Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Mbowe: Mama! Mama! Mama! Kwenye hili HAPANA

Huyo mama si alikuwa mmoja wa timu magufuli kama aliona maovu kwanini hakusema hadharani? Kitumbua chake alikiona muhimu sana kuliko haki za Watanzania kudhulumiwa?
Unakuwaje shukrani na dikteta anayetaka eti atengeneze uchumi kwanza kisha ndiyo katiba mpya. Uchumi atautengeneza kwa miaka miaka mingapi? 10, 20 au 30!?
Akufukuzaye hakwambii toka! Au hamjui?
 
Uchumi utamalizika kurekebishwa lini?.
giphy.gif
 
Kwani hujui kwamba tulikuwa na DIKTETA? Kwanini Kikwete alikubali wahamishiwe Bara kwa tuhuma za Visiwani? Jaribu kutumia akili japo kiduchu. Unadhani huyo Samia alikuwa hajui kuhusu dhuluma na udhalimu uliokuwa unafanywa na dhalimu magufuli!? Si ALIUFYATA ili kitumbua chake kisiingie mchanga? Kama ni political will kwanini hakumpinga hadharani? Kwanini hakujiuzulu!?
Hakuna ukweli wowote wakati huyo mama alikuwa amekumbatia maovu yote ya dhalimu kwa miaka mitano leo anataka kujifanya eti ana usafi!!!!
Ningemuheshimu sana kama angepinga maovu hadharani au kujiuzulu vinginevyo ni mnafiki tu ambaye anataka kujisafisha na kujiweka mbali na dhalimu mwendazake wakati kwa miaka mitano hayo maovu anayoyaona leo hii HAKUYAONA.
Wewe usimuheshimu kwanza sio lazima.

Nyinyi watu sijui akili zenu zikoje. Nilionya humu kwamba mama ameamua kuwa na staha na busara, kuweni na staha na busara.

Mkijifanya mandezi mtaletewa undezi.
 
Mama amekwishasema yeye yoyoooo people power na ulevi wa Konyagi na mwenyekiti milele wasubiri.Big up mama na mkimtest hapigi na mikanda kama Baba atawafinya na kuwamwagia radhi mpate laana.
Itafika wakati mama atasema fvck these guys, kumbe ndio wako hizi....to hell with them, i will do it my fvcking way....
 
..Mama ameteleza.

..Eti anarekebisha uchumi!

..Na kutengeneza ajira!!

..hizo ni kazi ENDELEVU, hufanyi miezi miwili mitatu halafu ukapumzika.
Ndugu,

Kwani movement hizi zinazotaka kuanzishwa ni kwa ajili ya nini haswa?? Kwa mfano hii movement wanayoifanya chadema na watu wao wa Twitter ni kwa ajili ya nini???
Tujadiliane
 
Unaongea Kama mtoto vile....

Kwa hiyo Samia aliyekuwa ni makamu Rais ajiuzulu na kuacha ndoto zake za KISIASA simply kwa sababu ya kutoridhishwa na uwepo wa ndani wa hao UAMSHO ?!! Khaaa....

Political will ninayosemea mimi ni ile "mikono yake mikubwa" KIKATIBA(presidential decree) iliyowatoa WOTE HAO......

Hata JK alikuwa na "MIKONO HIYO"...
Hata JPM alikuwa na "MIKONO HIYO".....

Kwani mh.Samia amewaogopa UAMSHO kufikia wakati wake kutolewa RUMANDE?!!!

Unajizungusha kwa kukataa kukubali tu kuwa mh.SAMIA "ameplay role" kubwa leo UAMSHO kujipiga BIRIANI nyumbani....na Mdude kwenda zake kula maparachichi.....

Halafu hebu ukue basi....uko Marekani eee?!!!

Unaongelea kujiuzulu Afrika kana kwamba ni kupinga "kamasi tu".....
These people are not being realistic
 
CDM acheni utoto, huu ni utoto....jaribu kuishi kwa busara hii nchi sio ya kwenu kila mkilia msikilizwe mbona kwa yule jamaa wengine walikimbia mpaka nchi mlikuwa hamdeki hivi...

CDM acheni kudeka, hizi kelele mbona hamkupigia yule jamaa?.....nyie wenyewe ndio mlikuwa mnapiga kelele mara hivi mara vile nakutuaminisha mambo yamevurugika kila mahala....leo mama anajaribu kuweka mambo sawa mnakuja na kila aina ya hitaji...kila jambo na wakati wake tumpe muda mama walau hata 3yrs.....

Tusipende saaana kupelekeshwa na kelele za wanasiasa wanaoangalia maslahi binafsi kuliko kuangalia uelekeo na ustawi wa Taifa...Mama ana miezi mitatu madarakani nyie mnataka afanye kila kitu mnachotaka nyie utafikiri nyie ndio washauri wa siasa, uchumi nk wa hii nchi..CDM acheni utoto kama ni siasa haziko hivyo hata kidogo..

Kuna wakati kumbe undava na mabavu yanahitajika sana kwa wajinga wajinga ili mambo mengine yaende katika nchi...CDM wenyewe mlituambia mwendazake alikuwa crisis na kuacha makovu mengi, sasa hayo makovu tunazibaje? kwa kuruhusu mikutano ya siasa, kwa kuanza mchakato wa katiba mpya.? tuache kudeka aisee hatujui wala kujulikana tunataka nini...
 
Sasa Kaka, Kwanini hawakuachiwa kipindi Cha Magufuli au kipindi Cha JK na wanasheria walikuwepo? Hili suala mama samia anapaswa kupongezwa. Bado hamuoni Kama kafanya jambo jema. Ni Kama vile hamna shukrani kwake
Demi,

Niliwahi kusema hapa tena siku si nyingi kwamba hawa watu hawana shukran.

Wajinye, wewe uende kuwachambisha basi pia hawatokushkuru.

Na wajiangalie sana.
 
Kimoyo moyo una kubali kuwa bila yeye matakwa yenu mengi yasingefanikiwa.
Uamsho
Mdude
Kina mbowe kurudishiwa fedha zao
Kesi ya kina Tito magoti na mengine mengi. Si mlikuwa mnapigania siku nyingi na amelegeza kamba. Kwanini unabisha tu ili mradi ubishe? Chadema bwana...
Na bado Kuna mambo mengi tu kutwa mnamuomba mama alegeze, analegeza na bado mnamponda
Hawa watu wana agenda yao ya siri. Sio maendeleo tu ya Tanzania.

Hatuelewi sijui wafanyiwe nini hawa
 
Acha UNAFIKI wewe!!! Mama ana staha ipi? Hukumsikia kutumia neno KUDEMKA ni staha hiyo? Wewe UONYE humu kama nani!? 😳😳😳
ACHA KUJIKWEZA zuzu wewe!!! kawatishe wengine siyo mimi.
Wewe usimuheshimu kwanza sio lazima.

Nyinyi watu sijui akili zenu zikoje. Nilionya humu kwamba mama ameamua kuwa na staha na busara, kuweni na staha na busara.

Mkijifanya mandezi mtaletewa undezi.
 
yaani uchaguzi umeisha 2020, wewe leo unataka ufanye mikutano ya siasa ya hadhara kila siku mitaani mpaka 2025....nini maana ya kuwepo kampeni kwenye uchaguzi?..

Hakuna jambo baya kama kuiweka nchi kwenye tension kila siku na watu kuacha kazi za msingi za kukuza uchumi matokeo yake kuwa busy kudeal na mikutano siasa...

Kama issue ni mikutano na ujenzi wa vyama, mikutano ya ndani na majimboni inatosha na sio active politics za mitaani na mabarabarani kila kukicha na kuleta ugumu kwenye shughuli nyingine za maendeleo na uchumi..
 
Mdude Nyagali ametoka RUMANDE kwa huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan......

Masheikh wa UAMSHO wanakula biriani mtaani kwa sababu ya huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan......

Mbowe amefutiwa kesi yake na kurudishiwa milioni zake 300 kwa sababu ya huruma ya mh.Rais Samia Suluhu Hassan......

Kwani MDUDE NA WENZAKE wangeendelea kukaa RUMANDE kingebadilika KIPI huku mitaani ?!!!!!!


#ChademaWameanzaKubeep
Mimi mwana CCM, lakini ni ujinga kuwa na mitazamo kama hiyo. Hatuhitaji haki kupatikana kwa HURUMA.
 
Back
Top Bottom