Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Huyu jamaa anaua upinzani, yaani jana tu katoka kusema anamuunga mkono mama then leo tena hawatashiriki uchaguzi. Chadema mwangalieni huyu mwenyekiti.
Hivyo nivitu viwili tofauti mbona kumuunga mkono Kwa mambo Fulani lkn sio Kwa mambo ya katiba
 
Katika hatua nyingine, Mbowe, alimpongeza Rais Samia kwa kile ambacho alikiita kurudisha tabasamu na matumaini kwa wananchi akidai walipoteza imani na viongozi kutokana na baadhi ya mambo maovu.
Yaani hapa Mbowe amenena, siku 60 na kadhaa tayari nina tabasamu hasa nikifiria kupanda daraja mwezi wa sita na vile vicopy vya barua za Chamwino vya kupandisha madaraja with effective from 91/06/2021 vinavyosambaa mitaondaoni ndio vinanipa hamasa kabisaaa.

Alafu nikifikiria kuondolewa ile dhulma ya 6% ya Bodi ya mikopo pamoja na faini yake ya 10% jumlisha ahadi tamu ya kupandishiwa mshahara mwakani,mie ni kumwemwesa shavu tu....

I love you Madame President.
 
YOTE namwachia Mungu, kama ilivyokuwa kwa Mwendazake alipokuwa anajiandaa kutawala milele. Mungu wa haki atauleta mkono wake. AMEN
Hata Mbowe hatakuwa mwenyekiti milele pamoja na kwamba anauwa wenzake wanaojaribu kugombea uenyekiti
 
Katiba mpya ni agenda ya kina Mbowe kwa manufaa ya matumbo yao tu basi
 
Uchaguzi wa kidemokrasia bila Tume huru? Wachekesha sana wewe. Si itawasaidia muweze kupata nafasi ya kuokoteza wa kuunda Covid # wengine.
 
Huyu jamaa anaua upinzani, yaani jana tu katoka kusema anamuunga mkono mama then leo tena hawatashiriki uchaguzi. Chadema mwangalieni huyu mwenyekiti.
Mbona unaandika kwa mihemuko husomi habari yote?Kampongeza mama kwa kurudisha tabasamu kwa Watanzania
 
Uchaguzi wa kidemokrasia bila Tume huru? Wachekesha sana wewe. Si itawasaidia muweze kupata nafasi ya kuokoteza wa kuunda Covid # wengine.
Wakina MBOWE, LISSU , LEMA na wengine wengi walishakua wabunge tena wengine wa muda mrefu tu kwa TUME hii ambayo wanapigia kelele sasa waulize mbona walipokuwa wabunge hawakukataa kwa sababu TUME haikuwa huru? mtu kashindwa uchaguzi na kushindwa kujibu maswali juu ya rufaa ya COVID 19 anakimbilia kujificha kwenye kichaka cha TUME HURU na nyie mnaishia tu kushangilia acheni kushikiwa akili na Mbowe mwenzenu anawacheka tu
 
Ni fursa kwa Act wazalendo kuwa chama kikuu cha upinzani chenye nguvu, kufa kufaana... Chama kinajiita demokrasia na maendeleo lakini kina mwenyekiti wa maisha ina maana hakuna mwenye uwezo wa kuongoza zaidi yake?
Akipewa nafasi ya Uraisi huyu si atabadili katiba awe mfalme kabisa.
 
Nyumbu ni taabu sana
 
Nyumbu hawatambui hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…