Mbowe hawezi kushinda hii kesi. Rais Samia amsamehe bure

Mbowe hawezi kushinda hii kesi. Rais Samia amsamehe bure

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Hii kesi ni kesi ambayo wanataka kujadili mambo madogo tu ambayo hayana umuhimu wowote kwa taifa.

Ikumbukwe alikuwepo Magufuli ambaye alikuwa mpole sana kwa raia wanyonge lakini mkali sana kwa mafisadi, mkali sana kwa wapinzani. Tumeona mambo ya ovyo yaliyokuwa yanawafika wapinzani, heart-rending videos za kuzuia maandamano ya wapinzani.
Wapinzani wakazuiwa kufanya mikutano, halafu Corona ikachukua mahala makatazo ya rais yalipoishia. Kwa hiyo wapinzani wakawa compromised katika Uchaguzi iliopita.

Halafu wazungu mabalozi wanahudhuria mahakamani out of sympathy, kwa ubinadamu tu, siyo kwa vile wanataka kumweka Mbowe Ikulu. Lakini serikali ikiwaona ina panic. Kwanza hao watu wanakuwa debased kwenda pale. Ukimwachia huru Mbowe utakuwa umeonyesha heshima kwa hao Big Brother. Ni mawazo yako tu wewe kwamba you are a sovereign country. Those people would beg to differ. Na bado hao watu hawawezi kwenda mahakamani kwa sababu yoyote isipokuwa wana shaka kuna atawatajataja pale

Huwezi kumfanya kitu Mbowe kwa sababu hao wameshaiteka nyara mahakama,so to speak. Mbowe asipoachiwa huru somebody will get hurt.

Haya mambo kutaka kuadhibu makosa yaliyofanyika katika awamu iliyopita,hayana maana. Nani alimzuia Magufuli kumdhibiti Mbowe muda wote alipokuwa madarakani? Au kumthibiti Harbinder Singh au Rugemarila ? Lakini hao watu wako jela mpaka leo.
Waachiwe huru. Rais ana uwezo kusamehe watu. Katiba ndio inavyosema. Awasamehe hao watu. Naomba kutoa hoja.
 
Aachiwe huru yeye kama nani? Watu wote wako chini ya sheria. Acha ifuate mkondo wake. Km ni gaidi itathibitika tu
 
Mbowe anataka kumuumiza nani? Mi nilikuwa nakwenda Mbowe Disco zamani. Mbowe Disco ilikuwa ilikuwa head above the shoulders ukilinganisha na disco nyingine. Mbowe ni DJ.
 
Unajua maana ya sadaka?
Sadaka inayokubalika ni sadaka ya vinono, si ya vinyonge, vigonjwa wala vilivyokondeana na visiwe vilema
😁😂🤣
Dah imenibid nicheke. Et vigonjwa.
Aya bhana. Naona ndug zako hutak kabisa waguswe.
 
Kwa Jeuri Kali na Mbaya aliyoionyesha Freeman Mbowe na Dharau pamoja na Kiburi cha wana CHADEMA sitaki Rais Samia amsamehe acha Jela ikamnyooshe vizuri kama akipatikana na Hatia.

Na kwa Legal Gurus niliobahatika Kukutana nao wamesema hii ni Kesi ambayo Mbowe Mwenyewe na Wafuasi wa CHADEMA wanaiona ni nyepesi ila Kisheria na Kiushahidi imekaa vibaya na wasipokuwa makini nayo Freeman Mbowe anaweza kuwa Mwenyekiti wa Wafungwa wote wa CHADEMA walioko Magerezani.
 
Yani unaweza poteza muda kwa kusoma ukijua kuna lamaana kumbe ovyo
 
Harufu ya bia. What are talking about? I am tea toe teller.
 
Mbowe almtukana sana Hayati magufuli nikasema he will pay karma inamfuata
 
Back
Top Bottom