Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Yaan huwa sitaki kuamini Mbowe ni mwenyekiti,,elimu hana,opportunist mkubwa na hana sera zozote za maana.
Team Zitto
 
Hapa CHADEMA lazima tukiri bila kuutawala ulimwengu wa Media ili kuyafikisha mawazo ya Chama kwa umma mpana zaidi,ili kuhubiri sera za Chama,ili watu kuijua historia na mashujaa wa Chama ili kuwafanya Wananchi wajihisi wao ni sehemu ya CHADEMA,ili kuelezea malengo na madhumuni ya Chama kwa Watanzania na Tanzania kwa ujumla basi tusije kushangaa Chama Tawala kikirejea madarakani 2015.Nimependa mikakati iliyofanywa na uongozi wa sasa katika kukiimarisha Chama lakini nadhani ni wakati muafaka kwa Chama kama kutakuwa Uchaguzi wa ndani mwaka huu basi tutoe nafasi kwa watu wengine wenye sifa kugombea na wachaguliwe ili waje na mikakati mipya ya kupapambana dhidi ya Chama cha Mapinduzi nadhani mapambano ya kwenye media yatakuwa bora zaidi dhidi ya CCM kitu ambacho kinapuuzwa na Uongozi wa sasa.
 
mbona sikuelewi? dhana ya kupokezana vijiti ni safi kabisa. LAKINI, MBONA huwaambii CCM wenzako kuwa wakabidhi nchi kwa wengine nao waongoze? au dhana ya kupokezana vijiti ni kwa Chadema tu? mbona husemi kuna watu ndani ya CCM toka Enzi za mwalimu mpaka sasa bado wamekalia madaraka hadi wanaota kutu, hiyo huoni? Acha unafiki
 
Kama mtoa maoni, ulianza vizuri kiasi nikadhani kuna kitu twaweza pata toka kwenye maoni yako but umekuja kuharibu paragraph mbili Za mwisho.
 
Ukiacha ushabiki wa kijinga na akili za kushikishwa, hoja yako ni nzito na umeona mbali. Tatizo wengi wetu ndani ya CDM hatujitegemei kimawazo linapokuja swala la kujadili mambo ya uongozi ndani ya CDM. Ukitaka kuwafurahisha watu hapa sifa Mbowe, Slaa, halafu ponda Zitto.

Umenifungua macho sana kuhusu media. Nilikuwa najiuliza sana kwa nini CDM hawataki kuanzisha media zao. I see the point.
 

Mawazo kama haya ni mfu na lengo kubwa ni kubomoa chama. Ujinga unaofanywa na ccm na cdm mnataka muufanye. Badilikeni jamani acheni kusema mbona ccm hawako hivi. Badaye mkipewa nchi mtakuwa mnaiba, mkiulizwa mtasema mbona na ccm walikuwa wanaiba. Jitambueni..
 
Ni wazo zuri mkuu kwa sababu cdm wanahubiri democracy na wanadai wao ni zaid ya ccm. Wanapaswa kuonesha democracy kwa vitendo ndani ya chama na sisi tutakuwa na imani na wanachokisema majukwaani. Tofauti na hapo ni propaganda zilezile...
 
heading inaonyesha Mbowe amepoteza sifa , ndani haionyeshi kama amepoteza sifa au kitu kingine chochote ! Sijakuelewa , kama kupoteza sifa maana yake ni kukipeleka chama juu basi tuendelee naye , kuanzisha media za cdm ni wazo zuri bali kuna kitu usichokijua , mchakato wa vibali unaweza kuchukua hata miaka 10 ! usiulize kwanini .
 

Point zako hazieleweki;anyway kila mtu ana fikra zake. Huenda utakuja na hoja badae
 
Mkuu,

Nikupongeze kwa kuwa huru na kuachana na utumwa wa fikra kama walivyo mashabiki wengine.

Hoja yako ni ya msingi sana, na nitoe rai yangu kwa wana CHADEMA kusu uhuru wa mawazo, ni vyema ukawa huru.

Kwa mwana CCM yeyote suala la Mbowe kuondoka katika safu ya uongozi CDM ni furaha tele. Kamanda anawanyima raha kweli kweli. Hatoki mtu hapo mpaka kazi ya kuikomboa nchi toka kwenye makucha ya mafisadi imekamilka. Endeleeni kusubiri ni lazima mngooke safari hii. Hatuna mchezo na hatudanganyiki.
 
Yaani hawa jamaa akili zao hazina kumbukumbu kabisa maana toka mfumo wa vyama vingi uanza CDM imetoa wenyevitu na CCM toka ianzishwe imetoa wenyeviti 4 tu.
 
Namuomba KITILA atagombea na yeye nafasi ya mwenyekiti, mshikaji anamachungu na ukomboz wa Taifa hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…