Pre GE2025 Mbowe iokoe CHADEMA kwa kuchukua maamuzi mazito ya kumuunga mkono Lissu, usisubiri kesho!

Pre GE2025 Mbowe iokoe CHADEMA kwa kuchukua maamuzi mazito ya kumuunga mkono Lissu, usisubiri kesho!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Njia mbadala ya Lissu ilikuwa ni ipi? Kabla ya mazungumzo alitaka kifanyike nini? Wakina mama kujirekodi huku wameshika mabango ndio kingeleta Katiba Mpya?

Sikubaliani na wewe kuwa ni madai ya Katiba ndio yalifanya Mbowe aachiwe. Ni realisation kuwa ile charade inamfanya Mbowe kuonekana martyr. Madai ya Katiba Mpya yalienda sambamba ni kilio kuwa " Mbowe sio gaidi"!

Amandla...
 
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Mbowe ana haki ya kikatiba kugombea sio sawa kusema amuachie TAL kny democrasia ya kweli kupiga kura ndo njia sahihi kumbuka chadema ni chama cha democrasia makini tuache ushabiki unaokinzana na dira na dhima ya chadema.
 
Mkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Njia mbadala ya Lissu ilikuwa ni ipi? Kabla ya mazungumzo alitaka kifanyike nini? Wakina mama kujirekodi huku wameshika mabango ndio kingeleta Katiba Mpya?
Haki hazikutakiwa kujadiliwa! Kilichotakiwa kujadiliwa ni Katiba na Tume ya Uchaguzi
Pili, haikupaswa kuitwa Maridhiano! Ilitakiwa kuitwa madai ! Maridhiano ya kitu gani?

Naomba unieleweshe, maridhiano kati ya nani ! na kwanini!
Sikubaliani na wewe kuwa ni madai ya Katiba ndio yalifanya Mbowe aachiwe. Ni realisation kuwa ile charade inamfanya Mbowe kuonekana martyr. Madai ya Katiba Mpya yalienda sambamba ni kilio kuwa " Mbowe sio gaidi"!

Amandla...
Kumbuka kilichompeleka Mbowe Jela ni Katiba.
Kama kuna kitu cha maana Wanachadema walifanikiwa ilikuwa ;
1. Martin Masesa kuchukua jukumu la kuufahamisha Umma kuhusu kesi ni real time
2. Wanachama kupiga kelele za Katiba mpya!

Ushahidi upo, kwamba, Mbowe aliitwa Ikulu kama kumwekewa 'kufuli'' na aliitwa mapema ili asikutane na wenzake watakokuwa na mawazo tofauti. Tangu alipotoka Ikulu Mbowe hakuongelea Katiba tena! Na kwamba alikataza BAVICHA waangalie ndimi zao. FAM akaulizwa kuhusu Katiba , akajibu '' ... Sijazuia mjadala wa Katiba, watu wanaweza kuendelea kudai wakati sisi tunazungumza'' Sasa fikiria ni nani anayeweza kuongea zaidi ya Mwneykiti tena anaposema ''chungeni ndimi zenu''
 
Mkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Njia mbadala ya Lissu ilikuwa ni ipi? Kabla ya mazungumzo alitaka kifanyike nini? Wakina mama kujirekodi huku wameshika mabango ndio kingeleta Katiba Mpya?

Sikubaliani na wewe kuwa ni madai ya Katiba ndio yalifanya Mbowe aachiwe. Ni realisation kuwa ile charade inamfanya Mbowe kuonekana martyr. Madai ya Katiba Mpya yalienda sambamba ni kilio kuwa " Mbowe sio gaidi"!

Amandla...
Fundi Mchundo aka Fundi Utumbo, mstaarabu akivuliwa nguo huchutama...watoto kama sisi tupo na hatujui unafiki hivyo hatutasita kutangaza kuwa mfalme yuko mtupu.

Katika hii serikali yetu ya CCM, hongo ina majina mengi sana. Kuna kutoa takrima, kuna kugawa kanga, kuna kutoa fadhila, kuna kutolewa gerezani na kuna kesi kufutwa.

Kaburu Voster Verwood, alitaka kumtoa mpigania uhuru wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, gerezani kama hongo ya kuwa huru, Mandela alimkatalia, hakutaka uhuru bandia.
 
Mkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Alternative kwa majadiliano ni nini? Wagome kufanya majadiliano yeyote kabla ya kupata Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi? Waandamane kwa sababu ni haki yao ya kikatiba? Waipeleke serikali Mahakamani? Hatua gani wachukue ili watu wao waachiwe?

Nimeiangalia na kuisikiliza tena hotuba aliyoitoa Mbowe Iringa mara baada ya kutoka gerezani.

Kitu kikubwa alichosema ni kuwa CDM sio chama cha visasi. Aliwashukuru wote waliompigania mpaka atoke. Aliwakumbusha kuwa aliyetunga wimbo wa "Mwamba Tuvushe" alifariki akiwa gerezani. Aliwaambia kuwa kitendo cha yeye kuwa gerezani kimekijenga chama chake.

Na aliwaambia kuwa alimuomba marehemu JPM zaidi ya mara 3 kukutana nae katika kikao cha kazi lakini alikataa. Ni kwa sababu hiyo ndio alikubali wito wa Rais kwa sababu alijua yeye ndie mwenye ufunguo wa kutatua changamoto zote zinazowakabili Chadema. Alipokutana nae alimwambia kuwa ni wakati wa ku focus kwenye Haki na sio Amani. Kuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa Haki inazingatiwa. Rais alikubaliana na ushauri huo na kwa mara ya kwanza Rais wa JMT alizungumzia suala la Haki akiwa amesimama na kiongozi wa chama alichokitambua kuwa ndio chama kikuu cha upinzani ( wote tulishuhudia hili).

Alisema details za matakwa ya kila upande zitajadiliwa baada ya kukaa na wenzake. Alisema wataendelea kushinikiza Haki itendeke kwa chama chao. Alisema kuwa wataendelea bila ruzuku. Hapa alikosea nini?

Amandla...
 
Mkuu Nguruvi3 , majadiliano kati ya CDM na CCM yalilenga katika kuhakikisha kuwa watanzania wanapata Haki zao zote zilizomo katika Katiba ya sasa. CDM, kama chama kikuu cha upinzani kilikuwa kinawasemea watanzania ambao hawakuwa na mtu wa kuwasemea. Ningependa kuona huo ushahidi wa kufuli. Kuwaambia Bavicha watunze ndimi zao maana yake ni wasitumie lugha ya matusi na shombo wakati wanadai Katiba Mpya. Huko sio kuwakataza kuzungumzia Katiba Mpya unless lugha pekee iliyostahili ni ya matusi na shombo. Na hata yeye na chama chake waliendelea kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Kusema vingine ni kuwaonea.

Amandla...
 
Ungejua who is sponsoring these outfits, you wouldn't have said that...
...
Ningependa kuona muamko mpya wa CDM kupitia TL,

Lakini wanaochochea haya mabadiliko ni watu wenye nia ovu sana na hicho chama pengine zaid na nchi yetu.

Tundu will f#$k it.
Propaganda
 
Mkuu Nguruvi3 , majadiliano kati ya CDM na CCM yalilenga katika kuhakikisha kuwa watanzania wanapata Haki zao zote zilizomo katika Katiba ya sasa.
Katiba ni muongozo wa sheria za nchi zinazopaswa kufuatwa na Watawala na Watawaliwa.
Haki ni takwa la kisheria, kwanini haki iombwe? Haki ikiombwa si haki tena bali Fadhila. Hapa ndipo FAM anapoonekana dhaifu. Unakwendaje kuomba haki ukijigamba ni Chama kikuu cha Upinzani!

Majadiliano a.k.a maridhiano yalikuwa na haja gani? Ni nani kati ya nani na juu ya nini!

CDM, kama chama kikuu cha upinzani kilikuwa kinawasemea watanzania ambao hawakuwa na mtu wa kuwasemea.
Sawa sawa na ndio maana hata Tusiokuwa na vyama tunajadili hii kwasababu Vyama vya siasa vina 'impact' katika maisha ya jamii yetu. Madhara ya kukosa upinzania Bungeni tumeyaona.
Hata hivyo, sauti za vyama lazima ziwe na ithbati, zisizo na utata na zenye kuaminika
Kuwaambia Bavicha watunze ndimi zao maana yake ni wasitumie lugha ya matusi na shombo wakati wanadai Katiba Mpya. Huko sio kuwakataza kuzungumzia Katiba Mpya unless lugha pekee iliyostahili ni ya matusi na shombo.
Kauli iliyompelekea awakemee vijana wake ni ile ya ' Hakieleweki isipokuwa Katiba mpya'' hili ni tusi?
Na hata yeye na chama chake waliendelea kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Kusema vingine ni kuwaonea.

Amandla...
Yeye alidai 'minimal reforms'' akisema muda wa Katiba ni mfupi.

Hakuna! narudia hakuna kiongozi wa CCM au Serikali aliyejitokeza tena kusema hilo.
Tayari FAM aligeuka msemaji wa timu ya Maridhiano, Vijana wake wakasalim amri wakisubiri Maridhiano.

Maridhiano yasiyo na definition ndicho chanzo cha ''revolt'' na ikitumiwa na Wapinzani wake vizuri ndio utakuwa mwisho wa FAM katika politics.
 
Mkuu Nguruvi3. Bado haujanijibu. Alternative kwa majadiliano ni nini?
Hkauna alternative ya Maridhiano! unless Katiba na NEC zipo mezani. Hizo ndizo agenda kuu
Kuachiwa watu wao , kurudishiwa mali n.k. havikupaswa kuchukua nafasi ya Katiba na Tume ya Uchaguzi.
Wagome kufanya majadiliano yeyote kabla ya kupata Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi?
Ndilo shinilizo alilowekewa JK akaukbali kuanzisha mchakato. Ilikuwa pressure tu
Hatua gani wachukue ili watu wao waachiwe?
Watu wao walikamatwa na kusingiziwa kesi ! Kilichotokea ni CDM kulipa ''ransom'

Hakuna majadiliano ya watu kuachiwa kwasababu next time CCM itafanya hivyo kama 'bargaining chip''
Hoja ilikuwa kuwaambia si kuomba maridhiano. Ukamatwe, usingiziwe kesi halafu uombe maridhiano! Please

ANC waliwaambia Mkaburu '' Usalama wa Mandela akitoka ni non-negotiable''
ANC wakasema '' Tujadili Katiba na South Africa post apartheid'' ANC hawakuta Mandela awe agenda!

Ulinzi wake ni haki ya Serikali iliyopo madarakani. Ikiwa kuachiliwa ilikuwa n sehemu ya mahjadiliano, ANC walikuwa tayari kuondoka na kumwacha Mandela aendelee kifungoni. That is leadership !
 
Hkauna alternative ya Maridhiano! unless Katiba na NEC zipo mezani. Hizo ndizo agenda kuu
Kuachiwa watu wao , kurudishiwa mali n.k. havikupaswa kuchukua nafasi ya Katiba na Tume ya Uchaguzi.
Asante sana Nguruvi3, kwa upande wangu nitaendelea kuwashukia kama mwewe wanaojaribu kuhalalisha vitendo vya rushwa kwa kutanguliza maslahi binafsi.

Mtanisamehe kwa lugha yangu ngumu lakini kwa nchi hii ilipofikia siwezi tena kutumia lugha laini kwa watu kama hao walio tayari kuuza utu wao kwa kipande cha mkate.

Nilikuwa mpenzi mkubwa wa Mbowe na tangu mwaka 2020 nilikuwa na imani kuwa, baada ya miaka 20, ataachia kiti na kupisha uongozi mpya kwa heshima na taadhima.

Bado nina imani hiyo. Najua anapata wakati mgumu kutoka kwa watu wanaomzunguka lakini, Mbowe, kwa hulka yake, najua atachukua maamuzi sahihi kabla ya 23/1/2025!
 
Hkauna alternative ya Maridhiano! unless Katiba na NEC zipo mezani. Hizo ndizo agenda kuu
Kuachiwa watu wao , kurudishiwa mali n.k. havikupaswa kuchukua nafasi ya Katiba na Tume ya Uchaguzi.
Kama nimekuelewa vizuri, unamlaumu Mbowe kwa kwa kuzungumzia watu kuachiwa, watu kurudishiwa mali zao, walio uhamishano kuhakikishiwa usalama wao, Covid-19,Mikutano ya hadhara ya kisiasa? Yote hayo unaona hayana maana mbele ya Katiba Mpya na Tume ya Uchaguzi iliyo huru? Sijui kama ungekuwa na ndugu yako rumande ameshitakiwa kwa kosa la mauaji? Kesi ambayo inapigwa dana dana kila siku kwa hiyo haujui huyo ndugu yako atakaa ndani kwa miaka mingapi. Na ndugu yako huyo alikuwa hana kipato cha maana na ameacha mke, watoto na wazazi wanaomtegemea. Unemwambia awe mvumilivu kwa sababu kukaa kwake ndani kutaifanya serikali ifanye marekebisho katika muundo wa Tume ya Uchaguzi. Mimi hapo natofautiana kabisa na wewe. Ninamuunga mkono kuwa maisha ya hao watu wasio na hatia, uwezo wa kufanya mikutano ya hadhara ni muhimu zaidi ya makubaliano yeyote kuhusu Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuachiwa kwa hao wapiganaji na kibali cha kufanya mikutano ya hadhara ni nyenzo muhimu katika kuwaelemisha wananchi kuhusu umuhimu wa Katiba Mpya ili kwa pamoja waweze kushirikiana kuipresha serikali ili ifanye mabadiliko hayo muhimu.
Ndilo shinilizo alilowekewa JK akaukbali kuanzisha mchakato. Ilikuwa pressure tu
Unazungumzia vitu viwili tofauti. JK hakuzuia mikutano ya hadhara. JK hakuwatia ndani wapinzani kwa kiasi kilichotokea baada ya utawala wake.
Watu wao walikamatwa na kusingiziwa kesi ! Kilichotokea ni CDM kulipa ''ransom'

Hakuna majadiliano ya watu kuachiwa kwasababu next time CCM itafanya hivyo kama 'bargaining chip''
Hoja ilikuwa kuwaambia si kuomba maridhiano. Ukamatwe, usingiziwe kesi halafu uombe maridhiano! Please
Unataka kutuambia kuwa wale watu walitiwa ndani kuzuia watu kudai Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi? Ninavyojua mimi ni kuwa wengi walikamatwa wakati wa uchaguzi. Wengi walikuwa wanapinga matokeo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi. Walichokuwa wanataka ni haki itendeke chini ya Tume iliyokuwepo wakati wa uchaguzi. Mbona Tume hiyo hiyo chini ya Katiba hiyo hiyo ilitangaza wagombea wengi kutoka vyama vya upinzani kuwa washindi? Na wapinzani hao waliweza kutoa presha kwa serikali iliyopo wakiwa ndani ya Bunge.
ANC waliwaambia Mkaburu '' Usalama wa Mandela akitoka ni non-negotiable''
ANC wakasema '' Tujadili Katiba na South Africa post apartheid'' ANC hawakuta Mandela awe agenda!

Ulinzi wake ni haki ya Serikali iliyopo madarakani. Ikiwa kuachiliwa ilikuwa n sehemu ya mahjadiliano, ANC walikuwa tayari kuondoka na kumwacha Mandela aendelee kifungoni. That is leadership !
Hii nayo mimi naikumbuka tofauti na wewe. Mandela alikataa masharti ya De Klerk yafuatayo 1) ku"renounce violence kama njia ya kupigana na mfumo wa apartheid. 2) kutii sheria za makaburu za usalama wa ndani. Na barua yake yakukataa masharti hayo ilisomwa katika mkutano wa hadhara na binti yake Zinzi. Suala la Katiba mpya na Afrika ya Kusini ya baadae hayakuwa sababu ya kukataa kukaa chini na makaburu. Alisema akikubali haya masharti atabakia kuwa mfungwa hata kama hayuko jela. Alisema pia kuwa makaburu wanatakiwa kuhalalisha chama cha ANC, waachie wafungwa wote wa kisiasa, waruhusu waliokuwa uhamishano warudi, watoe uhuru wa kufanya siasa na waji commit katika kuacha siasa za kibaguzi. Mkutano huo aliohutubia binti yake uliandaliwa na UDF kwa vile ANC bado kilikuwa hakitambuliwi. Katika barua yake alisisitiza pia mshikamano kati yake na Oliver Tambo kwa sababu kulikuwa na rumours kuwa ndani ya ANC kuna mpasuko.

Kabla ya yote hayo , mwaka 1991, Mandela akiwa bado mfungwa alikutana kwa siri na De Klerk nyumbani kwake Cape Town. Hapo ndipo walizungumzia mwelekeo wa Afrika Kusini na uwezekano wa kuachiwa Mandela. Hii ina tofauti gani na Mbowe kukutana na Samia? Mandela mwenyewe alisema ni baada ya mkutano huo ndio aliweza kuwaambia wanachama wenzake kuwa De Klerk ni tofauti na waliomtangulia na ni mtu ambae wanaweza kfikia nae maridhiano

Cha kukumbuka ni kuwa baada ya kuachiwa Mandela majadiliano yaliendelea kwa miaka mitano ndio Mandele akachaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini. Halafu nyinyi mnaamini miaka miwili ya majadiliano na chama ambacho hakina mpango wowote wa kutoka madarakani ( De Klerk aliishakubali kuwa siku za utawala wa kikaburu zimeisha) yataenda fasta kwa sababu kuna watu wanakuna Club House na kuweka Clip zao mitandaoni bila ya kuwa na mikutano ya hadhara na uhuru wa watu kukutana na kufanya shughuli za kisiasa. Hizo kwa kweli ni ndoto na kiongozi yeyote anayesema hilo litawezekana na muongo. Katiba Mpya halali haiwezi kupitishwa na Chadema na CCM peke hayo. Hata hiyo inayoitwa ya Warioba haiwezi kuanza kutumika bila kuangalia kama inakidhi matakwa ya wakati huu uliopo.

Katiba Mpya ya Afrika Kusini iliandaliwa na Bunge lililochaguliwa 1994 na ilianza kutumika 1997, ikichukuwa nafasi ya Katiba ya mpito ya mwaka 1993.

Amandla...
 
Kama nimekuelewa vizuri, unamlaumu Mbowe kwa kwa kuzungumzia watu kuachiwa, watu kurudishiwa mali zao, walio uhamishano kuhakikishiwa usalama wao, Covid-19,Mikutano ya hadhara ya kisiasa?
Ningeomba kueleweshwa. Katika maridhiano, FAM aliwaambia CCM kitu gani kuhusu hayo mambo tajwa ?
-Naomba mturuhusu tufanye mikutano ya hadhara !
-Naomba Watu wetu waliofungwa waachiliwe kwa hisani yenu!
-Tunahitaji fadhila zenu mturudishie mali zetu mlizochukua !
-Tafadhali sana wenzetu walioko uhamishoni waruhusiwe kupita mipakani wakija Tz!
-COVID-19 , tujadiliane namna gani watarejea chamani au watabaki kuwa Wabunge
Cha kukumbuka ni kuwa baada ya kuachiwa Mandela majadiliano yaliendelea kwa miaka mitano ndio Mandele akachaguliwa kuwa rais wa Afrika Kusini.
Struggle za South Africa ni tofauti! Wao walikuwa vitani! Mbowe hakuwa vitani
ANC walikuwa katika mazungumzo, FAM alikuwa katika Maridhiano!

ANC walifanya maridhiano baada ya ku abolish apartheid. Mbowe anatanguliza maridhiano bila kujua ni kati ya nani na nani na kwa ugomvi gani. Anakwenda kwenye maridhiano akiwa katika 'weak position'

Hata yeye alikiri udhaifu huo kule Iringa aliposema '' Niliitwa Ikulu na Rais, mimi nina kiburi gani cha kumkatalia''. Hii ni baada ya kuulizwa uharaka wa kukimbilia Ikulu bila consulatation na viongozi wenzake .
Kibaya zaidi aliporudi akashawishi wenzake na nina nukuu '' Mama ana ni njema katika maridhiano''
Mbowe akawananga wenzake ''' Hata kwenye chama chetu tuna wahafidhina wasiotaka maridhiano''
Akiwa Zanzibar akasema '' Wenzangu waliokataa maridhiano walikuwa sahihi''

Ndio maana tuna question, je, alijua anakwenda kufanya kuongea nini na nani na kwa muktadha gani
Halafu nyinyi mnaamini miaka miwili ya majadiliano na chama ambacho hakina mpango wowote wa kutoka madarakani ( De Klerk aliishakubali kuwa siku za utawala wa kikaburu zimeisha) yataenda fasta kwa sababu kuna watu wanakuna Club House na kuweka Clip zao mitandaoni bila ya kuwa na mikutano ya hadhara na uhuru wa watu kukutana na kufanya shughuli za kisiasa. Hizo kwa kweli ni ndoto na kiongozi yeyote anayesema hilo litawezekana na muongo.
Hapa una point kubwa sana! kwamba CCM hawataki kuondoka madarakani! Ni kweli
Hivi huoni kutumia mbinu zile zile miaka 21 ya FAM bila matokeo tofuati ina fit vizuri na definition ya Insanity.

In fact hii ndiyo sababu kubwa ya 'rebellion' , watu wamechoka na status quo!

Katiba Mpya halali haiwezi kupitishwa na Chadema na CCM peke hayo. Hata hiyo inayoitwa ya Warioba haiwezi kuanza kutumika bila kuangalia kama inakidhi matakwa ya wakati huu uliopo.
Hivi tungefanikiwa kupitisha Katiba ya Warioba 2014 unataka kusema leo tungekaa tena kujadili kama inakidhi nyakati zilizopo.

Ni kweli Katiba mpya ni jambo shirikishi, lakini process nzima lazima iwe na 'leaders'' ambao ni CCM na Chadema. Ikiwa CDM itajivua jukumu ipo siku ombwe litajazwa kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF
Katiba Mpya ya Afrika Kusini iliandaliwa na Bunge lililochaguliwa 1994 na ilianza kutumika 1997, ikichukuwa nafasi ya Katiba ya mpito ya mwaka 1993.

Amandla...
Sawa kabisa, hata ya Warioba ilikuwa na transition period ya 2014-2018
 
Ningeomba kueleweshwa. Katika maridhiano, FAM aliwaambia CCM kitu gani kuhusu hayo mambo tajwa ?
-Naomba mturuhusu tufanye mikutano ya hadhara !
-Naomba Watu wetu waliofungwa waachiliwe kwa hisani yenu!
-Tunahitaji fadhila zenu mturudishie mali zetu mlizochukua !
-Tafadhali sana wenzetu walioko uhamishoni waruhusiwe kupita mipakani wakija Tz!
-COVID-19 , tujadiliane namna gani watarejea chamani au watabaki kuwa Wabunge
Mimi sio Mbowe na simo katika Kuu. Kwa kauli ya Mbowe ni kwamba alipoenda Ikulu baada ya kutoka gerezani, Rais alimuuliza chama chake kinataka nini. Mbowe akamuambia cha msingi kabisa ni kuwa badala kuhubiri amani wahubiri haki. Akamwambia kuwa inabidi aongee kwanza na wenzake kabla ya kuendelea na mazungumzo. Akapeleka suala kwenye Kamati Kuu ambapo tunaambiwa kuna wengine hawakutaka mazungumzo ya aina yeyote kabla ya kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuna wengine wakamuunga mkono kuwa mazungumzo yaanze na mahitaji ya chama yawe hayo uliotaja pamoja na kuanzishwa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Sidhani kama waliomba bali walisema:
1. Zuio haramu la mikutano ya hadhara liondolewe.
2. Watu waliofungwa waachiwe na wale ambao kesi zao zilikuwa zinaendelea zifutwe.
3. Mali zilizoporwa zirudishwe na akaunti zilizofungwa zifunguliwe.
4. Wanachama waliokuwa uhamishoni wahakikishiwe usala wao ili waweze kurudi.
5. Covid-19 waondolewe Bungeni kwa sababu hawastahili kuwepo mle. Mbowe hajawahi kuzungumzia kuwareesha chamani. Kama alivyosema hivi karibuni kuwa suala la kuwasamehe ni moot kwa sababu hamna hata mmoja aliyeomba msamaha. Aidha, suala la kuwareesha chamani haliwezi kuzungumzwa na CCM.
6. Mchakato wa Katiba Mpya uanze tena na vyama viwe na uhuru wa kuijadili.
7. Iundwe Tume Mpya ya Uchaguzi itakayo kuwa huru.
Majadilano yakaanza na CCM wakasema ewala kwa 1 mpaka 4 lakini ya 5 mpaka 7 wakapata kigugumizi. Mbowe na Chadema hawakubembeleza kitu kama unavyotaka tuamini. Na Makamu Mwenyekiti wa Chadema alitoa matamko kuunga mkono yanavyoendelea lakini with caution.
Struggle za South Africa ni tofauti! Wao walikuwa vitani! Mbowe hakuwa vitani
ANC walikuwa katika mazungumzo, FAM alikuwa katika Maridhiano!
Ingawa South Afrika walikuwa vitani lakini walikuwa wanafuata Katiba yao ambayo iliruhusu vyama vilvyo halalishwa kufanya shughuli za kisiasa. Ndio maana Zinzi Mandela hakufungwa aliposoma barua ya baba ikikataa masharti mengine ya makaburu alifanya hivyo hadharani. Wakati kwetu vyama vya upinzani viliambiwa kuwa akiitokeza mtu yeyote katika mikutano/maandamano yao atapigwa kipigo cha mbwa mwizi! Na vilipotoa taarifa ya mkutano waliambiwa wasifanye kwa sababu za kiusalama.
Ili tuweze kuelewana vizuri naomba uniambie tofauti ya mazungumzo na maridhiano. Ninavyojua mimi kuwa lengo la mazungumzo yeyote ni kufikia kwenye maridhiano. Chadema walikuwa hawajafika kwenye maridhiano kamili kwa hiyo kusema kuwa walikuwa kwenye "maridhiano" ni kuwa disingenous. Na walipoona kuwa hakuna dalili kuwa mwenzao anajadiliana in good faith wakajitoa. Hata hayo mazungumzo ya ANC lengo lilikuwa kufikia kwenye maridhiano.
Njia mbadala ya mazungumzo ni wananchi na watu wengine kulazimisha kwa njia kama maandamano, migomo, kushtaki kwa nchi rafiki n.k. Mimi siamini kuwa hizo njia zingeleta matokeo ya maana hata wale ambao sasa hivi ndio wako mstari wa mbele kumsema Mbowe kuwa msaliti walishindwa kuandamana huko katika nchi ambazo zina uhuru kamili wa wakazi wake kuandamana kupinga jambo lolote. Washington sana sana walijitokeza watu 10 na ushee. London hivyo hivyo. Rais na viongozi wenzake mara chungu mzima anatembelea nchi zao lakini hatuwaoni wakiandamana. Wanachojua kufanya ni kuandaa mikutano baina yao na viongozi wa vyama vya upinzani wakitembelea nchi zao. Halafu hao hao wanamwambia Mbowe asihangaike kuwatoa watu maskini waliofungwa mpaka wao watakapotoa njia mbadala ambayo mpaka leo bado ni siri kubwa! Kuweni na huruma na wenzenu. Ninachowashangaa ni kwa nini hizo njia mbadala hazikufanyika wakati mazungumzo ya maridhiano yanafanyika! Samahani, nimekosea hapo. Kumbe yalifanyika na Makamu Mwenyekiti alishiriki vizuri na aliwasifia polisi kwa kazi nzuri waliyofanya ya kutunza amani. Lakini yote hayo mmeyasahau na kusema kuwa Mwenyekiti alizuia njia mbadala. Kuweni na aibu kidogo.
ANC walifanya maridhiano baada ya ku abolish apartheid. Mbowe anatanguliza maridhiano bila kujua ni kati ya nani na nani na kwa ugomvi gani. Anakwenda kwenye maridhiano akiwa katika 'weak position'
ANC walifanya mazungumzo wakati apartheid ingalipo. Mbowe ameingia katika mazungumzo akidai haki ambazo aliamini zimeminywa na serikali pasipo halali. Naomba niambie strong position" ambayo Mbowe aliiacha ni ipi? Kununa nyumbani na kuwa na press conference na mashirika ya nje akilalamika kuwa haki zao zimeminywa? Akiulizwa mbona mwenzako yuko tayari kuyajadili lakini wewe ndio kikwazo angewajibu nini? Kwamba anaogopa kukosana na Makamu wake? Wakati watu wanaendelea kusota jela na rumande bila uhakika wa lini watatoka?
Hata bila kibali cha maandamano, Mbowe hakuacha kuhimiza yafanyike. Unfortunately Makamu Mwenyekiti shujaa alikuwa anaingia gizani au anajiweka katika mkao wa kuzuiwa kuhudhuria!
Hata yeye alikiri udhaifu huo kule Iringa aliposema '' Niliitwa Ikulu na Rais, mimi nina kiburi gani cha kumkatalia''. Hii ni baada ya kuulizwa uharaka wa kukimbilia Ikulu bila consulatation na viongozi wenzake .
Alijibu sahihi. Maana hamna faida yeyote ambayo angepata kwa kumkatalia. Hakujua anaitiwa nini. Labda alikuwa anaenda kupewa pole. Au kunywa juisi tu na kujadili kuhusu wajukuu zao. Asingejua dhumuni la wito ule bila kuuitikia. Hakwenda Ikulu kuanza majadiliano bali kusikia ameitiwa nini. Ilikuwa pia nafasi ya kumpima Rais kama ambavyo Mandela alivyompima de Klerk. Alipojua sababu za wito akawaambia wenzake na wakakubaliana ya kushiriki kwenye majadiliano.
Kibaya zaidi aliporudi akashawishi wenzake na nina nukuu '' Mama ana ni njema katika maridhiano''
Naam. Wengi waliamini hilo. Sio peke yake. Kosa liko wapi?
Mbowe akawananga wenzake ''' Hata kwenye chama chetu tuna wahafidhina wasiotaka maridhiano''
Kwani ilikuwa uongo? Wahafidhina hao walikuwepo pande zote. Nakumbuka zilikuwa zina leak taarifa kuhusu push back aliyokuwa anapata Makamu Mwenyekiti wa CCM kuhusu hili suala. Maridhiano yangefikiwa lingekuwa jambo jema kwa taifa letu

Akiwa Zanzibar akasema '' Wenzangu waliokataa maridhiano walikuwa sahihi''

Ni alama ya ukomavu wake kuwa hasiti kusema kuwa alikosea. Mimi nadhani hakukosea lakini mimi sio Mbowe.

Ndio maana tuna question, je, alijua anakwenda kufanya kuongea nini na nani na kwa muktadha gani
Ameeleza dhumuni kwa ufasaha lakini mmeweka pamba masikioni. Alipoitwa mara ya kwanza hakujua sababu ya wito. Baada ya kupata kibali cha Kamati Kuu Chadema ikaunda jopo la watu wakuongea na counterparts wao wa CCM.
Hapa una point kubwa sana! kwamba CCM hawataki kuondoka madarakani! Ni kweli
Hivi huoni kutumia mbinu zile zile miaka 21 ya FAM bila matokeo tofuati ina fit vizuri na definition ya Insanity.
Mbinu zilizotumika mpaka utawala wa awamu ya 5 zilileta mafanikio makubwa. Kushindwa kwa CDM katika chaguzi zilizofanyika wakati wa awamu ya 5 na 6 yalitokana na aina ya utawala uliokuwepo. Tofauti na unavyodai, Mbowe amekuwa akibadilisha mbinu zake kulingana na uongozi uliokuwepo. Alimpokea Lowassa kwa sababu alijua kuwa ni nafasi ya kujiongezea wabunge , kura za wabunge na rais. Idadi ile ilikipa CDM platform kubwa sana ya kushindana na CCM katika mazingira magumu. Hata uchaguzi ujao angeweza kufanya vizuri kwa sababu kwa kushiriki katika uchaguzi wa hivi karibuni ame wa expose CCM kwa jamii sio tu ya Tanzania bali dunia nzima kuwa hawana nia ya kuachia madaraka kirahisi. Bahati mbaya, mtu wa karibu amemu undermine under the "mistaken belief" kuwa anaweza kutembea juu ya maji.
In fact hii ndiyo sababu kubwa ya 'rebellion' , watu wamechoka na status quo!
Hamna rebellion hapa. Ni watu wachache wenye sauti kubwa kwenye majukwaa kama haya wanataka kuwa king makers. Hao watu wangekuwa wamechoka na status quo wangeandamana pale walipoombwa kuandamana. Shida yetu sisi ni kila wakati tunataka mtu wa kutuokoa badala ya kujipigania wenyewe. Ndio maana tunajazana kwa Babu wa Loliondo, Mwamposa, Kiboko wa Wachawi n.k. kwa sababu wanatuahidi mafanikio bila kufanya kazi na tiba isiyo na maumivu. Huyu mnae mpigia debe ni design hiyo. Atakapoona mambo ni magumu atawalaumu wenzake na kuwaacha waendelee wenyewe na mapigano.
Hivi tungefanikiwa kupitisha Katiba ya Warioba 2014 unataka kusema leo tungekaa tena kujadili kama inakidhi nyakati zilizopo.
Hamna Katiba isiyofanyiwa Amendments. Hata ya Warioba ingefanyiwa Amendments.
Ni kweli Katiba mpya ni jambo shirikishi, lakini process nzima lazima iwe na 'leaders'' ambao ni CCM na Chadema. Ikiwa CDM itajivua jukumu ipo siku ombwe litajazwa kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF
Na atakae sababisha yote hayo ni Makamu Mwenyekiti wa CDM. Ninachojua ni kuwa hata kama CDM itatetereka Mbowe ana uwezo wa kuijenga tena. Hilo ametuonyesha.

Sawa kabisa, hata ya Warioba ilikuwa na transition period ya 2014-2018

South Africa walikuwa na Katiba ya Mpito. Unataka kutuambia kuwa ya Warioba na yenyewe ilikuwa ya mpito?

Kama wanavyosema wamarekani "FAFO"

Amandla....
 
Mheshimiwa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe, ukitangaza leo kwamba baada ya tafakuri nzito umeamua kutogombea kwa mara nyingine uenyekiti wa Chadema leo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja.
  1. Utaijengea CHADEMA heshima
  2. Utajijengea heshima kubwa zaidi
Kwa kuijengea CHADEMA heshima utakuwa umefuta kabisa dhana ile ya bila Mbowe hakuna CHADEMA hivyo kudhihirisha ukomavu wa CHADEMA kama chama chenye misingi imara.

Kwa kujijengea heshima utakuwa umedhihirisha ukomavu wako kidemokrasia kama mstaafu aliyeheshimu, kutetea na kulinda demokrasia kwa vitendo ndani na nje ya uongozi.

Ningependa kuwaona mmekaa pamoja wakati ukitangaza uamuzi wako huo na nakuhakikishia, utashangaa jinsi wananchi wengi wazalendo wakatavyoupokea uamuzi wako huo.
Apumuzike tu amefanya mengi
 
...Akapeleka suala kwenye Kamati Kuu wengine hawakutaka mazungumzo ya aina yeyote kabla ya kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuna wengine wakamuunga mkono kuwa mazungumzo yaanze
Kwa hoja hii mimi si CDM wala sipo hata karibu na ofisi zao. Sijui nini kilijiri lakini nadhani kulikuwa na ku bulldoze waliokataa. Sijui kama kura zilitumika na sijui kama hoja za waliokataa ziliangaliwa kwa ubora. Sijui
Ninachokijua, waliokataa ni vigogo waandamizi ! na hili linaeleza jambo.
Ili tuweze kuelewana vizuri naomba uniambie tofauti ya mazungumzo na maridhiano.
Mazungumzo (dialogue) hutokea kati ya wawili au zaidi katika kubadilishana fikra na mawazo
Maridhiano (reconcilliation) ni upatanishi unaoleta muafaka baada ya pande husika kuhitilafiana

Hili la MARIDHIANO hatukulizua, tumeliazima kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh FAM

Kwa mujibu wake, kulikuwa na Maridhiano 1, wakati wa JPM ambayo hayakuwa na matunda
Alichokwenda kuongea na Mh Rais ilikuwa kutafuta maridhiano 2 ya kisiasa nchini. Ni kwa mujibu wake

Kwa Maana ya maridhiano hapo juu, tuna maswali; ni pande ngapi zilihitifiana, je zilihitilafiana kwa jambo gani, na wahusika ni akina nani.
Ninavyojua mimi kuwa lengo la mazungumzo yeyote ni kufikia kwenye maridhiano.
Hapana, lengo la mazungumzo ni kuwa na Muafaka! consensus
Chadema walikuwa hawajafika kwenye maridhiano kamili kwa hiyo kusema kuwa walikuwa kwenye "maridhiano" ni kuwa disingenous.
Hapa unanioea ! Aliyeleta neno Maridhiano katika kikoa (Domain) ni FAM.
Amelitumia katika kila mkutano. Tafadhali rejelea clip zake
Hata hayo mazungumzo ya ANC lengo lilikuwa kufikia kwenye maridhiano.
Of course, baada ya kuwa na Muafaka (concensus) kuhusu South Africa ikiwemo Katiba, iliundwa timu ya Maridhiano(reconciliation) chini ya Askofu D.Tutu (R.I.P) iliyoitwa Truth and reconciliation Commission. Kwa S.Africa Maridhiano yali conclude the process. Kwa FAM alianza na Maridhiano ndio maana tnapata shida ya kumwelewa
Njia mbadala ya mazungumzo ni wananchi na watu wengine kulazimisha kwa njia kama maandamano, migomo, kushtaki kwa nchi rafiki n.k. Mimi siamininjia zingeleta matokeo ya maana hata wale ambao sasa hivi ndio wako mstari wa mbele kumsema Mbowe kuwa msaliti walishindwa kuandamana huko katika nchi ambazo zina uhuru kamili wa wakazi wake kuandamana kupinga jambo lolote. Washington sana sana walijitokeza watu 10 na ushee. London hivyo hivyo. Rais na viongozi wenzake mara chungu mzima anatembelea nchi zao lakini hatuwaoni wakiandamana.
Kuna siku Rais alibadili njia na kutokea uani. Ilikuwa notable . Tu criticise na kutoa credit inapobidi
Ninachowashangaa ni kwa nini hizo njia mbadala hazikufanyika wakati mazungumzo ya maridhiano yanafanyika!.
Haiwezekani kuwa na 'mbadala' wakati Mwenyekiti yupo katika Maridhiano.

Mfano mzuri ni pale Tanga wakati wa Mazishi ya Mzee Kibao (Pumzika kwa amani).
Kuna watu walitaka yule bwana asiongee kabisa! M/Kiti akasimama na kusema '' hapana ataongea'' na yule Bw akasema ''msikilizeni Mwenyekiti wenu, hakusema Msikilizeni FAM''.
Mafano 2, BAVICHA waliambiwa na M/Kiti wachunge ndimi zao! kwa maana wasije vuruga Maridhiano.
Wahafidhina hao walikuwepo pande zote. Nakumbuka zilikuwa zina leak taarifa kuhusu push back aliyokuwa anapata Makamu Mwenyekiti wa CCM kuhusu hili suala. Maridhiano yangefikiwa lingekuwa jambo jema kwa taifa letu
Kutofautiana mitazamo hakufanyi awaye awe Mhafidhina. Neno hilo alilitumia FAM kuwadhalilisha wasiokubaliana naye. Kumbuka ukitaka kumuua Mbwa mpe jina baya kwanzaAngeweza kusema wasioafiki!

Hapo ndipo ukaona wahafidhina wakakaa pembeni jambo unalosema '' waliingia gizani''.
Akiwa Zanzibar akasema '' Wenzangu waliokataa maridhiano walikuwa sahihi''
Ni alama ya ukomavu wake kuwa hasiti kusema kuwa alikosea. Mimi nadhani hakukosea lakini mimi sio Mbowe.
Wakati wa JPM aliomba maridhiano yakafeli, na sasa ameomba yamefeli.
Huwezi kufeli kila mara ukasema ni ukomavu ukizingatia experience ya miaka 21 kama Mwenyekiti na 33 katika siasa.
Hamna rebellion hapa. Ni watu wachache wenye sauti kubwa kwenye majukwaa kama haya wanataka kuwa king makers.
Ni lini FAM aliwahi kukabiliwa na sauti nyingi kama sasa! Hii ni rebellion baada ya incessant failures

Ni rebellion baada ya kuona CDM haina msimamo imepoteza uelekeo na inachanganya Wanachama wake
Ni rebellion baada ya kuona same old tricks. Ni rebellion inayotokana na kufanya kile kile kwa def ya insanity
Hao watu wangekuwa wamechoka na status quo wangeandamana pale walipoombwa kuandamana.
Well, Watu hawakuwa na uhakika kama wakiandamana M/Kiti atakuwepo au ataibukia Ikulu.
Kumbuka kuwa Watu walikuwa Mahakama Kuu wakikabiliana na FFU kabla ya kuona picha za FAM Ikulu.
Hamna Katiba isiyofanyiwa Amendments. Hata ya Warioba ingefanyiwa Amendments.
Katiba ingekuwa na miaka 6 tu. Jiulize ya 1977 imefanyiwa amendments ngapi katika average ya miaka.

FAM kuzungumzia ufinyu wa muda ilikuwa kosa! Yeye hakupaswa kuwa sehemu ya serikali! ni Mpinzani
Muda ulikuwepo lakini Maridhiano yalimtia kibano, akageuka kuwa msemaji wa Kamati ya Maridhiano
Na atakae sababisha yote hayo ni Makamu Mwenyekiti wa CDM. Ninachojua ni kuwa hata kama CDM itatetereka Mbowe ana uwezo wa kuijenga tena. Hilo ametuonyesha.
Nakuhakikishia wakati huu itakuwa tofauti sana. Huko nyuma alikuwa na support ya Bigwigs na Wanachama.
This time hana zaidi ya nusu ya Wanachama. Please kumbuka siongelei wajumbe wa mkutano mkuu.
Kama wanavyosema wamarekani "FAFO"
😂 nimeongeza msamiati.
 
Mimi sio Mbowe na simo katika Kuu. Kwa kauli ya Mbowe ni kwamba alipoenda Ikulu baada ya kutoka gerezani, Rais alimuuliza chama chake kinataka nini.
Kwa kumnukuu James Hadley Chase, "Believe this and you will believe anything!" Mfungwa (gaidi) unatolewa gerezani, unakaribishwa Ikulu na kuulizwa ungependa upewe nini!

Hii inanikumbusha issue ya Covid - 19. Mtu anatolewa mahabusu kinyemela usiku usiku ili awahi uapisho wa kuwa mbunge wa viti maalum, really?
Kama wanavyosema wamarekani "FAFO"
Yeah "eff around and find out" ni tisho kwetu tunaopinga usultani Chadema, kwamba tusithubutu kuchezea moto la sivyo tusubiri kuungua kama hatujaungua!

Chini ya uongozi wa Mh. Tundu Antiphas Lissu, naamini mambo kama haya hayana nafasi. Kwa kweli penye uchafu ndipo Chawa hupiga kambi!
 
Apumuzike tu amefanya mengi
Sawasawa na wengine hatujasita kutoa huo ushauri...hekima na busara ndizo zimetuongoza kumshauri kujitoa na kumuunga mkono Lissu.
 
Back
Top Bottom