Mama Samia ndio kwanza anamaliza miezi 3 tangu apate urais
Ndani ya kipindi hicho tumeona mabadiliko mengi yanayohusu haki na uhuru ambayo watu wengi wapinzani na wananchi wa kawaida waliyalalamikia
Kutaja tu machache
Kuna kesi za kubambiza zaidi ya 147 zimefutwa
Vyama vya upinzani vimezunguka nchi nzima vikifanya mikutano ya ndani bila rabsha zozote kabisa
Vyombo vya habari vilianza kurudi, na hata kuandika kwa uhuru
Kuondolewa kwa watu kama Sabaya, ambaye yupo mahabusu kwa sasa na wengine kama akina Biswalo Mganga, DC Odunga. Chalamila n.k
Kuondolewa kwa utaratibu wa kukusanya kodi kwa mtutu wa bunduki
Wapinzani kushinda kesi zao ama rufaa za kesi ambazo walihukumiwa kipindi cha Magufuli
Kuachiwa kwa mashehe wa uamsho
Hata suala la katiba mpya alitoa lugha ya matumaini kidogo kuwa ni suala muhimu ila apewe muda, (tujilinganisha na Magufuli ambaye ali rule out kabisa)
Haya ni machache niliyoweza kukumbuka kwa haraka
Sasa kwa haya amewakwaza watu wengi ndani ya CCM ambao wanatja angefuata umagufuli
nilitarajia upinzani ungempa muda kidogo aendelee kurekebisha zaidi mengi,
Kwa hizi provocation walizoanza nazo Wapinzani ndani ya kipindi hiki kifupi, kutishia maandamano nchi nzima na mikutano ya kudai katiba, nadhani wale hardliners wa Magufulism watakuwa wamepata cha kumwambia, Samia kuwa, tulikuambia njia pekee ya ku deal na hawa watu ni Magufuli's way