Uchaguzi 2020 Mbowe itampa wakati mgumu sana kumnadi Lissu

Uchaguzi 2020 Mbowe itampa wakati mgumu sana kumnadi Lissu

Uko sahihi sana mkuu. Nikuongezee hili kwenye ufahamu wako, je unazijua principles za mgeni?
  1. Siku ya kwanza watu wanakuwa na hamu naye, hata yeye anakuwa na hamu sana na watu, sababu siku nyingi hawajaonani
  2. Siku ya pili bado hamu iko pale pale ila si kama ya siku ya kwanza
  3. Siku ya tatu watu wameshaanza kumzoea
  4. Siku ya nne watu wameshaanza kumchoka
  5. Ya tano, anaanza kutamani kurudi kwake
  6. Kasi ya kurudi ndo inazidi kupanda
  7. Mgeni hapa hana hamu tena ya kukaa
  8. Lazima atoke
Watu saizi wameshamzoe Lisu ndugu yangu, ndo na kauli zimeanza kubadilika
Kama wamemzoea mngemtuma mvuta bange wenu Ole Sabaya na wavuta bange wenzake kwenda kuharibu ziara yake ya kutafuta wadhanini Arusha na Hai??? Nyie jamaa hadi shetani naisi anawashangaa
 
Kama amechacha kwa nini mnawehuka humu kila saa kuanzisha thread zinazomuhusu???? Kawashika pabaya na bado nawaambia!!! Lazima mtembee uchi nyie lumumba hadi ifike october
Tunaujulisha umma ili usije ukafanya makosa, hatuki na raisi ambaye anaremotiwa na mabeberu. Hujui ana chip yule?
 
Ni wachache sana waonao hili mkuu, wengi ni washabiki hawajui lolote, ila wachache tumeliona hili

Mbowe ni nani? Sisi tunamtaka Lisu na hatutaki mtu yoyote awe na furaha. Kwa taarifa yako Lisu hahitaji kunadiwa na yoyote maana anakubalika. Hiyo ramli chonganishi mpelekeeni jiwe, maana ndio mkimpelekea anawapa hela ya kununua waunga juhudi.
 
Kama wamemzoea mngemtuma mvuta bange wenu Ole Sabaya na wavuta bange wenzake kwenda kuharibu ziara yake ya kutafuta wadhanini Arusha na Hai??? Nyie jamaa hadi shetani naisi anawashangaa
Unauhakika na unachokiongea? Waliomfanyia makelele Magu kule mbeya walitumwa? Hivi we unajua Tl anakubalika na kila MTU?
 
Lissu si mwanasiasa ila analazimisha siasa matokeo yake kila anapohutubia wananchi badala ya kuongeza kura anapunguza kura na kitu cha kushangaza kwa vijana na wapenzi wa Chadema hawalioni hilo ingawaje baadhi ya viongozi wa juu wa Chadema walishaliona tatizo ila kutokana na shinikizo la wachama wao hawakuwa na jinsi.
Kama analazimisha siasa kwa nini mlimpiga risasi???
 
Tunaujulisha umma ili usije ukafanya makosa, hatuki na raisi ambaye anaremotiwa na mabeberu. Hujui ana chip yule?

Umeanzisha uzi ili uongee huu utoto?
 
Unauhakika na unachokiongea? Waliomfanyia makelele Magu kule mbeya walitumwa? Hivi we unajua Tl anakubalika na kila MTU?
Walimfanyia kelele Magu Mbeya lini???

Uko Tanzania kweli ???Au wewe ni mmoja wa wale wahuni mlioenda kufanya fujo kwa Lissu huku mkisema mnamlinda Dc Sabaya???
 
Ndugu yangu, ana human microchip yule kam hujui, tatizo vijana wa ufipa wavivu sana kuchunguza vitu, mnabakia ushabiki tu
Hujui kuwa magufuli ana pacemaker aliyowekewa na wajerumani??
 
Hivi wewe unamjua Magu, usijitoe ufahamu, Magu is one of the best president of our life time ever! Dunia nzima wanamjua wewe usilete utani kabisa. Amelipa heshima kubwa saba taifa letu

Taifa letu limepewa heshima na Nyerere tu
Alafu acha ushabiki basi, unakuwa shabiki Mpaka unapitiliza haha
 
Mbowe ni nani? Sisi tunamtaka Lisu na hatutaki mtu yoyote awe na furaha. Kwa taarifa yako Lisu hahitaji kunadiwa na yoyote maana anakubalika. Hiyo ramli chonganishi mpelekeeni jiwe, maana ndio mkimpelekea anawapa hela ya kununua waunga juhudi.
Muulize kilichompata mwanza ndo utajua nyie vijana mtabakia kubwabwanja tu. Hapo ndugu yangu tl anategemea kura za huruma ya wananchi Period. Ndo maana Nyerere alisema kazi ya kujenga nchi ni ngumu. Tutapa watetezi wa mabepari humuhumu, unasemaje raisi wako na makinikia?
 
Muulize kilichompata mwanza ndo utajua nyie vijana mtabakia kubwabwanja tu. Hapo ndugu yangu tl anategemea kura za huruma ya wananchi Period. Ndo maana Nyerere alisema kazi ya kujenga nchi ni ngumu. Tutapa watetezi wa mabepari humuhumu, unasemaje raisi wako na makinikia?
Mtetezi wa mabeberu kivipi??? Embu fafanua ueleweke ????

Alafu ukiwa unafafanua tuambie kampuni inayojenga uwanja wa ndege Chato ni ya nani??? Na ujenzi wa ule uwanja unatumia gharama gani na zilipitia utaratibu upi kuidhinishwa???
 
Taifa letu limepewa heshima na Nyerere tu
Alafu acha ushabiki basi, unakuwa shabiki Mpaka unapitiliza haha
Hivi wewe uko tz? Yawezekana hata hujui tuko kwenye uchumi wa kati, ndo unaamini tz watu wankufa na kuzikwa usiku sababu ya korona, jitafakari
 
Kipindi hichi kuna kundi moja la siasa watakuja kuhadithia kitakachowatokea yan hawatoamin kabisa kile ambacho kitamkuta mgombea wao kwenye sanduku la kura ni suala LA muda tu
 
Ndugu zangu,

Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa siku ya leo.

Katika uchaguzi ambao niliufuatilia kwa karibu kubwa sana tangia nianze kufuatilia siasa na wanasiasa, basi ulikuwa ule wa 2015. Ulikuwa uchaguzi wa kipekee sana kuwahi kutokea hapa nchini, na ulikuwa uchaguzi mgumu sana kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ila CCM walicheza karata kubwa sana ya kumweka Mh. Magufuli. Kwa kutumia rekodi za nyuma za umahili wake wa uchapazi kazi katika kila wizara aliyoteuliwa, ilinifanya kura yangu nimpe huyu ndugu. Na kama CCM wangempitisha Membe, basi kura yangu ingeenda kwa Mh. Lowasa. Na itachukua miaka mingi sana kuwa na uchaguzi kama ule.

Kamari ambayo waliicheza Ukawa, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kumkaribisa Mh. Lowasa (), Mh. Mbowe alikuwa na furaha mno na confidence kubwa sana huku alikuwa anajua kabisa Lowasa anaenda kuingia Ikulu, kulingana na nyota ya siasa amabayo Lowasa alikuwa nayo ambayo ilisababishwa na kuwa na maandalizi ya muda mrefu kwa nafasi hii kubwa kabisa katika kulitumikia taifa. Kama ukisikia mafuriko ya watu kipindi cha Mh. Lowasa, basi yalikuwa mafuriko kwelikweli, Tundulisu hawezi hata kumfikia nusu yake ()

().

Kipindi hiki naona kama Mh. Mbowe hana ile confidence kabisa ambayo aliyokuwa nayo 2015 kipindi cha Mh. Lowasa (). Kwa kutumia uwezo wangu, ambao amenipa mwenyezi Mungu wa kusoma saikolojia ya mtu, yafuatayo yanaweza kuwa ndio sababu ya Mh. Mbowe kuloose confidence kabisa kuelekea uchaguzi mkuu, yaani hajui kinachoenda kutokea. TL alipokuwa Arusha kusaka wadhamini, wananchi walimtaka Mbowe aongee, Mbowe akaja na hakusema chapuo lolote kwa TL, badala yake alitaja kauli mbiu tu (). Kwa jambo hili kwangu linaweza kubeba hoja zifuatazo:

  • Mbowe alikuwa anajua kabisa kuwa watu walikuwa wanamtaka Tundulisu ili aweze kupeperusha bendera ya uraisi Chadema kwa sababu ya lile tukio la mashambulizi dhidi yake ili kulenga kura za huruma ya wananchi, ila bado najiuliza kwa nini aliamua naye kutangaza nia, baadae akaacha?
  • Au Mbowe aliogopa aibu ya kushindwa na Lisu, maana asilimia kubwa ya wajumbe walikuwa wanataka Lisu apeperushe bendera?
  • Kuna uwezekano Mh. Mbowe alikuwa anajua kabisa, Tundulisu hana uwezo wa kupambana na Magufuli, ila kura atakazopata zitakuwa za huruma ya wananchi, ila kwakuwa mkutano mkuu ulikuwa unamtaka TL, basi hakuwa na namna yoyote zaida ya kuunga mkono
Namalizia nakusema, Mh. Mbowe hana confidence kabisa kwenye uchaguzi huu, japokuwa wengine wanaonekana wanayo, ila ni tofauti sana na huyu ndugu, anajua kabisa Lisu hawezi kuifikia level ya Lowasa, hata nusu yake hawezi, ila ataleta upinzani angalau kidogo tu.

Asante,
Nawasilisha
Kejuu
Unataka kusema nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom