Mbowe: Bunge likipitisha Mkataba wa DP World, tutaamsha Nchi nzima

Mbowe: Bunge likipitisha Mkataba wa DP World, tutaamsha Nchi nzima

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuondoa Mkataba huo kwenye majadiliano Bungeni kwasababu unakwenda kuiingiza Nchi kwenye migogoro usio na faida.

Pia, amewataka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, Plasduce Mikeli Mbossa kujitafakari kama wana hadi ya kuendelea kubaki kwenye ofisi za Umma kutokana na kuiingiza Nchi kwenye Mkataba huo.

Aidha, amesema ifike wakati sasa badala ya kutoa Kinga kwa Viongozi, wengine waanze kushtakiwa kwa makosa wanayofanya kwa kutumia Mamlaka yao vibaya na kuiingiza Nchi katika mikataba ya ovyo.
Naomba Bunge wapitishe huu mkataba na Nasubiria Kwa hamu na gamu waliamshwe Nitakuwa paleee nasikilizia..

Ila naona Bunge litajadili wee na kusema Serikali ikafanye maboresho kama ilivyokuwa Kwa mswada wa bima ya Afya Kwa wote umeshakufa kibudu..
 
ukitaka kujua watanganyika wana dukuduku, mbowe afanye hivyo halafu uone idadi ya watu watakaokuwa nyuma yake, hapo ndipo utajua kumbe tanganyika bado inaishi mioyoni mwa watu.
Akithibutu ndio mwisho wake, ajenge hoja kwa muktadha wa kujenga sio kueneza chuki za kikabila.
Tutamtegua kiuno.
 
Wewe mwenyewe akili ya kuuchambua mkataba Na udhaifu wake hujui kazi kufuata upepo tuu
Daah mkuu mbona umenivamia kwani mimi nilienda Dubai na wakina Msukuma au unataka nichambue nini ili uelewe...sihitaji kujisifia akili wakati Taifa linatapeliwa na wenye akili wapo Kimya tuu...
 
Hivi nyie Machadema mnatuonaje ss Watz mmetuibia hela za join the chain sahz mpo fyokofyoko
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameitaka Serikali kuondoa Mkataba huo kwenye majadiliano Bungeni kwasababu unakwenda kuiingiza Nchi kwenye migogoro usio na faida.

Pia, amewataka Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari, Plasduce Mikeli Mbossa kujitafakari kama wana hadi ya kuendelea kubaki kwenye ofisi za Umma kutokana na kuiingiza Nchi kwenye Mkataba huo.

Aidha, amesema ifike wakati sasa badala ya kutoa Kinga kwa Viongozi, wengine waanze kushtakiwa kwa makosa wanayofanya kwa kutumia Mamlaka yao vibaya na kuiingiza Nchi katika mikataba ya ovyo.
Mkiingia mitaani tutawapa kipigo cha mbwa koko. Credit: Afande Muroto
 
Hizo nguvu nenda ukalimie maharage na mahindi [emoji706]
Watu wa aina yako hawawezi kujitetea kwa lolote. Ukikuta hata mshedede umetinga kwako waweza kusema malizia bwana niendelee na shughuli zingine. Hata ukipiganiwa huthamini.
 
Watu wa aina yako hawawezi kujitetea kwa lolote. Ukikuta hata mshedede umetinga kwako waweza kusema malizia bwana niendelee na shughuli zingine. Hata ukipiganiwa huthamini.
Nyie chadema mnapenda sana kuzungumzia Mambo ya ushoga...vp viongozi wenu walio enda ujerumani wamerudi?
 
Kaandamane wewe, mi sitaandamana mana sifaidiki na kitu.
Nitaandamana siku mtoto au wadogo au wazazi wangu wakiuliwa, nitaandamana mwenyewe.

Nitaandamana pale tutapovamiwa kivita.

Itasaidia nini kuandamana mkuu wakati ushavamiwa? Na pengine ushapoteza wapendwa wako” ngoja tuone hili lina kwendaje
 
Back
Top Bottom