Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Maandamano ya WANANCHI yanayoratibiwa na chama kikuu cha upinzani Chadema chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.

Yameendelea kuungwa mkono
na wananchi mbalimbali huku
Mwanaharakati tishio Tanzania na Diaspora Mange kimambi akiyaunga mkono.

Kupitia mtandao wa Instagram mange ameweka clip huku akinukuliwa "guys nimeamua nijitokeze kwa njia ya clip maana kuandika inaniwia ngumu.... ni hivi maandamano ya wananchi yaliyotangazwa na chadema waingie barabarani niko tayari kuyaunga mkono na kuhamasisha watanzania wenzangu waliochoshwa na serikali hii ya kipumbavu...."
mange ameendelea kuishutumu serikali Kwa utekaji na utesaji unaondelea nchini baada ya kutekwa na kuuawa kwa Bwana Ali Mohamed Kibao kada wa chadema.

Duru za kisiasa zinasema kujitosa kwa mange kimambi kwenye Maandamano hayo kutatikisa nchi.
hivyo serikali inapaswa ifanyie kazi yale mambo ambayo Mwenyekiti wa chadema taifa Freeman Mbowe aliyo yataja kwenye mkutano wake na wanachadema jijini Dar es salam huku akiipa serikali siku kumi itoe majibu.
Huyo Mange ambaye hata kalio la kutingisha tu hana sasa atawezaje kutingisha nchi?
 
Hii ni bongo baba tunajuana,, hizo nchi nyingine hawapo kama huku,, ,huku wengi ji ma keyboard warriors tu,,,,labda hayo maandamano waruhusu wenyewe serikali ila sio ya kufosi
Nakuunga mkono Mkuu. Mm ningekuwa mmoja wa viongozi wa CDM nisingeitisha maandamano ambayo, kwa vyovyote, hayatafanikiwa. Watanzania hawajawa tayari kwa kudai haki zao kwa njia ya shinikizo. Kitakachotokea ni watu wachache kutokea barabarani, watachimbwa mkwala na Polisi, wengine watapigwa km wanayama na kukamatwa na wengi wao watakimbia na ndio itakuwa mwisho wa mchezo.
Hata maandamano waliyofanya CDM hapo awali yaliyoruhusiwa nayo hayakuwa na maana yoyote. Maandamano yaliyoruhusiwa hayana impact yoyote, ni km jogging tu. Kwa ujumla kwa wakati huu siyo njia sahihi. Akili za watanzania bd kdg japo juzi wamasai walituonyesha mfano mzuri sana. Ipo siku kila mtu au ndugu au Jamaa zake watatendewa km wanavyotendewa watu fulani wakati huu, hapo ndipo watakapogundua kuwa Umoja na uasi dhidi ya uovu ndio njia pekee ya kujikomboa. Hapo hawatahitaji chama Wala taasisi. Kila mtu nafsi yake itakataa Maovu na kujitolea kutoa ht uhai wake kupinga uovu kwani ataona ht akiulinda uhai wake kwa woga, bado kuna tishio halisi dhidi yake kutoka kwa watawala. Hayo maandamano yataleta mabadiliko makubwa na madai ya haki yatapata majibu. Mfumo uliopo sasa wa watu wachache kuamua juu ya uhai Wa wengine utaanguka.
 
Mimi nitashiriki maandamano hapa mtandaoni, na nitaungana na wazalendo hapa hapa mtandaoni katika kuandamana kwa amani, naandamana kama aka MANGE, warrior wa maandamano ya mitandaoni.
 
Endelea kujidanganya ufe maskini mkeo agongwe

Tafuta maisha dogo
Hivi hata kina Nyerere, Kenyatta na wale waliopingana na madikteta wabaya Duniani na kushinda wangefikiria wake zao kugongwa na kutafuta Maisha hali ingekuwa leo kwa maeneo waliyotoa uhai wao kuyapigania? Hivi wale Gen Z Wa Kenya wasingefanya yale waliyofanya kupinga bajeti waliyoiona itawaumiza kwa kuogopa girlfriend zao kugongwa na wengine na kuamua kukaa majumbani kutafuta Maisha kama unavyotaka hali ingekuwaje leo kwao? Kama huoni umuhimu wa Jambo fulani basi waachie wenzio wanaoona umuhimu wake. Bila Shaka ww ni mnufaika wa mfumo uliopo, lazima useme hivyo. Upo upande Salama, ambao kina Msigwa waliuchagua juzi. Ni upande ambao ukiwa huko, Kula yako ni guaranteed. Usalama dhidi ya watekaji ni 100%. Hakuna kukamatwa au kuitwa na Polisi, hakuna kupotezwa. Ht ukiropoka Siri za mauaji au wizi Wa Kura kwa wasiowaunga mkono hakuna shida. Kwa ujumla, ukiwa huko, sheria ipo chini ya miguu yako. Lkn ujue siyo wote watakuwa huko. Hongera sana kwa raha unazopata. Kumbuka upande mwingine unaowatishia kugongewa wake zao kuna vilio. Wanapigwa risasi mchana kweupe km Swala.
 
Mimi Naunga mkono maandamano ya amani kwani ni haki ya kila Mtanzania. Lakini tuseme Ukweli, Mange Kimambi ana impact yoyote ile kwa Watanzania kwa kusema anayaunga mkono? Eti nchi inaweza ikasimama siku hiyo sababu ya Mange kahamasisha watu waandamane. Ni watu wachache saana wanaomfahamu Mange hasa hao wa Facebook na Instagram. Na hata hivyo hawamchukulii serious.
 
Naona kuna hashtag ya SAMIA MUST GO sasa inakuwaje kuhusu hii tassisi inayoshikilia katiba ya chama kushika hatamu au haya matukio yatakoma ikiwa SAMIA ataondoka madarakani?

Naomba mbadilishe hiyo slogan hata kabla kufika tarehe 20 la sivyo itafeli pakubwa.
 
Sawa kiongozi umeeleweka vema kabisa na Kila mtanzania mpenda amani bila kujari tofauti zetu za kivyama naamini watanzania watajiktokeza kwa wingi ili kuwaonesha watawala kuwa hatuliziki na namna wanavyo tawala
 
CHADEMA endesheni siasa safi...tumechoka kila siku nyinyi na Serikali. Why CHADEMA not other Political Parties? Mkiona vip fumueni uongozi wenu wote wa juu wekeni viongozi mahiri...lakin mkiendelea hvo mtakuja kukumbuka haya maneno ya leo.mimi sio Mwanasiasa nachangia maoni yangu tu nakama hamjanielewa katafuteni movies ya zamani inaitwa "DEAD PRAY"Mtajifunza kitu.
 
Sera zimeisha wananchi wanataka maendeleo sio maandamano.Samia anatosha.
 
Mbowe pia ametoa rai kwa viongozi wa CHADEMA siku 12 kuanzia sasa kuja Dar kwaajili ya kupeana mikakati muhimu kwa hatua zaidi.
=====
"Lingine, kuanzia siku ya Jumatatu, tar 23/9/2024 mkumbuke nilitangaza tar 21 tunategemea tuone hatua za watu kuwajibika zimeanza. Kama hawatachukuliana hatua wenyewe kwa wenyewe, sisi kuanzia tarehe 23 jiji lote la Dar es Salaam, kila kata kila mtaa.. ndugu zangu tumekuwa tunafanya utani mara nyingi, lakini kwa wakati huu hatuna utani.

"Kuanzia jumatatu sisi tutaingia barabarani kudai tunachoona ni uhai wa watu wetu waliopotenzwa unless serikali imechukua hatua za haraka na za makusudi kuwarejesha, watu kujiuzulu na watu wote kuwajibika kwa mujibu wa tamko letu la leo." - [/I]Amesema Mbowe katika mkutano kwenye ofisi za CHADEMA, Mikocheni leo 11/9/2024
Baada ya tangazo hili Kuelekea 2025 - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu then tunaishauri Chadema wasitishe maandamano.
P
 
Utaandamana na Nani vijana wapo busy na Aviator

Hao wacheza aviator ndio wazuri maana wameshakata tamaa za kutafuta pesa kwa jasho, wakipewa smartgin na elf kumi ya kula sidhani kama watakataa kuandamana
 
Msingi wa hoja hii unajengwa na Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Toleo la mwaka 2005 kama ilivyonukuliwa hapa chini:-

8. (1). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:-
(a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi Kwa mujibu wa katiba hii;
(b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) Wananchi watashiriki katika shughuli za serikali yao Kwa mujibu wa masharti ya katiba hii


======================================
Kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya katiba hii, kumbe kila kiongozi mwenye madaraka na mamlaka ya kiserikali akiwemo aitwaye "Rais" amepewa au tumempa sisi wananchi.......

Kama ni hivyo, kumbe pia wakati wowote (si lazima kusubiri uchaguzi) tukiona hawezi au ameshindwa au anayatumia vibaya madaraka na mamlaka hayo, SISI TENA WANANCHI tunaweza kumtoa kwa njia halali kwa mujibu wa katiba hii hii katika muktadha wa Ibara hiyo hiyo ya 8 [1] (a) - (c) kwa kutumia njia halali 3 zifuatazo:

1. Shinikizo la umma (public pressure):

Ni njia halali na ya kidemokrasia kabisa. Hufanyika kwa utaratibu wa kupaza sauti kuonesha na kulisema tatizo. Sauti ikishindwa kusikika na kueleweka kwa muhusika, njia hii huenda hatua inayofuata ya juu zaidi yaani maandamano ya amani (mass mobilization) yakiwa yamebeba ajenda hiyo hiyo tu, BI. SAMIA SULUHU HASSAN, ONDOKA UMESHINDWA KAZI....!

Hii njia ni very effective isiyo na urasimu na yenye kuleta matokeo ya haraka na ya papo kwa papo. Viongozi walengwa wanaiogopa sana njia hii inapotumiwa na wananchi. Na kwa sababu hii, njia hii mara zote huwa ni ngumu yenye risks nyingi kwa sababu huhusisha mapambano na vyombo vya dola kama polisi na hata Majeshi ya ulinzi ambayo huwa chini ya udhibiti na amri za kiongozi (Rais) anayekataliwa na anayetakiwa kuondoka madarakani lakini hujaribu kuwa loyal kwake na kumlinda unless navyo viwe na wananchi. Huanza kwa vyombo hivi ku - resist kidogo. Lakini people's power - nguvu ya umma inapokuwa kubwa, hivi vyombo hunyoosha mikono juu na kuungana na wananchi. Ikitokea hivi, UMMA UNAKUWA UMESHINDWA...!

2. Kwa njia ya mashitaka ya ki - Bunge . Yaani Bunge kumshitaki Rais na kisha kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye maarufu kwa kiingereza kama "impeachment"

Nayo ni njia halali ya kisheria na kidemokrasia pia. Lakini hii njia ni ngumu sana na pengine isiyowezekana kabisa ingalau katika mazingira ya sasa kwa sababu nature ya Bunge letu la sasa ambalo typically ni la chama kimoja atokako Rais huyu aliyeshindwa. Aidha, ni kwa sababu pia ya masharti magumu ya kikatiba katika Katiba ya JMT Ibara ya 46A (1) - (11) sambamba na Ibara ya 90 (1) - (2) juu ya nguvu Rais aliyonayo kulivunja Bunge wakati wowote kwa sababu anayoweza hata kuitengeneza tu......

3. Kwa njia ya uchaguzi wa HAKI, HURU na wa WAZI.

Hii ndiyo njia kuu ya kidemokrasia iwapo mambo yako kawaida. Chaguzi mara nyingi zina vipindi vya muda maalumu. Hapa kwetu Tanganyika ni kila baada ya miaka mitano....

Kwa mazingira ya Rais aliyeshindwa kutekeleza wajibu wake, wananchi na nchi haiwezi kusubiri miaka mitano ifike ndiyo tuondoe tatizo......

##Ndo kusema kuwa movement ya CHADEMA ya "SAMIA MUST GO" si uhaini, si kuvunja katiba wala sheria yoyote ile ya Tanzania. Hili ni shinikizo la umma kwa mtu ambaye yuko chini ya mamlaka yao ya kisiasa kwa kuwa hawezi au kashindwa kutekeleza wajibu wake kwa makusudi au kwa kuwa tu uwezo wake kiuongozi ni mdogo.....

##Polisi wao ndiyo wanavunja sheria na Katiba kwa kuanza kutisha watu ili wasi - exercise haki yao kuwajijibisha kiongozi wao (Rais) ambaye ame - prove total failure ktk kulinda uhai wa wananchi/watulioshindwa kwa mujibu wa Ibara ya 8 [1] (b) inayosema "Lengo kuu la serikali itakuwa ni ustawi wa wananchi"

Mpaka hatua hii, serikali hii chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inafisha wananchi wake kinyume cha katiba badala ya kuwastawisha.....

Hakuna shaka kuwa, baadhi ya viongozi ndani ya serikali ya Rais Samia, wameunda vikundi vya uhalifu dhidi ya binadamu na kwa kuwa ameshindwa kuchukua hatua stahiki, basi tafsiri yake ni kuwa mauaji haya yana baraka zake. Kama ndivyo, Rais huyu hafai kuendelea kubaki hata kwa siku mbili zijazo....!!

##Katika hali hii, wananchi (umma) ni lazima tuyatumie mamlaka yetu kwa ukamilifu kwa kumwambia waziwazi mchana kweupe kuwa "SAMIA STEP DOWN, GO HOME...!"
 
Back
Top Bottom