Ningeomba kueleweshwa. Katika maridhiano, FAM aliwaambia CCM kitu gani kuhusu hayo mambo tajwa ?
-Naomba mturuhusu tufanye mikutano ya hadhara !
-Naomba Watu wetu waliofungwa waachiliwe kwa hisani yenu!
-Tunahitaji fadhila zenu mturudishie mali zetu mlizochukua !
-Tafadhali sana wenzetu walioko uhamishoni waruhusiwe kupita mipakani wakija Tz!
-COVID-19 , tujadiliane namna gani watarejea chamani au watabaki kuwa Wabunge
Mimi sio Mbowe na simo katika Kuu. Kwa kauli ya Mbowe ni kwamba alipoenda Ikulu baada ya kutoka gerezani, Rais alimuuliza chama chake kinataka nini. Mbowe akamuambia cha msingi kabisa ni kuwa badala kuhubiri amani wahubiri haki. Akamwambia kuwa inabidi aongee kwanza na wenzake kabla ya kuendelea na mazungumzo. Akapeleka suala kwenye Kamati Kuu ambapo tunaambiwa kuna wengine hawakutaka mazungumzo ya aina yeyote kabla ya kupatikana Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Kuna wengine wakamuunga mkono kuwa mazungumzo yaanze na mahitaji ya chama yawe hayo uliotaja pamoja na kuanzishwa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya. Sidhani kama waliomba bali walisema:
1. Zuio haramu la mikutano ya hadhara liondolewe.
2. Watu waliofungwa waachiwe na wale ambao kesi zao zilikuwa zinaendelea zifutwe.
3. Mali zilizoporwa zirudishwe na akaunti zilizofungwa zifunguliwe.
4. Wanachama waliokuwa uhamishoni wahakikishiwe usala wao ili waweze kurudi.
5. Covid-19 waondolewe Bungeni kwa sababu hawastahili kuwepo mle. Mbowe hajawahi kuzungumzia kuwareesha chamani. Kama alivyosema hivi karibuni kuwa suala la kuwasamehe ni moot kwa sababu hamna hata mmoja aliyeomba msamaha. Aidha, suala la kuwareesha chamani haliwezi kuzungumzwa na CCM.
6. Mchakato wa Katiba Mpya uanze tena na vyama viwe na uhuru wa kuijadili.
7. Iundwe Tume Mpya ya Uchaguzi itakayo kuwa huru.
Majadilano yakaanza na CCM wakasema ewala kwa 1 mpaka 4 lakini ya 5 mpaka 7 wakapata kigugumizi. Mbowe na Chadema hawakubembeleza kitu kama unavyotaka tuamini. Na Makamu Mwenyekiti wa Chadema alitoa matamko kuunga mkono yanavyoendelea lakini with caution.
Struggle za South Africa ni tofauti! Wao walikuwa vitani! Mbowe hakuwa vitani
ANC walikuwa katika mazungumzo, FAM alikuwa katika Maridhiano!
Ingawa South Afrika walikuwa vitani lakini walikuwa wanafuata Katiba yao ambayo iliruhusu vyama vilvyo halalishwa kufanya shughuli za kisiasa. Ndio maana Zinzi Mandela hakufungwa aliposoma barua ya baba ikikataa masharti mengine ya makaburu alifanya hivyo hadharani. Wakati kwetu vyama vya upinzani viliambiwa kuwa akiitokeza mtu yeyote katika mikutano/maandamano yao atapigwa kipigo cha mbwa mwizi! Na vilipotoa taarifa ya mkutano waliambiwa wasifanye kwa sababu za kiusalama.
Ili tuweze kuelewana vizuri naomba uniambie tofauti ya mazungumzo na maridhiano. Ninavyojua mimi kuwa lengo la mazungumzo yeyote ni kufikia kwenye maridhiano. Chadema walikuwa hawajafika kwenye maridhiano kamili kwa hiyo kusema kuwa walikuwa kwenye "maridhiano" ni kuwa disingenous. Na walipoona kuwa hakuna dalili kuwa mwenzao anajadiliana in good faith wakajitoa. Hata hayo mazungumzo ya ANC lengo lilikuwa kufikia kwenye maridhiano.
Njia mbadala ya mazungumzo ni wananchi na watu wengine kulazimisha kwa njia kama maandamano, migomo, kushtaki kwa nchi rafiki n.k. Mimi siamini kuwa hizo njia zingeleta matokeo ya maana hata wale ambao sasa hivi ndio wako mstari wa mbele kumsema Mbowe kuwa msaliti walishindwa kuandamana huko katika nchi ambazo zina uhuru kamili wa wakazi wake kuandamana kupinga jambo lolote. Washington sana sana walijitokeza watu 10 na ushee. London hivyo hivyo. Rais na viongozi wenzake mara chungu mzima anatembelea nchi zao lakini hatuwaoni wakiandamana. Wanachojua kufanya ni kuandaa mikutano baina yao na viongozi wa vyama vya upinzani wakitembelea nchi zao. Halafu hao hao wanamwambia Mbowe asihangaike kuwatoa watu maskini waliofungwa mpaka wao watakapotoa njia mbadala ambayo mpaka leo bado ni siri kubwa! Kuweni na huruma na wenzenu. Ninachowashangaa ni kwa nini hizo njia mbadala hazikufanyika wakati mazungumzo ya maridhiano yanafanyika! Samahani, nimekosea hapo. Kumbe yalifanyika na Makamu Mwenyekiti alishiriki vizuri na aliwasifia polisi kwa kazi nzuri waliyofanya ya kutunza amani. Lakini yote hayo mmeyasahau na kusema kuwa Mwenyekiti alizuia njia mbadala. Kuweni na aibu kidogo.
ANC walifanya maridhiano baada ya ku abolish apartheid. Mbowe anatanguliza maridhiano bila kujua ni kati ya nani na nani na kwa ugomvi gani. Anakwenda kwenye maridhiano akiwa katika 'weak position'
ANC walifanya mazungumzo wakati apartheid ingalipo. Mbowe ameingia katika mazungumzo akidai haki ambazo aliamini zimeminywa na serikali pasipo halali. Naomba niambie strong position" ambayo Mbowe aliiacha ni ipi? Kununa nyumbani na kuwa na press conference na mashirika ya nje akilalamika kuwa haki zao zimeminywa? Akiulizwa mbona mwenzako yuko tayari kuyajadili lakini wewe ndio kikwazo angewajibu nini? Kwamba anaogopa kukosana na Makamu wake? Wakati watu wanaendelea kusota jela na rumande bila uhakika wa lini watatoka?
Hata bila kibali cha maandamano, Mbowe hakuacha kuhimiza yafanyike. Unfortunately Makamu Mwenyekiti shujaa alikuwa anaingia gizani au anajiweka katika mkao wa kuzuiwa kuhudhuria!
Hata yeye alikiri udhaifu huo kule Iringa aliposema '' Niliitwa Ikulu na Rais, mimi nina kiburi gani cha kumkatalia''. Hii ni baada ya kuulizwa uharaka wa kukimbilia Ikulu bila consulatation na viongozi wenzake .
Alijibu sahihi. Maana hamna faida yeyote ambayo angepata kwa kumkatalia. Hakujua anaitiwa nini. Labda alikuwa anaenda kupewa pole. Au kunywa juisi tu na kujadili kuhusu wajukuu zao. Asingejua dhumuni la wito ule bila kuuitikia. Hakwenda Ikulu kuanza majadiliano bali kusikia ameitiwa nini. Ilikuwa pia nafasi ya kumpima Rais kama ambavyo Mandela alivyompima de Klerk. Alipojua sababu za wito akawaambia wenzake na wakakubaliana ya kushiriki kwenye majadiliano.
Kibaya zaidi aliporudi akashawishi wenzake na nina nukuu '' Mama ana ni njema katika maridhiano''
Naam. Wengi waliamini hilo. Sio peke yake. Kosa liko wapi?
Mbowe akawananga wenzake ''' Hata kwenye chama chetu tuna wahafidhina wasiotaka maridhiano''
Kwani ilikuwa uongo? Wahafidhina hao walikuwepo pande zote. Nakumbuka zilikuwa zina leak taarifa kuhusu push back aliyokuwa anapata Makamu Mwenyekiti wa CCM kuhusu hili suala. Maridhiano yangefikiwa lingekuwa jambo jema kwa taifa letu
Akiwa Zanzibar akasema '' Wenzangu waliokataa maridhiano walikuwa sahihi''
Ni alama ya ukomavu wake kuwa hasiti kusema kuwa alikosea. Mimi nadhani hakukosea lakini mimi sio Mbowe.
Ndio maana tuna question, je, alijua anakwenda kufanya kuongea nini na nani na kwa muktadha gani
Ameeleza dhumuni kwa ufasaha lakini mmeweka pamba masikioni. Alipoitwa mara ya kwanza hakujua sababu ya wito. Baada ya kupata kibali cha Kamati Kuu Chadema ikaunda jopo la watu wakuongea na counterparts wao wa CCM.
Hapa una point kubwa sana! kwamba CCM hawataki kuondoka madarakani! Ni kweli
Hivi huoni kutumia mbinu zile zile miaka 21 ya FAM bila matokeo tofuati ina fit vizuri na definition ya Insanity.
Mbinu zilizotumika mpaka utawala wa awamu ya 5 zilileta mafanikio makubwa. Kushindwa kwa CDM katika chaguzi zilizofanyika wakati wa awamu ya 5 na 6 yalitokana na aina ya utawala uliokuwepo. Tofauti na unavyodai, Mbowe amekuwa akibadilisha mbinu zake kulingana na uongozi uliokuwepo. Alimpokea Lowassa kwa sababu alijua kuwa ni nafasi ya kujiongezea wabunge , kura za wabunge na rais. Idadi ile ilikipa CDM platform kubwa sana ya kushindana na CCM katika mazingira magumu. Hata uchaguzi ujao angeweza kufanya vizuri kwa sababu kwa kushiriki katika uchaguzi wa hivi karibuni ame wa expose CCM kwa jamii sio tu ya Tanzania bali dunia nzima kuwa hawana nia ya kuachia madaraka kirahisi. Bahati mbaya, mtu wa karibu amemu undermine under the "mistaken belief" kuwa anaweza kutembea juu ya maji.
In fact hii ndiyo sababu kubwa ya 'rebellion' , watu wamechoka na status quo!
Hamna rebellion hapa. Ni watu wachache wenye sauti kubwa kwenye majukwaa kama haya wanataka kuwa king makers. Hao watu wangekuwa wamechoka na status quo wangeandamana pale walipoombwa kuandamana. Shida yetu sisi ni kila wakati tunataka mtu wa kutuokoa badala ya kujipigania wenyewe. Ndio maana tunajazana kwa Babu wa Loliondo, Mwamposa, Kiboko wa Wachawi n.k. kwa sababu wanatuahidi mafanikio bila kufanya kazi na tiba isiyo na maumivu. Huyu mnae mpigia debe ni design hiyo. Atakapoona mambo ni magumu atawalaumu wenzake na kuwaacha waendelee wenyewe na mapigano.
Hivi tungefanikiwa kupitisha Katiba ya Warioba 2014 unataka kusema leo tungekaa tena kujadili kama inakidhi nyakati zilizopo.
Hamna Katiba isiyofanyiwa Amendments. Hata ya Warioba ingefanyiwa Amendments.
Ni kweli Katiba mpya ni jambo shirikishi, lakini process nzima lazima iwe na 'leaders'' ambao ni CCM na Chadema. Ikiwa CDM itajivua jukumu ipo siku ombwe litajazwa kama ilivyokuwa kwa NCCR na CUF
Na atakae sababisha yote hayo ni Makamu Mwenyekiti wa CDM. Ninachojua ni kuwa hata kama CDM itatetereka Mbowe ana uwezo wa kuijenga tena. Hilo ametuonyesha.
Sawa kabisa, hata ya Warioba ilikuwa na transition period ya 2014-2018
South Africa walikuwa na Katiba ya Mpito. Unataka kutuambia kuwa ya Warioba na yenyewe ilikuwa ya mpito?
Kama wanavyosema wamarekani "FAFO"
Amandla....