Kama maandamano yatafanyika bila kuzuiliwa nitampongeza sana mama.
Haya maandamano CCM huwa wanayapaisha wenyewe.
Hivi kwa mfano wapinzani wakitaka kufanya maandamano yao ya amani, na serikali ikasema itawapa askari wa kuwaongoza barabarani mwanzo mpaka mwisho, wapinzani wakafanya maandamano yao wakamaliza, kutatokea nini cha ajabu cha kuitishia CCM hivyo?
Kipi ambacho wapinzani watasema kwenye maandamano haya ambacho hawajasema au hawawezi kusema kwenye mitandao na mikutano yao?
Naona kama jitihada za kuyazuia ndiyo zinayapa press zaidi na kuyapaisha kiumuhimu haya maandamano.
Enzi za Kikwete, kuna siku Maxence Mello alishikwa na Polisi, kumbe Polisi walikuwa hata hawajatumwa, walikuwa wanajipendekeza tu.
Tukajioanga kinataifa kumulika udhalimu ule. Tukawaarifu "Committee for Protection of Journalism" New York City. Wakalishikia bango suala hilo kimataifa.
Kikwete akaambiwa kuna vijana wameshikwa na Polisi, Tanzania imeanza kuandikwa kwamba inaminya uhuru wa habari kwenye vyombo vya habari kimataifa.
Kikwete akasema waachieni mara moja, mimi hao vijana hawanisumbui na wala sijaagiza wakamatwe, hizi habari kwamba mmewakamata na Tanzania inaminya uhuru wa habari ndiyo zinanisumbua, msiipake matooe nchi yangu.
Max akaachiwa.
Yani, kwa Kikwete, ile zimazima ya Polisi ilikiwa imetengeneza tatizo kubwa kuliko kuachia mambo yaende tu.