Msingi wa hoja hii unajengwa na Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Toleo la mwaka 2005 kama ilivyonukuliwa hapa chini:-
8. (1). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:-
(a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi Kwa mujibu wa katiba hii;
(b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) Wananchi watashiriki katika shughuli za serikali yao Kwa mujibu wa masharti ya katiba hii
======================================
Kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya katiba hii, kumbe kila kiongozi mwenye madaraka na mamlaka ya kiserikali akiwemo aitwaye "Rais" amepewa au tumempa sisi wananchi.......
Kama ni hivyo, kumbe pia wakati wowote (si lazima kusubiri uchaguzi) tukiona hawezi au ameshindwa au anayatumia vibaya madaraka na mamlaka hayo, SISI TENA WANANCHI tunaweza kumtoa kwa njia halali kwa mujibu wa katiba hii hii katika muktadha wa Ibara hiyo hiyo ya 8 [1] (a) - (c) kwa kutumia njia halali 3 zifuatazo:
1. Shinikizo la umma (public pressure):
Ni njia halali na ya kidemokrasia kabisa. Hufanyika kwa utaratibu wa kupaza sauti kuonesha na kulisema tatizo. Sauti ikishindwa kusikika na kueleweka kwa muhusika, njia hii huenda hatua inayofuata ya juu zaidi yaani maandamano ya amani (mass mobilization) yakiwa yamebeba ajenda hiyo hiyo tu, BI. SAMIA SULUHU HASSAN, ONDOKA UMESHINDWA KAZI....!
Hii njia ni very effective isiyo na urasimu na yenye kuleta matokeo ya haraka na ya papo kwa papo. Viongozi walengwa wanaiogopa sana njia hii inapotumiwa na wananchi. Na kwa sababu hii, njia hii mara zote huwa ni ngumu yenye risks nyingi kwa sababu huhusisha mapambano na vyombo vya dola kama polisi na hata Majeshi ya ulinzi ambayo huwa chini ya udhibiti na amri za kiongozi (Rais) anayekataliwa na anayetakiwa kuondoka madarakani lakini hujaribu kuwa loyal kwake na kumlinda unless navyo viwe na wananchi. Huanza kwa vyombo hivi ku - resist kidogo. Lakini people's power - nguvu ya umma inapokuwa kubwa, hivi vyombo hunyoosha mikono juu na kuungana na wananchi. Ikitokea hivi, UMMA UNAKUWA UMESHINDWA...!
2. Kwa njia ya mashitaka ya ki - Bunge . Yaani Bunge kumshitaki Rais na kisha kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye maarufu kwa kiingereza kama "impeachment"
Nayo ni njia halali ya kisheria na kidemokrasia pia. Lakini hii njia ni ngumu sana na pengine isiyowezekana kabisa ingalau katika mazingira ya sasa kwa sababu nature ya Bunge letu la sasa ambalo typically ni la chama kimoja atokako Rais huyu aliyeshindwa. Aidha, ni kwa sababu pia ya masharti magumu ya kikatiba katika Katiba ya JMT Ibara ya 46A (1) - (11) sambamba na Ibara ya 90 (1) - (2) juu ya nguvu Rais aliyonayo kulivunja Bunge wakati wowote kwa sababu anayoweza hata kuitengeneza tu......
3. Kwa njia ya uchaguzi wa HAKI, HURU na wa WAZI.
Hii ndiyo njia kuu ya kidemokrasia iwapo mambo yako kawaida. Chaguzi mara nyingi zina vipindi vya muda maalumu. Hapa kwetu Tanganyika ni kila baada ya miaka mitano....
Kwa mazingira ya Rais aliyeshindwa kutekeleza wajibu wake, wananchi na nchi haiwezi kusubiri miaka mitano ifike ndiyo tuondoe tatizo......
##Ndo kusema kuwa movement ya CHADEMA ya "SAMIA MUST GO" si uhaini, si kuvunja katiba wala sheria yoyote ile ya Tanzania. Hili ni shinikizo la umma kwa mtu ambaye yuko chini ya mamlaka yao ya kisiasa kwa kuwa hawezi au kashindwa kutekeleza wajibu wake kwa makusudi au kwa kuwa tu uwezo wake kiuongozi ni mdogo.....
##Polisi wao ndiyo wanavunja sheria na Katiba kwa kuanza kutisha watu ili wasi - exercise haki yao kuwajijibisha kiongozi wao (Rais) ambaye ame - prove total failure ktk kulinda uhai wa wananchi/watulioshindwa kwa mujibu wa Ibara ya 8 [1] (b) inayosema "Lengo kuu la serikali itakuwa ni ustawi wa wananchi"
Mpaka hatua hii, serikali hii chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inafisha wananchi wake kinyume cha katiba badala ya kuwastawisha.....
Hakuna shaka kuwa, baadhi ya viongozi ndani ya serikali ya Rais Samia, wameunda vikundi vya uhalifu dhidi ya binadamu na kwa kuwa ameshindwa kuchukua hatua stahiki, basi tafsiri yake ni kuwa mauaji haya yana baraka zake. Kama ndivyo, Rais huyu hafai kuendelea kubaki hata kwa siku mbili zijazo....!!
##Katika hali hii, wananchi (umma) ni lazima tuyatumie mamlaka yetu kwa ukamilifu kwa kumwambia waziwazi mchana kweupe kuwa "SAMIA STEP DOWN, GO HOME...!"