Hili tulishalidokeza siku nyingi; labda tu ni kwa vile haikuanzishwa kama mada.
Dalili zote zinaonyesha kwamba siasa za Kenya ndizo zinazokuja kujaribiwa Tanzania.
Ni kama Tanzania siku hizi inaiga kila kitu kinachofanyika Kenya; iwe ukulima wa parachichi, nasi tunakimbilia kuiga; kuzungumza kiingereza, nasi tunataka tuwe kama wao. Wakisema wao wanawatambua 'diaspora' wao kwa kiwango fulani, nasi tunatafuta kuhimiza watu wetu watoke kwenda nje;, kana kwamba hapa kwetu hakuna fursavtele ambazo vijana wetu hawa wanaweza kuzitumia kujenga taifa lao kwa ufanisi.
Tumekuwa watu wa kuiga tu kila kitu, hatuna ubunifu wowote tunaoweza kujivunia...; la hasha; nisisahau Kiswahili chetu na taasisi yetu iliyofanya kazi nzuri sana BAKITA.
Nje ya hapo, ninaomba kukumbushwa eneo jingine tunaloweza kujivunia katika kulifanya vizuri.
Lakini naomba usinitajie udumu wa CCM kwenye madaraka, kama mfano.