Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Mbowe anaungwa mkono zaidi na wajinga, tafakari!!.Jf ni wapiga debe TU,ila wamiliki WA kura na uchaguzi Jf hakuna hata mmoja!
Mbowe ana haki ya kikatiba kugombea sio sawa kusema amuachie TAL kny democrasia ya kweli kupiga kura ndo njia sahihi kumbuka chadema ni chama cha democrasia makini tuache ushabiki unaokinzana na dira na dhima ya chadema.Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.
- Utaijengea CHADEMA heshima
- Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.
Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Haki hazikutakiwa kujadiliwa! Kilichotakiwa kujadiliwa ni Katiba na Tume ya UchaguziMkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Njia mbadala ya Lissu ilikuwa ni ipi? Kabla ya mazungumzo alitaka kifanyike nini? Wakina mama kujirekodi huku wameshika mabango ndio kingeleta Katiba Mpya?
Kumbuka kilichompeleka Mbowe Jela ni Katiba.Sikubaliani na wewe kuwa ni madai ya Katiba ndio yalifanya Mbowe aachiwe. Ni realisation kuwa ile charade inamfanya Mbowe kuonekana martyr. Madai ya Katiba Mpya yalienda sambamba ni kilio kuwa " Mbowe sio gaidi"!
Amandla...
Fundi Mchundo aka Fundi Utumbo, mstaarabu akivuliwa nguo huchutama...watoto kama sisi tupo na hatujui unafiki hivyo hatutasita kutangaza kuwa mfalme yuko mtupu.Mkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Njia mbadala ya Lissu ilikuwa ni ipi? Kabla ya mazungumzo alitaka kifanyike nini? Wakina mama kujirekodi huku wameshika mabango ndio kingeleta Katiba Mpya?
Sikubaliani na wewe kuwa ni madai ya Katiba ndio yalifanya Mbowe aachiwe. Ni realisation kuwa ile charade inamfanya Mbowe kuonekana martyr. Madai ya Katiba Mpya yalienda sambamba ni kilio kuwa " Mbowe sio gaidi"!
Amandla...
PropagandaUngejua who is sponsoring these outfits, you wouldn't have said that...
...
Ningependa kuona muamko mpya wa CDM kupitia TL,
Lakini wanaochochea haya mabadiliko ni watu wenye nia ovu sana na hicho chama pengine zaid na nchi yetu.
Tundu will f#$k it.
Katiba ni muongozo wa sheria za nchi zinazopaswa kufuatwa na Watawala na Watawaliwa.Mkuu Nguruvi3 , majadiliano kati ya CDM na CCM yalilenga katika kuhakikisha kuwa watanzania wanapata Haki zao zote zilizomo katika Katiba ya sasa.
Sawa sawa na ndio maana hata Tusiokuwa na vyama tunajadili hii kwasababu Vyama vya siasa vina 'impact' katika maisha ya jamii yetu. Madhara ya kukosa upinzania Bungeni tumeyaona.CDM, kama chama kikuu cha upinzani kilikuwa kinawasemea watanzania ambao hawakuwa na mtu wa kuwasemea.
Kauli iliyompelekea awakemee vijana wake ni ile ya ' Hakieleweki isipokuwa Katiba mpya'' hili ni tusi?Kuwaambia Bavicha watunze ndimi zao maana yake ni wasitumie lugha ya matusi na shombo wakati wanadai Katiba Mpya. Huko sio kuwakataza kuzungumzia Katiba Mpya unless lugha pekee iliyostahili ni ya matusi na shombo.
Yeye alidai 'minimal reforms'' akisema muda wa Katiba ni mfupi.Na hata yeye na chama chake waliendelea kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Kusema vingine ni kuwaonea.
Amandla...
Hkauna alternative ya Maridhiano! unless Katiba na NEC zipo mezani. Hizo ndizo agenda kuuMkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Alternative kwa majadiliano ni nini?
Ndilo shinilizo alilowekewa JK akaukbali kuanzisha mchakato. Ilikuwa pressure tuWagome kufanya majadiliano yeyote kabla ya kupata Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi?
Watu wao walikamatwa na kusingiziwa kesi ! Kilichotokea ni CDM kulipa ''ransom'Hatua gani wachukue ili watu wao waachiwe?
Asante sana Nguruvi3, kwa upande wangu nitaendelea kuwashukia kama mwewe wanaojaribu kuhalalisha vitendo vya rushwa kwa kutanguliza maslahi binafsi.Hkauna alternative ya Maridhiano! unless Katiba na NEC zipo mezani. Hizo ndizo agenda kuu
Kuachiwa watu wao , kurudishiwa mali n.k. havikupaswa kuchukua nafasi ya Katiba na Tume ya Uchaguzi.
Kama nimekuelewa vizuri, unamlaumu Mbowe kwa kwa kuzungumzia watu kuachiwa, watu kurudishiwa mali zao, walio uhamishano kuhakikishiwa usalama wao, Covid-19,Mikutano ya hadhara ya kisiasa? Yote hayo unaona hayana maana mbele ya Katiba Mpya na Tume ya Uchaguzi iliyo huru? Sijui kama ungekuwa na ndugu yako rumande ameshitakiwa kwa kosa la mauaji? Kesi ambayo inapigwa dana dana kila siku kwa hiyo haujui huyo ndugu yako atakaa ndani kwa miaka mingapi. Na ndugu yako huyo alikuwa hana kipato cha maana na ameacha mke, watoto na wazazi wanaomtegemea. Unemwambia awe mvumilivu kwa sababu kukaa kwake ndani kutaifanya serikali ifanye marekebisho katika muundo wa Tume ya Uchaguzi. Mimi hapo natofautiana kabisa na wewe. Ninamuunga mkono kuwa maisha ya hao watu wasio na hatia, uwezo wa kufanya mikutano ya hadhara ni muhimu zaidi ya makubaliano yeyote kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuachiwa kwa hao wapiganaji na kibali cha kufanya mikutano ya hadhara ni nyenzo muhimu katika kuwaelemisha wananchi kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya ili kwa pamoja waweze kushirikiana kuipresha serikali ili ifanye mabadiliko hayo muhimu.Hkauna alternative ya Maridhiano! unless Katiba na NEC zipo mezani. Hizo ndizo agenda kuu
Kuachiwa watu wao , kurudishiwa mali n.k. havikupaswa kuchukua nafasi ya Katiba na Tume ya Uchaguzi.
Unazungumzia vitu viwili tofauti. JK hakuzuia mikutano ya hadhara. JK hakuwatia ndani wapinzani kwa kiasi kilichotokea baada ya utawala wake.Ndilo shinilizo alilowekewa JK akaukbali kuanzisha mchakato. Ilikuwa pressure tu
Unataka kutuambia kuwa wale watu walitiwa ndani kuzuia watu kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi? Ninavyojua mimi ni kuwa wengi walikamatwa wakati wa uchaguzi. Wengi walikuwa wanapinga matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi. Walichokuwa wanataka ni haki itendeke chini ya Tume iliyokuwepo wakati wa uchaguzi. Mbona Tume hiyo hiyo chini ya Katiba hiyo hiyo ilitangaza wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani kuwa washindi? Na wapinzani hao waliweza kutoa presha kwa serikali iliyopo wakiwa ndani ya Bunge.Watu wao walikamatwa na kusingiziwa kesi ! Kilichotokea ni CDM kulipa ''ransom'
Hakuna majadiliano ya watu kuachiwa kwasababu next time CCM itafanya hivyo kama 'bargaining chip''
Hoja ilikuwa kuwaambia si kuomba maridhiano. Ukamatwe, usingiziwe kesi halafu uombe maridhiano! Please
Hii nayo mimi naikumbuka tofauti na wewe. Mandela alikataa masharti ya De Klerk yafuatayo 1) ku"renounce violence kama njia ya kupigana na mfumo wa apartheid. 2) kutii sheria za makaburu za usalama wa ndani. Na barua yake yakukataa masharti hayo ilisomwa katika mkutano wa hadhara na binti yake Zinzi. Suala la Katiba mpya na Afrika ya Kusini ya baadae hayakuwa sababu ya kukataa kukaa chini na makaburu. Alisema akikubali haya masharti atabakia kuwa mfungwa hata kama hayuko jela. Alisema pia kuwa makaburu wanatakiwa kuhalalisha chama cha ANC, waachie wafungwa wote wa kisiasa, waruhusu waliokuwa uhamishano warudi, watoe uhuru wa kufanya siasa na waji commit katika kuacha siasa za kibaguzi. Mkutano huo aliohutubia binti yake uliandaliwa na UDF kwa vile ANC bado kilikuwa hakitambuliwi. Katika barua yake alisisitiza pia mshikamano kati yake na Oliver Tambo kwa sababu kulikuwa na rumours kuwa ndani ya ANC kuna mpasuko.ANC waliwaambia Mkaburu '' Usalama wa Mandela akitoka ni non-negotiable''
ANC wakasema '' Tujadili Katiba na South Africa post apartheid'' ANC hawakuta Mandela awe agenda!
Ulinzi wake ni haki ya Serikali iliyopo madarakani. Ikiwa kuachiliwa ilikuwa n sehemu ya mahjadiliano, ANC walikuwa tayari kuondoka na kumwacha Mandela aendelee kifungoni. That is leadership !
Ningeomba kueleweshwa. Katika maridhiano, FAM aliwaambia CCM kitu gani kuhusu hayo mambo tajwa ?Kama nimekuelewa vizuri, unamlaumu Mbowe kwa kwa kuzungumzia watu kuachiwa, watu kurudishiwa mali zao, walio uhamishano kuhakikishiwa usalama wao, Covid-19,Mikutano ya hadhara ya kisiasa?
Struggle za South Africa ni tofauti! Wao walikuwa vitani! Mbowe hakuwa vitaniCha kukumbuka ni kuwa baada ya kuachiwa Mandela majadiliano yaliendelea kwa miaka mitano ndio Mandele akachaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini.
Hapa una point kubwa sana! kwamba CCM hawataki kuondoka madarakani! Ni kweliHalafu nyinyi mnaamini miaka miwili ya majadiliano na chama ambacho hakina mpango wowote wa kutoka madarakani ( De Klerk aliishakubali kuwa siku za utawala wa kikaburu zimeisha) yataenda fasta kwa sababu kuna watu wanakuna Club House na kuweka Clip zao mitandaoni bila ya kuwa na mikutano ya hadhara na uhuru wa watu kukutana na kufanya shughuli za kisiasa. Hizo kwa kweli ni ndoto na kiongozi yeyote anayesema hilo litawezekana na muongo.
Hivi tungefanikiwa kupitisha Katiba ya Warioba 2014 unataka kusema leo tungekaa tena kujadili kama inakidhi nyakati zilizopo.Katiba Mpya halali haiwezi kupitishwa na Chadema na CCM peke hayo. Hata hiyo inayoitwa ya Warioba haiwezi kuanza kutumika bila kuangalia kama inakidhi matakwa ya wakati huu uliopo.
Sawa kabisa, hata ya Warioba ilikuwa na transition period ya 2014-2018Katiba Mpya ya Afrika Kusini iliandaliwa na Bunge lililochaguliwa 1994 na ilianza kutumika 1997, ikichukuwa nafasi ya Katiba ya mpito ya mwaka 1993.
Amandla...
Mimi sio Mbowe na simo katika Kuu. Kwa kauli ya Mbowe ni kwamba alipoenda Ikulu baada ya kutoka gerezani, Rais alimuuliza chama chake kinataka nini. Mbowe akamuambia cha msingi kabisa ni kuwa badala kuhubiri amani wahubiri haki. Akamwambia kuwa inabidi aongee kwanza na wenzake kabla ya kuendelea na mazungumzo. Akapeleka suala kwenye Kamati Kuu ambapo tunaambiwa kuna wengine hawakutaka mazungumzo ya aina yeyote kabla ya kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuna wengine wakamuunga mkono kuwa mazungumzo yaanze na mahitaji ya chama yawe hayo uliotaja pamoja na kuanzishwa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Sidhani kama waliomba bali walisema:Ningeomba kueleweshwa. Katika maridhiano, FAM aliwaambia CCM kitu gani kuhusu hayo mambo tajwa ?
-Naomba mturuhusu tufanye mikutano ya hadhara !
-Naomba Watu wetu waliofungwa waachiliwe kwa hisani yenu!
-Tunahitaji fadhila zenu mturudishie mali zetu mlizochukua !
-Tafadhali sana wenzetu walioko uhamishoni waruhusiwe kupita mipakani wakija Tz!
-COVID-19 , tujadiliane namna gani watarejea chamani au watabaki kuwa Wabunge
Ingawa South Afrika walikuwa vitani lakini walikuwa wanafuata Katiba yao ambayo iliruhusu vyama vilvyo halalishwa kufanya shughuli za kisiasa. Ndio maana Zinzi Mandela hakufungwa aliposoma barua ya baba ikikataa masharti mengine ya makaburu alifanya hivyo hadharani. Wakati kwetu vyama vya upinzani viliambiwa kuwa akiitokeza mtu yeyote katika mikutano/maandamano yao atapigwa kipigo cha mbwa mwizi! Na vilipotoa taarifa ya mkutano waliambiwa wasifanye kwa sababu za kiusalama.Struggle za South Africa ni tofauti! Wao walikuwa vitani! Mbowe hakuwa vitani
ANC walikuwa katika mazungumzo, FAM alikuwa katika Maridhiano!
ANC walifanya mazungumzo wakati apartheid ingalipo. Mbowe ameingia katika mazungumzo akidai haki ambazo aliamini zimeminywa na serikali pasipo halali. Naomba niambie strong position" ambayo Mbowe aliiacha ni ipi? Kununa nyumbani na kuwa na press conference na mashirika ya nje akilalamika kuwa haki zao zimeminywa? Akiulizwa mbona mwenzako yuko tayari kuyajadili lakini wewe ndio kikwazo angewajibu nini? Kwamba anaogopa kukosana na Makamu wake? Wakati watu wanaendelea kusota jela na rumande bila uhakika wa lini watatoka?ANC walifanya maridhiano baada ya ku abolish apartheid. Mbowe anatanguliza maridhiano bila kujua ni kati ya nani na nani na kwa ugomvi gani. Anakwenda kwenye maridhiano akiwa katika 'weak position'
Alijibu sahihi. Maana hamna faida yeyote ambayo angepata kwa kumkatalia. Hakujua anaitiwa nini. Labda alikuwa anaenda kupewa pole. Au kunywa juisi tu na kujadili kuhusu wajukuu zao. Asingejua dhumuni la wito ule bila kuuitikia. Hakwenda Ikulu kuanza majadiliano bali kusikia ameitiwa nini. Ilikuwa pia nafasi ya kumpima Rais kama ambavyo Mandela alivyompima de Klerk. Alipojua sababu za wito akawaambia wenzake na wakakubaliana ya kushiriki kwenye majadiliano.Hata yeye alikiri udhaifu huo kule Iringa aliposema '' Niliitwa Ikulu na Rais, mimi nina kiburi gani cha kumkatalia''. Hii ni baada ya kuulizwa uharaka wa kukimbilia Ikulu bila consulatation na viongozi wenzake .
Naam. Wengi waliamini hilo. Sio peke yake. Kosa liko wapi?Kibaya zaidi aliporudi akashawishi wenzake na nina nukuu '' Mama ana ni njema katika maridhiano''
Kwani ilikuwa uongo? Wahafidhina hao walikuwepo pande zote. Nakumbuka zilikuwa zina leak taarifa kuhusu push back aliyokuwa anapata Makamu Mwenyekiti wa CCM kuhusu hili suala. Maridhiano yangefikiwa lingekuwa jambo jema kwa taifa letuMbowe akawananga wenzake ''' Hata kwenye chama chetu tuna wahafidhina wasiotaka maridhiano''
Ameeleza dhumuni kwa ufasaha lakini mmeweka pamba masikioni. Alipoitwa mara ya kwanza hakujua sababu ya wito. Baada ya kupata kibali cha Kamati Kuu Chadema ikaunda jopo la watu wakuongea na counterparts wao wa CCM.Ndio maana tuna question, je, alijua anakwenda kufanya kuongea nini na nani na kwa muktadha gani
Mbinu zilizotumika mpaka utawala wa awamu ya 5 zilileta mafanikio makubwa. Kushindwa kwa CDM katika chaguzi zilizofanyika wakati wa awamu ya 5 na 6 yalitokana na aina ya utawala uliokuwepo. Tofauti na unavyodai, Mbowe amekuwa akibadilisha mbinu zake kulingana na uongozi uliokuwepo. Alimpokea Lowassa kwa sababu alijua kuwa ni nafasi ya kujiongezea wabunge , kura za wabunge na rais. Idadi ile ilikipa CDM platform kubwa sana ya kushindana na CCM katika mazingira magumu. Hata uchaguzi ujao angeweza kufanya vizuri kwa sababu kwa kushiriki katika uchaguzi wa hivi karibuni ame wa expose CCM kwa jamii sio tu ya Tanzania bali dunia nzima kuwa hawana nia ya kuachia madaraka kirahisi. Bahati mbaya, mtu wa karibu amemu undermine under the "mistaken belief" kuwa anaweza kutembea juu ya maji.Hapa una point kubwa sana! kwamba CCM hawataki kuondoka madarakani! Ni kweli
Hivi huoni kutumia mbinu zile zile miaka 21 ya FAM bila matokeo tofuati ina fit vizuri na definition ya Insanity.
Hamna rebellion hapa. Ni watu wachache wenye sauti kubwa kwenye majukwaa kama haya wanataka kuwa king makers. Hao watu wangekuwa wamechoka na status quo wangeandamana pale walipoombwa kuandamana. Shida yetu sisi ni kila wakati tunataka mtu wa kutuokoa badala ya kujipigania wenyewe. Ndio maana tunajazana kwa Babu wa Loliondo, Mwamposa, Kiboko wa Wachawi n.k. kwa sababu wanatuahidi mafanikio bila kufanya kazi na tiba isiyo na maumivu. Huyu mnae mpigia debe ni design hiyo. Atakapoona mambo ni magumu atawalaumu wenzake na kuwaacha waendelee wenyewe na mapigano.In fact hii ndiyo sababu kubwa ya 'rebellion' , watu wamechoka na status quo!
Hamna Katiba isiyofanyiwa Amendments. Hata ya Warioba ingefanyiwa Amendments.Hivi tungefanikiwa kupitisha Katiba ya Warioba 2014 unataka kusema leo tungekaa tena kujadili kama inakidhi nyakati zilizopo.
Na atakae sababisha yote hayo ni Makamu Mwenyekiti wa CDM. Ninachojua ni kuwa hata kama CDM itatetereka Mbowe ana uwezo wa kuijenga tena. Hilo ametuonyesha.Ni kweli Katiba mpya ni jambo shirikishi, lakini process nzima lazima iwe na 'leaders'' ambao ni CCM na Chadema. Ikiwa CDM itajivua jukumu ipo siku ombwe litajazwa kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF
Apumuzike tu amefanya mengiMheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.
- Utaijengea CHADEMA heshima
- Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.
Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Kwa hoja hii mimi si CDM wala sipo hata karibu na ofisi zao. Sijui nini kilijiri lakini nadhani kulikuwa na ku bulldoze waliokataa. Sijui kama kura zilitumika na sijui kama hoja za waliokataa ziliangaliwa kwa ubora. Sijui...Akapeleka suala kwenye Kamati Kuu wengine hawakutaka mazungumzo ya aina yeyote kabla ya kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuna wengine wakamuunga mkono kuwa mazungumzo yaanze
Mazungumzo (dialogue) hutokea kati ya wawili au zaidi katika kubadilishana fikra na mawazoIli tuweze kuelewana vizuri naomba uniambie tofauti ya mazungumzo na maridhiano.
Hapana, lengo la mazungumzo ni kuwa na Muafaka! consensusNinavyojua mimi kuwa lengo la mazungumzo yeyote ni kufikia kwenye maridhiano.
Hapa unanioea ! Aliyeleta neno Maridhiano katika kikoa (Domain) ni FAM.Chadema walikuwa hawajafika kwenye maridhiano kamili kwa hiyo kusema kuwa walikuwa kwenye "maridhiano" ni kuwa disingenous.
Of course, baada ya kuwa na Muafaka (concensus) kuhusu South Africa ikiwemo Katiba, iliundwa timu ya Maridhiano(reconciliation) chini ya Askofu D.Tutu (R.I.P) iliyoitwa Truth and reconciliation Commission. Kwa S.Africa Maridhiano yali conclude the process. Kwa FAM alianza na Maridhiano ndio maana tnapata shida ya kumwelewaHata hayo mazungumzo ya ANC lengo lilikuwa kufikia kwenye maridhiano.
Kuna siku Rais alibadili njia na kutokea uani. Ilikuwa notable . Tu criticise na kutoa credit inapobidiNjia mbadala ya mazungumzo ni wananchi na watu wengine kulazimisha kwa njia kama maandamano, migomo, kushtaki kwa nchi rafiki n.k. Mimi siamininjia zingeleta matokeo ya maana hata wale ambao sasa hivi ndio wako mstari wa mbele kumsema Mbowe kuwa msaliti walishindwa kuandamana huko katika nchi ambazo zina uhuru kamili wa wakazi wake kuandamana kupinga jambo lolote. Washington sana sana walijitokeza watu 10 na ushee. London hivyo hivyo. Rais na viongozi wenzake mara chungu mzima anatembelea nchi zao lakini hatuwaoni wakiandamana.
Haiwezekani kuwa na 'mbadala' wakati Mwenyekiti yupo katika Maridhiano.Ninachowashangaa ni kwa nini hizo njia mbadala hazikufanyika wakati mazungumzo ya maridhiano yanafanyika!.
Kutofautiana mitazamo hakufanyi awaye awe Mhafidhina. Neno hilo alilitumia FAM kuwadhalilisha wasiokubaliana naye. Kumbuka ukitaka kumuua Mbwa mpe jina baya kwanzaAngeweza kusema wasioafiki!Wahafidhina hao walikuwepo pande zote. Nakumbuka zilikuwa zina leak taarifa kuhusu push back aliyokuwa anapata Makamu Mwenyekiti wa CCM kuhusu hili suala. Maridhiano yangefikiwa lingekuwa jambo jema kwa taifa letu
Wakati wa JPM aliomba maridhiano yakafeli, na sasa ameomba yamefeli.Akiwa Zanzibar akasema '' Wenzangu waliokataa maridhiano walikuwa sahihi''
Ni alama ya ukomavu wake kuwa hasiti kusema kuwa alikosea. Mimi nadhani hakukosea lakini mimi sio Mbowe.
Ni lini FAM aliwahi kukabiliwa na sauti nyingi kama sasa! Hii ni rebellion baada ya incessant failuresHamna rebellion hapa. Ni watu wachache wenye sauti kubwa kwenye majukwaa kama haya wanataka kuwa king makers.
Well, Watu hawakuwa na uhakika kama wakiandamana M/Kiti atakuwepo au ataibukia Ikulu.Hao watu wangekuwa wamechoka na status quo wangeandamana pale walipoombwa kuandamana.
Katiba ingekuwa na miaka 6 tu. Jiulize ya 1977 imefanyiwa amendments ngapi katika average ya miaka.Hamna Katiba isiyofanyiwa Amendments. Hata ya Warioba ingefanyiwa Amendments.
Nakuhakikishia wakati huu itakuwa tofauti sana. Huko nyuma alikuwa na support ya Bigwigs na Wanachama.Na atakae sababisha yote hayo ni Makamu Mwenyekiti wa CDM. Ninachojua ni kuwa hata kama CDM itatetereka Mbowe ana uwezo wa kuijenga tena. Hilo ametuonyesha.
😂 nimeongeza msamiati.Kama wanavyosema wamarekani "FAFO"
Kwa kumnukuu James Hadley Chase, "Believe this and you will believe anything!" Mfungwa (gaidi) unatolewa gerezani, unakaribishwa Ikulu na kuulizwa ungependa upewe nini!Mimi sio Mbowe na simo katika Kuu. Kwa kauli ya Mbowe ni kwamba alipoenda Ikulu baada ya kutoka gerezani, Rais alimuuliza chama chake kinataka nini.
Yeah "eff around and find out" ni tisho kwetu tunaopinga usultani Chadema, kwamba tusithubutu kuchezea moto la sivyo tusubiri kuungua kama hatujaungua!Kama wanavyosema wamarekani "FAFO"