Mwaka 2015 nikiwa na ID nyingine kongwe niliwahi kuandika kuhusu Lowasa anapanga kukimbilia chadema baada ya kutemwa ccm. Wapo walionishambulia, walionipinga na walioandika kama wewe hivi. Vigezo vyao vilikuwa kwamba Lowasa ni fisadi kwahiyo isingekuwa rahisi kukubaliwa kujiunga na watu wasafi (chadema ya wakati huo) wengine walisema chadema kamwe hawezi kushirikiana na mafisadi papa kama vile Lowasa na wengineo, eti ni mara kumi chadema inaweza kushirikiana na mchawi lakini sio fisadi Lowasa.
Kifupi maneno yalikuwa mengi sana kwenye uzi ule, ila baada ya siku kidogo za usoni akahamia na cha kuchekesha zaidi akapewa nafasi ya kugombea uraisi. Nilivyofufua uzi nikakuta wengi wameshakimbia ID zao kutokana na aibu ya maneno yao waliyoandika kabla hajahamia chadema, wengine wakaanza kuandika visingizio mbali mbali ambavyo havikuwa hata na mashiko.
So kwahiyo hata wewe ulieandika hivi sikushangai, muda ukifika wa Mbowe kuteuliwa, wewe utapotea kama walivyopotea wale wa 2015. Hii ndio siasa ya bongo.