Toka 2022 ndio watu wanajitokeza leo kuanika "dhambi" za Mbowe? Hayo mapendekezo yalitoka kwa nani? Kama ni kutoka kwa CCM, alifanya kosa gani kuwashirikisha wenzake? Hayo yalikuwa ni mapendekezo ambayo Kamati Kuu ilikuwa na mamlaka ya kuyakataa na nadhani ndivyo ilivyokuwa. Sidhani kama Mbowe angekubali kupewa majimbo 20 maana kwa experience yake ni lazima alijua kuwa kuna uwezekano mkubwa wa CCM kumgeuka kwa ama kutoruhusu CDM washinde kama walivyo ahidi ( mfano ni NCCR Mageuzi) ama watatoa nje makubaliano hayo ili wakimalize kabisa chama chake. Mbowe sio mjinga kiasi hicho.
Mimi ninavyojua ni kuwa Lissu alitangaza nia ya kugombea urais kama chama chake kitampa idhini. Sijamsikia Mbowe akisema lolote kuhusu hilo. Kama angekuwa hataki angeweza kusema kuwa ametangaza nia mapema mno. Na mpaka hivi karibuni Lissu alikuwa anasisitiza kuwa yeye nia yake ni kugombea umakamu Mwenyekiti na urais tu. Kama alifanya hivyo huku akijua kuhusu usaliti mkubwa wa Mbowe basi tatizo litakuwa lake. Wenje amezungumzia tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mbowe za kuhongwa magari mawili ambayo kiukweli aliyanunua katika mnada. Mpaka sasa hivi hatujaelezwa kama ni kweli tuhuma zilitolewa na kama zilikuwa za kweli.
Ninavyojua mimi ni kuwa strategists wengi wa vyama vya siasa huwa wanaangalia ni sehemu gani ndiko wana uhakika zaidi wa kushinda, na huko ndiko wanaweka nguvu kubwa. K.m. sio rahisi kwa Chadema kushinda Pemba na Mafia kwa hiyo itakuwa busara zaidi kuwekeza zaidi kwenye majimbo ya Mbeya, Mara n.k.
Hivi karibuni pamejitokeza tuhuma za ajabu ajabu kutoka kwa watu wanaodai wako jikoni. Kuna wanaodai walizuiwa na watu wa Mbowe kugawa kompyuta na kadhalika. Humu ndani wamejaa watu ambao wanaamini wakimchafua Mbowe ndio mtu wao atashinda na chama chao kitaingia kwenye era mpya ya mafanikio.
Nashauri wanyamaze. Kama wana ushahidi wa tuhuma hizo wazikabidhi kwa Kamati Kuu. Kama hawana imani nayo basi wamfanyie kampeni safi mgombea wao ili ashinde bila kukivuruga chama zaidi. Akishinda, wataweza kuzifuatilia na kuzichukulia hatua stahiki. Haya wanayofanya ni kwa faida ya wapinzani wao na sio chama chao.
Amandla...