Haijulikani ni shinikizo la wafadhili wao, imani potofu za kishirikina, ramli au muujiza umewatokea...
Hata hivyo awali kulika na migawanyiko baina ya viongozi waandamizi wa Chadema kuhusu slogan ya Samia must go, kwamba kivyovyote Lazima itaambatana na fujo na isingewezekana kua ya amani.
Lakini viongozi wengine walienda mbali zaidi na kudai kwamba tangazo la maandamano lilifanyika kwa mihemko bila tahmini ya kina, na hivyo Samia Must Go Ilikua ni kwenda kinyume na misingi ya kidemokrasia ya chama hicho..
Kupitia barua yao ya usiku wa manane kwa jeshi la polisi iliyoonekana leo, inaonyesha kuna mabadiliko ya kimyakimya au ya kuzinduka usingizini yamefanyika dhidi ya dhima, dhumuni na nia ya maandamano ya kuvuruga amani ya fujo ya Samia must go.
Sasa eti yamebadilika na kua sijui maandamano ya nini vile? Huenda Chadema hawajui hata wanadai wala wanatetea nini. Na Tatizo ni dhahiri Uongozi wao..
kiufupi kwa maoni yangu hawezi kufanikiwa wala kuruhusiwa kuandamana kabisa.
Na upo uwezekano mkubwa sana wakaahirisha maandamano hayo, kwasababu moja haikai, mbili haikai miongoni mwao.🐒
Mungu Ibariki Tanzania