Hapa ndiyo tutaona umuhimu wa upinzani. Upinzani unapoipa kashi kashi serikali, basi serikali inatafuta mlango wa kutokea ambapo wananchi hunufaika au kupata hasara. Ila kwa utawala wa mama, kashi kashi za wapinzani kwa serikali zitawanufaisha wananchi.
Nachomaanisha, kwa vyovyote vile, mama President + CCM hawawezi kuruhusu katiba mpya. Hivyo, mama atakachokifanya ni kukimbilia kwa wananchi na kuwatimizia yale wanayoyataka ili wawaunge mkono CCM. Na kwa kuwa Watanzania huwa tunangalia matumbo yetu bila kuangalia future, basi mama ataongeza mishahara, atapunguza kodi, atatoa ajira, na mambo mengine mazuri. Hii itaisaidia CCM kwa sababu wananchi hawatawasikiliza sana wapinzani. Wananchi wanajali Ugali wao!