Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuondoa Mkataba huo kwenye majadiliano Bungeni kwasababu unakwenda kuiingiza Nchi kwenye migogoro usio na faida.
Pia, amewataka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, Plasduce Mikeli Mbossa kujitafakari kama wana hadi ya kuendelea kubaki kwenye ofisi za Umma kutokana na kuiingiza Nchi kwenye Mkataba huo.
Aidha, amesema ifike wakati sasa badala ya kutoa Kinga kwa Viongozi, wengine waanze kushtakiwa kwa makosa wanayofanya kwa kutumia Mamlaka yao vibaya na kuiingiza Nchi katika mikataba ya ovyo.