Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Ubaya ni kwamba chama cha upinzani si kimoja kwa sasa. Vyama vingine vikishiriki show inapigwa tena kali mno na kijani inabaki madarakani.
Yes Zito Kabwe atashiriki na chama chake kitashinda na kuwa chama kikuu cha upinzani nchini
 
Mbna iblis na farao wanazungumziwa kila kukicha????
Angekuwa hapendwi mgekuwa mnamuongelea hadi leo? Imagine mtu ana miezi 3 kaburini lakini kila siku ni kumjadili yeye tu.

Mzee aliwashika pabaya wafanyabiashara kanjanja msiolipa Kodi, wauza ngada, misheni town, vyeti feki, wahujumu uchumi, Wala rushwa na mafisadi. Kwa hasira mlizo nazo sishangai mtaendelea kumuongelea kwa miaka mingi ijayo.
 
Hivi nyie binadam wenzangu mpoje mnajuaje Kama mama Samia at survive mpaka 25
sio tu ku survive!,wanajuaje 2025yr,atagombea SSH!? wanahangaika tu nao hawa.muda hutoa majibu yote!tuliwaambia mbowe sio kabisa,ni dalali.wakawa wanang'aka humu.
 
Tutashitakiwa MIGA
20210601_075916.jpg
 
Swala la katiba mpya linakuwa shida kwa sababu ccm wanafahamu fika kwa asilimia mia moja kwamba hii katiba yao ndio mungu wao na kwamba siku isipokuwepo na wao hawatakuwepo.

Lakini siku wazungu wakitaka Tanzania ipate katiba mpya, tutaipata ndani ya masaa 24 tu. Walipotaka mabadiliko ya urais yafanyike yamefanyika mara moja na rais aliyeko kama hawezi kuelewa somo basi zoezi linaweza kurudiwa.
 
Oya tujenge uchumi wadau

Ujenz unaanzia chin tudai marekebisho ya sheria ndogondogo znazotunyonya kila siku zkishughulikiwa tuendlee na nyingne.
 
Oya tujenge uchumi wadau

Ujenz unaanzia chin tudai marekebisho ya sheria ndogondogo znazotunyonya kila siku zkishughulikiwa tuendlee na nyingne.
Sheria zipi hizo
 
Ninaelekea kukubaliana na wewe katika hili.

Mbowe kasema wanakwenda kwa wananchi kulielezea hili la katiba mpya.

Matumaini yangu makubwa ni kwamba watakapolipeleka swala hili kulieleza kwa wananchi watakuwa na ushawishi mkubwa wa kuwaelimisha wananchi hayo haya uliyoyaandika hapa wewe, ili wananchi watoe shaka yote juu ya nani anayeng'ang'ania katiba mbovu na kwa sababu zipi.

Wananchi ni lazima waelewe vyema kabisa kuhusu swala hili la katiba mpya na kwa nini kuna chama hakitaki iwepo katiba mpya.

CHADEMA wakifanikiwa kuifanya kazi hiyo muhimu ya kuwaelimisha wananchi, hapo sasa kazi yao itabaki kuongoza juhudi za wananchi wenyewe kuitafuta katiba mpya.
CHADEMA wasipofanikiwa kuwavuta wananchi juu ya swala hilo, hakuna lolote litakalobadilika hiyo 2021.

CHADEMA ni lazima wajizatiti kufanya kazi hii ngumu, lakini muhimu sana kwa ushirikiano na wananchi.

Leo na 2025, hakuna muda mwingi. KAZI INAPASHWA KUANZA MARA MOJA.
Shida nayoiona Chadema wanataka katiba mpya ya Taifa lakini Katiba ya Chadema inampa mwanya mtu moja tu kuwa Mkiti miaka yote kwanini?
 
100% Nakubaliana na Mbowe; the only solution kwa kile wanachokitafuta Vyama Mbadala ni Kupambana usiku na Mchana kudai Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi. Mengine yote ni Mbwembwe tu Itakaa Ikatokea hapa Tanzania kwa Wapinzani Kuingia Ikulu kwa tume hizi za CCM.

However, Main objective ya Opposition ni Kuongoza nchi, but inapokuwa Imeshindikana au Kura hazijatosha kwa sababu yoyoteile basi uwakilishi wao bungeni ulete Tija katika Jamii. Mh. Mbowe, Mnyika plus your people kaza boot (Kudai Haki Kuna gharama Zake) it's never too late and not ease task to pursue.
Mbowe huwa ana hekima iliyo kubwa kuzidi umri wake. Ninaona mkakati wake hapa anaiangalia 2030 kwa sababu anajua kwa sasa hivi hayuko sawa sana kwa ajili ya 2025. Kwa hiyo anaamua kuiachia 2025 but at a price ambayo inaweza kuja kumlipa 2030 kama atafanikiwa kujiweka sawa kati ya 2025 na 2030. Ni option moja ya busara sana na iliyotumia hekima ya hali ya juu sana. Wapinzani wake inabidi waiangalie option hii kwa jicho la hekima sana

Kuna siku mwaka jana aliwahi kusema "tarehe 01/04/2020 tunaanza mikutano ya kisiasa nchi nzima" lakini wakati huo huo karibia dunia nzima ilikuwa inaingia kwenye lockdown. Mbowe huwa wakati mwingine anatumiwa kutabiri matukio yajayo. Ni mtu mwenye hekima tu anayeweza kutumiwa na Mungu kwa namna hiii
 
Huwa mnajipa moyo sana
 
Huwa mnajipa moyo sana
Akina nani, sisi wapinzani?
Tunaweza pia tusiwe ni wapinzani, ila watu ambao tunazijua fair grounds za kisiasa kiasi kwamba huwa tunatoa ushauri kwa kuangalia mazingira halisi namna yalivyo pasipo kuwa na ushabiki wowote ule wa kisiasa
 
Mbowe huwa ana hekima iliyo kubwa kuzidi umri wake. Ninaona mkakati wake hapa anaiangalia 2030 kwa sababu anajua kwa sasa hivi hayuko sawa sana kwa ajili ya 2025. Kwa hiyo anaamua kuiachia 2025 but at a price ambayo inaweza kuja kumlipa 2030 kama atafanikiwa kujiweka sawa kati ya 2025 na 2030. Ni option moja ya busara sana na iliyotumia hekima ya hali ya juu sana. Wapinzani wake inabidi waiangalie option hii kwa jicho la hekima sana

Kuna siku mwaka jana aliwahi kusema "tarehe 01/04/2020 tunaanza mikutano ya kisiasa nchi nzima" lakini wakati huo huo karibia dunia nzima ilikuwa inaingia kwenye lockdown. Mbowe huwa wakati mwingine anatumiwa kutabiri matukio yajayo. Ni mtu mwenye hekima tu anayeweza kutumiwa na Mungu kwa namna hiii
Aisee. Wafuasi wa Mbowe mna matatizo ya akili.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameenda kinyume na Lisu kwa kutangaza kuwa Chadema haitashiriki uchaguzi mkuu nchini wa mwaka 2025, hivyo kumpa nafasi rais Samia kuendelea kutawala mpaka 2030.

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi wa tano Tundu Lisu alitangaza kumvaa rais Samia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

===

Mbowe alitoa msimamo huo jana jijini, akisisitiza kwamba wanakusudia kupita nchi nzima kuidai katiba hiyo kwa kuwa ni haki ya wananchi.

Alikuwa akizindua mfumo wa kielekroniki wa chama hicho wa kuwatambua wanachama wake. “Tunaposema tunahitaji Katiba Mpya, tutawafundisha wanachama na viongozi wetu, watambue umuhimu na uzito wake, kwa sababu udhaifu wa katiba yetu ya sasa umesababisha kuwa na kiongozi aliyekuwa madarakani kuharibu nchi, kuumiza na kuwatesa wananchi kwa kuwa katiba hii inampa mamlaka makubwa ya kifalme.

“Rais akisema mfunge mtu huyu, sitaki kuona mikutano ya hadhara au kuona kiongozi wa upinzani, anashinda uchaguzi na haki za wananchi wote milioni 60 zinapotea shauri ya kiongozi mmoja mwenye madaraka na mamlaka makubwa kutokana na udhaifu wa katiba hii ya sasa," alifafanua.

Mbowe alisema tayari ameshazungumza na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la Katiba Mpya, kwamba siyo mapenzi ya mtu mmoja, bali ni mapenzi ya taifa.

“Nimemwambia Mama Samia (Rais), mambo ya katiba siyo mambo ya mapenzi yake, ni mapenzi ya taifa la Tanzania na Katiba Mpya tutaitafuta na kuipigania kwa jasho na damu ili kupata katiba ya nchi yetu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025," alisema.
Katika hatua nyingine, Mbowe, alimpongeza Rais Samia kwa kile ambacho alikiita kurudisha tabasamu na matumaini kwa wananchi akidai walipoteza imani na viongozi kutokana na baadhi ya mambo maovu.

"Mama (Rais) amerejesha matumaini na tabasamu kwenye sura za Watanzania na CHADEMA, kwa hilo tunamuunga mkono na nilimwandikia ujumbe wa kutaka kuonana naye kwa ajili ya mazungumzo.

"Alinijibu kwamba tutakutana na kuzungumza, hivyo basi tunasubiri nafasi hiyo ya mazungumzo kwa kuwa kuna mambo mengi mabaya yamefanyika kwenye nchi hii," alisema.

Mbowe alidai kuwa moja ya mambo watakayoyawasilisha kwa Mkuu wa Nchi ni kitendo cha wafuasi wa chama hicho zaidi ya 250 kufungwa gerezani huku akidai baadhi yao wameshtakiwa kwa makosa ya kubambikwa ukiwamo unyang’anyi, uhujumu uchumi, mauaji na ubakaji.

Pia alitangaza mkakati wa CHADEMA kuanza kujenga ofisi za chama hicho kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na kanda ili kuongeza imani kwa wanachama wake, kuwaziba midomo baadhi ya makada kutoka vyama vingine vya siasa kuwa chama hicho hakina ofisi.

"Ofisi hizi zitajengwa kwa nguvu za wanachama ili kuonyesha nguvu ya umma inaweza kufanya chochote bila kutengemea ruzuku ya Sh. milioni 380 kwa wabunge na madiwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020, walizokuwa wanapokea kwa mwezi.
Alisema kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, walipaswa kupokea ruzuku ya Sh. milioni 140 kwa mwezi, lakini waliikataa kutokana na kutoutambua uchaguzi huo.

"Atakayeomba kurudi na kuomba msamaha tumpokee na kumsamehe kwa kuwa chama chetu hakihukumu bali tunataka kujenga taifa lenye haki na mshikamano pasipo kuwabagua watu kutokana na itikadi za vyama, sura, rangi, kabila au dini," alisema.
*Imeandikwa na Allan Isack na Cynthia Mwilolezi.

Chanzo: IPP Media
Mheshimiwa Mwenyekit Mh Mbowe anasemaje kuhusu uchaguzi wa kipima joto wa serikali za mitaa utakofanyika 2024?
 
Uchaguzi wa kidemokrasia bila Tume huru? Wachekesha sana wewe. Si itawasaidia muweze kupata nafasi ya kuokoteza wa kuunda Covid # wengine.
Tume iko Huru, nenda kasome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 74 (11) utaelewa ndugu yangu usipotoshe watu.
 
Shida nayoiona Chadema wanataka katiba mpya ya Taifa lakini Katiba ya Chadema inampa mwanya mtu moja tu kuwa Mkiti miaka yote kwanini?
Kwa nini hiyo ikupe shida wewe, kwani ni mwanachama wao? Kama ni mwanachama, basi lifikishe chamani litatuliwe.

CHADEMA kuhimiza katiba mpya ya nchi haizuiwi kwa wao kutokuwa na katiba mpya.
 
Back
Top Bottom