Pre GE2025 Mbowe: Makubaliano na Jeshi la Polisi yamefikiwa kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa

Pre GE2025 Mbowe: Makubaliano na Jeshi la Polisi yamefikiwa kuwa maandamano yataendelea kama yalivyopangwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mimi nina tatizo la miguu, naweza kuandamana nikiwa kwenye gari langu/kiti mwendo ama lazima nitembee!!??
Kuandamana maandamano ya amani, sio lazima kuandamana kwa kutembea kwa miguu tuu, unaweza kuandamana ukiwa ndani ya gari yako.
Wanaanza watembea kwa miguu, wanafuata wenye maguta, mikokoteni, then baiskeli, wanafuata boda boda, bajaji mpaka wenye magari, kama Mei Mosi!.
P
 
Polisi wawe na akili na wao kama mtu anatqka kufanya fujo kwanini ataarifu polisi? Achaneni na mlamba viatu chalamlamba ana njaaa yule.
 
Chochote cha kihalifu endapo kitajitokeza nashauri " Iwe ni mwisho wa maandamano, na katiba iende kuondolewa kifungu kinachoruhusu maandamano" just simply....!
Maanake ni kwamba polisi wameshindwa kazi yao, warejeshwe majumbani kwao.
 
Kuandamana maandamano ya amani, sio lazima kuandamana kwa kutembea kwa miguu tuu, unaweza kuandamana ukiwa ndani ya gari yako.
Wanaanza watembea kwa miguu, wanafuata wenye maguta, mikokoteni, then baiskeli, wanafuata boda boda, bajaji mpaka wenye magari, kama Mei Mosi!.
P
Hakuna kitu inaitwa maandamano ya magari, kama ilivyo hakuna mzururaji anayetumia gari.

Magari yakiwa mengi ni msururu, Si maandamano, na katika historia ya nchi yetu, hajawahi mtu yeyote kushtakiwa Kwa case ya uzururaji wa kutumia gari😀
 
Nipo serious kweli,nina changamoto ya miguu kwa sasa,siwezi kusimama au kutembea kwa dakika kumi.

Nitakuwepo kwenye maandamano kesho nikiwa ama kwenye gari au kitimwendo.
tatizo la watanzania ni hili, people are not serious. Ona wewe sasa unaleta utani kweye mambo serious. Kwni huko uliko sukar ni bei gani? petrol? residentura mbona unaniangusha?
 
Hatuhitaji hisani Paskali. Naona mnalazimisha watu waone wema kwenye haki zao. Tunahitaji haki, na sio hizo hisani zenye kubeba malengo ya siasa za ulaghai.
Mkuu Tindo , kwanza naungana na wewe, haki ni kitu stahiki na sio hisani, ndio maana haki haiombwi na hauletewi kwenye kisahani cha chai!, haki hudaiwa na ikibidi hupiganiwa, na gharama zake sometimes hugharimiwa kwa machozi, jasho na damu!. - Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki

Unapoamua kutumia njia ya mkato kwa kualikwa karamuni, na ukaukubali mwaliko, ukakaa mezani karamuni meza Kuu, mkajilia vinono na kukubaliana kugawana nusu mkate, lazima uwe ni mtu wa shukrani!, baada ya kukubali kula fadhila, mtu yule yule hawezi kugeuka na kupeleka watu barabarani kupigania haki.

The right thing to do baada ya maridhiano kuvunjika, ni Mbowe kukaa pembeni, akawapisha wengine, Lissu au Heche ndio waongoze mapambano ya kudai haki.
Mtu ukiwa ni mlafi, unapenda kufakamia mkate, hakuna mkate mgumu mbele chai, lazima utalainika tuu!. Huo mkate wenu baada ya kulainishwa na ule mdomo laini, lipstick Nyekundu, na yale macho legevu, utadhani mtu kala kungu!, hata ningekuwa mimi, kiukweli kabisa lazima ningelainika!.

Mkate mgumu ukiisha lainika, hauwezi kuwa mgumu tena, huo ni laini kama mlenda!.
P
 
Back
Top Bottom