Mbowe: CHADEMA hatutashiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 (bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi)

Siyo majambazi, mafisadi na wachezea mifumo ya serikali tu wanaomjaribu rais Samia hata Chadema wanamjaribu.

Leo wametangaza maandamano ya kudai katiba mpya na tume huru yani wanataka rais aache kufocus na kukamilisha SGR ,Bwawa la nyerere ,ajira, viwanda ambavyo ndiyo hitaji la wananchi akaanze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya katiba ambayo ni hitaji la wanasiasa tu?

Mbaya zaidi wanataka mchakato wa katiba uanze upyaaaaa na siyo pale ulipoishia zamani
 
100% Nakubaliana na Mbowe; the only solution kwa kile wanachokitafuta Vyama Mbadala ni Kupambana usiku na Mchana kudai Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi. Mengine yote ni Mbwembwe tu Itakaa Ikatokea hapa Tanzania kwa Wapinzani Kuingia Ikulu kwa tume hizi za CCM.

However, Main objective ya Opposition ni Kuongoza nchi, but inapokuwa Imeshindikana au Kura hazijatosha kwa sababu yoyoteile basi uwakilishi wao bungeni ulete Tija katika Jamii. Mh. Mbowe, Mnyika plus your people kaza boot (Kudai Haki Kuna gharama Zake) it's never too late and not ease task to pursue.
Yule mwana wa Saspenda le marehemu Mchungaji aligomagaaa weweee akalegeza akashiriki, akapata ajali akafa, tukamzika.

Na hadithi yetu ikaishia hapo.
 
Sasa isiposhiriki uchaguzi wa kidemokrasia inategemea kufanya mapinduzi ya kibabe? ifike wakati CHADEMA muache hizi siasa maji taka fanyeni sisa zenye dira kwa maslahi mapana ya taifa. mmeshindwa kumpelekea spika uthibitisho wa vikao vilivyowafukuza Covid 19 wananchi tunawaangalia tu mnavyocheza na akili zetu tunaomba mjibu swali kwanza la rufaa za wale Covid 19 ndio tuwasikilize kwa haya mengine. kusudi la kusema hayo ni kuonyesha kuwa tunahangaika na adui wa nje wakati tunamwacha adui tuliekaa naye mezani shida ya CHADEMA inaanzia ndani ya chama najua katika hili watanielewa wachache kwa sasa lakini wengi watanielewa baadae
Mimi nimekuwa mwanachama tangu 1994 nakuelewa vizuri sana, uzuri yeyote mwenye muono wa uongozi wa kushindanisha anafahamu.

Hizi kelele za mitandaoni hazifanyi kazi sawa sawa kama sumu tunayo mwaga tuliokuwa wanachama. Sio muda mrefu chama kitabadilika na kukaa sawa.

Virtually all dependable brain within the party have left, we have remain with immature member regardless of age. We have lost an entire generation of leaders and voters for selfish gains and preservation of positions and power within the party. It is very sad turn of events, he now realises to have lost dependable friends.
 
Katiba mpya haitawezekana
Ccm hawawezi kutoa katiba mpya kamwe.
Katiba mpya itatoka kwa kulazimisha ila sio kwa matakwa ya ccm
Kupata katiba mpya mi sawa na kupata uhuru kutoka kwa mkoloni tena bora mkoloni alikuwa na kwao. Anakupa anaondoka. Ccm hawana kwao tupo nao hapa hapa.
Suala la katiba mpya sahauni labda watu waingie kitaa damu zimwagike etc. Ila bure bure hio haipo
Sawa mku lakini twambie wewe uko tayari kuingia barabarani ufe damu yako imwagike kwa kudai katiba mpya?
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameenda kinyume na Lisu kwa kutangaza kuwa Chadema haitashiriki uchaguzi mkuu nchini wa mwaka 2025, hivyo kumpa nafasi rais Samia kuendelea kutawala mpaka 2030.

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi wa tano Tundu Lisu alitangaza kumvaa rais Samia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

===

Mbowe alitoa msimamo huo jana jijini, akisisitiza kwamba wanakusudia kupita nchi nzima kuidai katiba hiyo kwa kuwa ni haki ya wananchi.

Alikuwa akizindua mfumo wa kielekroniki wa chama hicho wa kuwatambua wanachama wake. “Tunaposema tunahitaji Katiba Mpya, tutawafundisha wanachama na viongozi wetu, watambue umuhimu na uzito wake, kwa sababu udhaifu wa katiba yetu ya sasa umesababisha kuwa na kiongozi aliyekuwa madarakani kuharibu nchi, kuumiza na kuwatesa wananchi kwa kuwa katiba hii inampa mamlaka makubwa ya kifalme.

“Rais akisema mfunge mtu huyu, sitaki kuona mikutano ya hadhara au kuona kiongozi wa upinzani, anashinda uchaguzi na haki za wananchi wote milioni 60 zinapotea shauri ya kiongozi mmoja mwenye madaraka na mamlaka makubwa kutokana na udhaifu wa katiba hii ya sasa," alifafanua.

Mbowe alisema tayari ameshazungumza na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la Katiba Mpya, kwamba siyo mapenzi ya mtu mmoja, bali ni mapenzi ya taifa.

“Nimemwambia Mama Samia (Rais), mambo ya katiba siyo mambo ya mapenzi yake, ni mapenzi ya taifa la Tanzania na Katiba Mpya tutaitafuta na kuipigania kwa jasho na damu ili kupata katiba ya nchi yetu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025," alisema.
Katika hatua nyingine, Mbowe, alimpongeza Rais Samia kwa kile ambacho alikiita kurudisha tabasamu na matumaini kwa wananchi akidai walipoteza imani na viongozi kutokana na baadhi ya mambo maovu.

"Mama (Rais) amerejesha matumaini na tabasamu kwenye sura za Watanzania na CHADEMA, kwa hilo tunamuunga mkono na nilimwandikia ujumbe wa kutaka kuonana naye kwa ajili ya mazungumzo.

"Alinijibu kwamba tutakutana na kuzungumza, hivyo basi tunasubiri nafasi hiyo ya mazungumzo kwa kuwa kuna mambo mengi mabaya yamefanyika kwenye nchi hii," alisema.

Mbowe alidai kuwa moja ya mambo watakayoyawasilisha kwa Mkuu wa Nchi ni kitendo cha wafuasi wa chama hicho zaidi ya 250 kufungwa gerezani huku akidai baadhi yao wameshtakiwa kwa makosa ya kubambikwa ukiwamo unyang’anyi, uhujumu uchumi, mauaji na ubakaji.

Pia alitangaza mkakati wa CHADEMA kuanza kujenga ofisi za chama hicho kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na kanda ili kuongeza imani kwa wanachama wake, kuwaziba midomo baadhi ya makada kutoka vyama vingine vya siasa kuwa chama hicho hakina ofisi.

"Ofisi hizi zitajengwa kwa nguvu za wanachama ili kuonyesha nguvu ya umma inaweza kufanya chochote bila kutengemea ruzuku ya Sh. milioni 380 kwa wabunge na madiwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020, walizokuwa wanapokea kwa mwezi.
Alisema kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, walipaswa kupokea ruzuku ya Sh. milioni 140 kwa mwezi, lakini waliikataa kutokana na kutoutambua uchaguzi huo.

"Atakayeomba kurudi na kuomba msamaha tumpokee na kumsamehe kwa kuwa chama chetu hakihukumu bali tunataka kujenga taifa lenye haki na mshikamano pasipo kuwabagua watu kutokana na itikadi za vyama, sura, rangi, kabila au dini," alisema.
*Imeandikwa na Allan Isack na Cynthia Mwilolezi.

Chanzo: IPP Media
Mku wakati tukipata 380 million kila mwezi za ruzuku, hatukuweza kujenga ofisi za chama hata hapa Dsm makao makuu, safari hii hatuna hiyo ruzuku, tupe mchang'anuo na uwezekano wa kupata hizo ofisi za Chama kuanzia ngazi ya wilaya, Mkoa na kanda.
 
It’s better to be both. But since this is almost impossible to achieve, a leader is better off being feared than loved, because men are ungreatful, fickle, and greedy.
In today's enlightened world, it's a very primitive impulse to wish for SUBSERVIENCE towards leaders - fellow men. Such was the situation in feudal societies of the past where it was assumed rulers knew everything and are almost divine. Where personality cults were the norm.

In modern sociopolitical settings like ours, STRONG RULE OF LAW governs and puts in check negative human traits of both leaders and the led. Selfishness and greedy are basic human weaknesses that have to be dealt with sustainably without having to resort to losing our civility and human dignity. Strong nations do well with "normal" leaders. Only banana republics are ruled by feared tyrants.

This culture of grovelling and begging before leaders amplified in Tanzania during the last presidency is unacceptable. We are very relieved it just disappeared.
 
Katiba mpya haitawezekana
Ccm hawawezi kutoa katiba mpya kamwe.
Katiba mpya itatoka kwa kulazimisha ila sio kwa matakwa ya ccm
Kupata katiba mpya mi sawa na kupata uhuru kutoka kwa mkoloni tena bora mkoloni alikuwa na kwao. Anakupa anaondoka. Ccm hawana kwao tupo nao hapa hapa.
Suala la katiba mpya sahauni labda watu waingie kitaa damu zimwagike etc. Ila bure bure hio haipo
Ninaelekea kukubaliana na wewe katika hili.

Mbowe kasema wanakwenda kwa wananchi kulielezea hili la katiba mpya.

Matumaini yangu makubwa ni kwamba watakapolipeleka swala hili kulieleza kwa wananchi watakuwa na ushawishi mkubwa wa kuwaelimisha wananchi hayo haya uliyoyaandika hapa wewe, ili wananchi watoe shaka yote juu ya nani anayeng'ang'ania katiba mbovu na kwa sababu zipi.

Wananchi ni lazima waelewe vyema kabisa kuhusu swala hili la katiba mpya na kwa nini kuna chama hakitaki iwepo katiba mpya.

CHADEMA wakifanikiwa kuifanya kazi hiyo muhimu ya kuwaelimisha wananchi, hapo sasa kazi yao itabaki kuongoza juhudi za wananchi wenyewe kuitafuta katiba mpya.
CHADEMA wasipofanikiwa kuwavuta wananchi juu ya swala hilo, hakuna lolote litakalobadilika hiyo 2021.

CHADEMA ni lazima wajizatiti kufanya kazi hii ngumu, lakini muhimu sana kwa ushirikiano na wananchi.

Leo na 2025, hakuna muda mwingi. KAZI INAPASHWA KUANZA MARA MOJA.
 
Siyo majambazi, mafisadi na wachezea mifumo ya serikali tu wanaomjaribu rais Samia hata Chadema wanamjaribu.

Leo wametangaza maandamano ya kudai katiba mpya na tume huru yani wanataka rais aache kufocus na kukamilisha SGR ,Bwawa la nyerere ,ajira, viwanda ambavyo ndiyo hitaji la wananchi akaanze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya katiba ambayo ni hitaji la wanasiasa tu?

Mbaya zaidi wanataka mchakato wa katiba uanze upyaaaaa na siyo pale ulipoishia zamani
Acha propaganda
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameenda kinyume na Lisu kwa kutangaza kuwa Chadema haitashiriki uchaguzi mkuu nchini wa mwaka 2025, hivyo kumpa nafasi rais Samia kuendelea kutawala mpaka 2030.

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi wa tano Tundu Lisu alitangaza kumvaa rais Samia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

===

Mbowe alitoa msimamo huo jana jijini, akisisitiza kwamba wanakusudia kupita nchi nzima kuidai katiba hiyo kwa kuwa ni haki ya wananchi.

Alikuwa akizindua mfumo wa kielekroniki wa chama hicho wa kuwatambua wanachama wake. “Tunaposema tunahitaji Katiba Mpya, tutawafundisha wanachama na viongozi wetu, watambue umuhimu na uzito wake, kwa sababu udhaifu wa katiba yetu ya sasa umesababisha kuwa na kiongozi aliyekuwa madarakani kuharibu nchi, kuumiza na kuwatesa wananchi kwa kuwa katiba hii inampa mamlaka makubwa ya kifalme.

“Rais akisema mfunge mtu huyu, sitaki kuona mikutano ya hadhara au kuona kiongozi wa upinzani, anashinda uchaguzi na haki za wananchi wote milioni 60 zinapotea shauri ya kiongozi mmoja mwenye madaraka na mamlaka makubwa kutokana na udhaifu wa katiba hii ya sasa," alifafanua.

Mbowe alisema tayari ameshazungumza na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu suala la Katiba Mpya, kwamba siyo mapenzi ya mtu mmoja, bali ni mapenzi ya taifa.

“Nimemwambia Mama Samia (Rais), mambo ya katiba siyo mambo ya mapenzi yake, ni mapenzi ya taifa la Tanzania na Katiba Mpya tutaitafuta na kuipigania kwa jasho na damu ili kupata katiba ya nchi yetu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025," alisema.
Katika hatua nyingine, Mbowe, alimpongeza Rais Samia kwa kile ambacho alikiita kurudisha tabasamu na matumaini kwa wananchi akidai walipoteza imani na viongozi kutokana na baadhi ya mambo maovu.

"Mama (Rais) amerejesha matumaini na tabasamu kwenye sura za Watanzania na CHADEMA, kwa hilo tunamuunga mkono na nilimwandikia ujumbe wa kutaka kuonana naye kwa ajili ya mazungumzo.

"Alinijibu kwamba tutakutana na kuzungumza, hivyo basi tunasubiri nafasi hiyo ya mazungumzo kwa kuwa kuna mambo mengi mabaya yamefanyika kwenye nchi hii," alisema.

Mbowe alidai kuwa moja ya mambo watakayoyawasilisha kwa Mkuu wa Nchi ni kitendo cha wafuasi wa chama hicho zaidi ya 250 kufungwa gerezani huku akidai baadhi yao wameshtakiwa kwa makosa ya kubambikwa ukiwamo unyang’anyi, uhujumu uchumi, mauaji na ubakaji.

Pia alitangaza mkakati wa CHADEMA kuanza kujenga ofisi za chama hicho kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na kanda ili kuongeza imani kwa wanachama wake, kuwaziba midomo baadhi ya makada kutoka vyama vingine vya siasa kuwa chama hicho hakina ofisi.

"Ofisi hizi zitajengwa kwa nguvu za wanachama ili kuonyesha nguvu ya umma inaweza kufanya chochote bila kutengemea ruzuku ya Sh. milioni 380 kwa wabunge na madiwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020, walizokuwa wanapokea kwa mwezi.
Alisema kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, walipaswa kupokea ruzuku ya Sh. milioni 140 kwa mwezi, lakini waliikataa kutokana na kutoutambua uchaguzi huo.

"Atakayeomba kurudi na kuomba msamaha tumpokee na kumsamehe kwa kuwa chama chetu hakihukumu bali tunataka kujenga taifa lenye haki na mshikamano pasipo kuwabagua watu kutokana na itikadi za vyama, sura, rangi, kabila au dini," alisema.
*Imeandikwa na Allan Isack na Cynthia Mwilolezi.

Chanzo: IPP Media
Motive ya kudai katiba mpya isiwe ya kuitoa ccm madarakani,au kuwezesha vyama vingine kushinda uchaguzi; hapana, bali ni HAKI yao wananchi wa kila Taifa.Wana nchi ndio wanaoajiri viongozi .Ni juu yao ya kuwaweka madarani viongozi wanaowataka
 
Huyu jamaa anaua upinzani, yaani jana tu katoka kusema anamuunga mkono mama then leo tena hawatashiriki uchaguzi. Chadema mwangalieni huyu mwenyekiti.

Kumuunga mkono huyo mama ni kushiriki uchaguzi wenye tume isiyoaminika?
 
Motive ya kudai katiba mpya isiwe ya kuitoa ccm madarakani,au kuwezesha vyama vingine kushinda uchaguzi; hapana, bali ni HAKI yao wananchi wa kila Taifa.Wana nchi ndio wanaoajiri viongozi .Ni juu yao ya kuwaweka madarani viongozi wanaowataka

Uko sahihi kabisa, ila ccm wanapata hofu maana wanajua kwenye ushindani sawa , hawana uwezo wakushinda kihalali.
 
Mku wakati tukipata 380 million kila mwezi za ruzuku, hatukuweza kujenga ofisi za chama hata hapa Dsm makao makuu, safari hii hatuna hiyo ruzuku, tupe mchang'anuo na uwezekano wa kupata hizo ofisi za Chama kuanzia ngazi ya wilaya, Mkoa na kanda.
Akikujibu katambike
 
Motive ya kudai katiba mpya isiwe ya kuitoa ccm madarakani,au kuwezesha vyama vingine kushinda uchaguzi; hapana, bali ni HAKI yao wananchi wa kila Taifa.Wana nchi ndio wanaoajiri viongozi .Ni juu yao ya kuwaweka madarani viongozi wanaowataka
Sasa ngoja nikupime na haya mawazo yako hapa:

Unaonaje ikiwa "motive" ya CCM wakikataa katiba mpya ili isiwaondoe madarakani?

Naona upande huo hukuusemea; pamoja na kwamba maelezo yako juu ya "HAKI" ya wananchi ni sahihi.
 
Sawa mku lakini twambie wewe uko tayari kuingia barabarani ufe damu yako imwagike kwa kudai katiba mpya?
Mimi sipo tayari kabisa. Na sio mimi tu nina uhakika hata wewe haupo tayari. Kwa sababu ambazo tunazijua wenyewe.
 
Mkuu@Saint Ivuga: huoni huo uamuzi wa mh Mbowe kuwa ni mwanzo wa kuanzisha vuguvugu la kudai hiyo katiba?

Unadhani au kufikiria chama kama ACT na CUF na TLP na wengine wanaweza kuamua uamuzi mgumu na wa kuumiza kama huo?
Mkuu sio kazi ndogo.
Inatakiwa chadema ijitambue haswaaa.
Mpaka sasa hivi tunaenda wote pamoja-
.
Wananchi wanaangalia kila move inayofanywa na cdm.
Mkibugi tu sijui mchukue ruzuku za wale covid sjui muwasamehe muwakubali ni wabunge wenu.
Then mkirudi kwa wananchi mtaambulia unyoya tu.

Mbowa asimame kama alivyo sasa hivi
 
Back
Top Bottom