Mbowe na genge lako, mnamtisha Amiri Jeshi Mkuu akitumia madaraka yake muanze tena kulalamika?

Mbowe na genge lako, mnamtisha Amiri Jeshi Mkuu akitumia madaraka yake muanze tena kulalamika?

Wewe punguani kweli nani alikuambia mimi ni CCM? Mimi ni raia mwema sina chama nakubaliana na Rais Samia, unataka fact gani kwa mtu anayempagia rais jinsi ya kufanya majukumu yake.
Wewe inaonekana umepungukiwa kuliko unaodhani wamepungukiwa. Hivi unataka Rais afanye kazi kwa matakwa ya nani?

Serikali inapata mamlaka yake toka kwa umma, na RAIS NI LAZIMA AFANYE KAZI YAKE KWA MATAKWA YA UMMA, siyo kwa matakwa yake. Rais analazimishwa kufanya kazi kwa matakwa ya umma. Hoja yako ingekuwa je, tamko la Mbowe ni matakwa ya umma, ya kwake pekee yake au kikundi kidogo cha watu?
 
Sisi Watanzania tumechagua muhimu 2 na 3.
Tuliulizwa lini kufahamu vipaumbele vyetu?!

SSH na timu yake wanafahamu vipi vipaumbele vya Wajomba zangu kule Mchinga, ambao pamoja na kupewa mtu maarufu kabisa, Mama Salma Kikwete awe ndie mgombea wetu wa ubunge, bado wananchi wa kule wanaamini Mama Salma hakuchaguliwa, bali alitangazwa tu?!

Wananchi ambao hata madiwani wao ni wa upinzani, huku NEC wakilazimisha Mama Salma awe ndie mbunge wao, hivi unaamini kabisa Mama Samia anafahamu vipaumbele vya wale wananchi?
Mbowe na wafuasi wako mnachekesha sana hivi mnataka rais wetu afuate mnachotaka nyie kwa maslahi yenu?

Rais akitumia madaraka yake kama katiba unavyomtaka mtaanza tena kulia kuwa Tanzania hamna demokrasia.
Unaweza kutaja vifungu vya katiba vinavyompa hayo mamlaka unayotaka kutuaminisha hapa kwamba anayo?! Unaweza kutueleza Mbowe na Wafuasi wake wamevunja sheria ipi ya nchi, au ibara ipi ya katiba katika kudai kwao katiba mpya?
 
Nakubaliana na wewe honey moon ya Samia imeisha. Na pia Mbowe anamlipa Samia ubaya kwa wema kwa kukosa uvumilivu. Lakini tusimtukane Mbowe anatimiza wajibu wake kama kiongozi wa Siasa. Katiba asiyoipenda bado inamruhusu kuongea na kudai uhuru wa mikusanyiko. Tumvumilie.
 
Mama Samia ndio kwanza anamaliza miezi 3 tangu apate urais
Ndani ya kipindi hicho tumeona mabadiliko mengi yanayohusu haki na uhuru ambayo watu wengi wapinzani na wananchi wa kawaida waliyalalamikia...
Mbona alishasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja.

Katoka kwenye UMagufuli lini?
 
Mimi kama mwananchi nahitaji maendeleo, katiba ipo tayari.
Mpaka wewe umeibuka leo!!!!
Nimeamini UVCCM huwa mnaambiwa nini cha kufanya kwenye mitandao.
Poleni kwa kushikiwa akili.
Poleni kwa kuwa misukule.
Poleni kwa kutobarikiwa akili ya kujipatia kipato kwa jasho.
Poleni.
 
Wewe ulikuwa mnufaika wa was mfumo wa Magufuli.

Msiwe washabiki kuchochea.

Mama akiendelea kufanya kazi zake bila za urais bila matamko yanayokinzana na katiba hutasikia hayo maandamano.

Utasikia kelele za mikutano tu

Kelele hizo zaweza kuwa na ujumbe au la.

Mama asijibizane nao,waachane wateme nyongo
 
Wanaukumbi,

Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyetambua umuhimu wa Katiba Mpya; tunapishana sehemu ndogo sana ‘timing’ na vipaumbele vya kitaifa kwa sasa viwe ni 1. Katiba Mpya au kupambana na 2. Janga la Corona na 3. Kuinua Uchumi na hali za wananchi masikini?...
CHADEMA hawana kitu cha kufanya sasa hivi ni kula kulala
 
Katiba ina maslahi gani kwenye familia yako?
mmemezeshwa mambo ya ajabu tu.
Kenya wana katiba mpya ila njaa na magonjwa yapo palepale
We Mataga mbona mnaogopa Katiba mpya kwani Ina sumu au bunduki?
 
Wanaukumbi,

Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyetambua umuhimu wa Katiba Mpya; tunapishana sehemu ndogo sana ‘timing’ na vipaumbele vya kitaifa kwa sasa viwe ni 1. Katiba Mpya au kupambana na 2. Janga la Corona na 3. Kuinua Uchumi na hali za wananchi masikini?..
Mbowe hajawahi kuwa na akili timamu....ni mtu wa mihemko sana. Yote hii ni kwa sababu ya hasira za wale wabunge wanaowakilisha chama chao bila ridhaa yake maana hawezi tena kuwacontrol kuomba uroda.
 
Rais Samia amekuwa tofauti na mtangulizi wake na kuna mabadiliko ameyafanya ndani siku 100 ikiwemo kumuondoa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, Ole Sabaya aliyekuwa akilalamikiwa. Kumuondoa DPP, kuachia wafungwa ie. Masheikh Uamsho, tumeanza kuona mwanga wa Haki na Sheria.
Mbowe na wafuasi wake wanataka kumpangia jinsi ya kuongoza nchi tena kwa vitisho.
Ulivyokuwa mpumbavu,maandishi yako haya yamedhihirisha umuhimu wa katiba mpya. Haiwezekani mtu mmoja aamue hatima ya watu milioni 60+ kwa jinsi aamkavyo. Mkiitwa wapumbavu,hamtukanwi,mnapewa sifa stahili.

Tunataka katiba mpya itakayoweka madaraka ya kila Mtanzania wazi na mipaka yake.
 
Magufuli sifa za kijinga zilizidi akajiona ni kama kimungu kidogo. Ilifikia ya kuwakemea hata viongozi wa dini tena kwa dharau kubwa sana. Yule alikuwa dikteta kwelikweli. SAMIA HATAFANYA UTOPOLO.
 
Mimi ushauri wangu wasivunje sheria tu, ila vingine vyote wafanye hata kama havina tija kwako au kwangu (ndio raha ya uhuru), Ilimradi wanayoyafanya yasiwe kero kwa wengine.
 
Ma

Matapeli ndo yanataka katiba mpya kwa nguvu,
Wananchi wanataka maisha yao yawe vizuri tu, hayo mambo y katiba hayawahusu.
Kwani nao wanataka vyeo?
Katiba inahusu vyeo?

Mwendakuzimu aliponipora hela zangu za duka la kubadilishia fedha za kigeni,alifanya hayo akilindwa na katiba.

Mwendakuzimu alipoingilia zao letu la korosho,akijua analindwa na katiba mbovu, alisababisha wafanyabiashara wapatao laki tatu kupoteza mitaji yao na serikali kukosa kodi,tozo na ushuru wa takribani 76 bilioni.
 
Unajua Lumumba mna matope kichwan

Shuguli za kisiasa nihaki ya watanzania

Badala ya kumshauri Mama yenu, mafuta yamepanda bei , wapigaji wameanza kuamka.

Nyinyi mnapambana na upinzan.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wananchi wanauliza Mbowe ni Mfalme Chadema? Kila siku kiongozi ni yeye atakayejaribu kugombea anafukuzwa chama alikuwepo wakati wa Mkapa, Kikwete, Magufuli, Samia, halafu anataka katiba daaah
Katiba ya chama ndiyo inamruhusu hiyo angekaa bila utaratibu wa chama ndiyo ingekuwa kosa, mbona hamsemi kuhusu uenyekiti wa Prof. Lipumba, Mrema, Cheyo au Mbatia? Tuwe na katiba yenye kujenga misingi ya utawala bora.

Magufuli alidai ananyosha nchi lakini uchumi umeanguka ktk kipindi chake toka asilimia 7 hadi 4, . Rais Samia anataka kukuza uchumi, je nani anajua Corona itaisha lini? Je akishidwa kupandisha uchumi? Mchakato uanze uende awamu kwa awamu tupate katiba nzuri
 
Naamini Mbowe was simply trying to remain relevant!

Otherwise ni ujinga wa daraja la kwanza, kumtishia Rais kiasi kile!

Mtakosa vyote, katiba hamupati na umaarufu utapotezwa trust me!

Hivi issue ni katiba mpya tu hata ikiwa mbovu?

Gurantees ni zipi kwamba kukianzishwa mchakato wa Katiba mpya itapatikana mnayoitaka nyinyi CHADEMA?

Msimchukulie mtu poa, hamkujifunza kwa KIKWETE!
 
Wana JF,

Mbowe sasa anaonekana wazi kuihujumu chadema kwa kuwa amekosa mvuto kwa umma kama mwanzo anawezaje kulazimisha kitu ambacho rais amesema apewe muda kweli kusubiri kidogo mambo yakae sawa unashindwa mpaka unalazimisha kila kitu kifanike kama unavyotaka.

Huo ni dharau kubwa kwa rais na anachokitafuta siyo kujenga bali kuibomoa chadema na akiondoka aje aseme mnaona nimeondoka chadema imekufa? inamaana atajiona kuwa bila yeye hakuna Chadema.

Atumie busara kumpa muda rais ili muda muafaka ukifika katiba itatengenezwa tena yeye mwenyewe anajuwa kabisa lazima liwepo bunge lingine la kutengeneza hiyo katiba ambalo tena litatumia mabilioni ya pesa

Busara itumike
 
Back
Top Bottom