapokea pesa kwa Lowassa mlitutukana Sasa hivi ndio mnaona ukweli.
 
Mbowe kweli alikengeushwa na niliyoandika aliyafanya. Mbowe huyu sie yule tuliyemuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…