Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Mbowe anadhani kuwapigisha ukunga wananchi mikutanoni kunaweza kuifanya CCM ilete katiba mpya.
Kitu pekee cha kuifanya CCM ilete katiba mpya ni mass action, na CHADEMA inayo nguvu za kusiaidia hilo. Ila viongozi wake akina Mbowe wao wanawaza ruzuku, nyomi, ubunge 2025, uenyekiti endelevu na wasirudishwe jela tena baasi.

Hizi siasa zetu zisipobadilika na kuwa za ngangari ngunguri hatutoboi. Unfortunately, Mbowe hayuko tayari kuraise up the stake na kuitia kibano kikali CCM na serikali yake!. Labda anaogopa kesi yake isije ikafufuliwa tena!
 
Dhambi mbaya anayoifanya Mbowe ni kuonyesha kumtenga Lissu waziwazi.
 
Uko sahihi sana.
Kila siku naimba kuwa Mbowe sasa ni kikwazo
 
Mbowe ningemdharau sana kama angeshiriki haya maandamano ya akina Slaa na Mdude, mtu yoyote mwenye akili aliyeona ile press conference yao ya kuipa serikali siku 30 angesema hawa watu ni vichaa
Shida mmeaminishwa na Mbowe kuwa mabadiliko ni kubembelezana na watawala kwa mnachoita maridhiano.Ukisilikiliza kauli ngumu kama za akina mdude lazima upagawe coz sio ulichoaminishwa na Mbowe. Tuseme kweli,siasa za Mbowe ndio CCM wanazitaka, ni siasa zisizowanyima usingizi na ndio maana wamewaacha wazunguke nchi nzima. SIASA za akina mdude ni mwiba kwa CCM ndio maana wanapambana kuzizima na ndio siasa zinazotakiwa nchi hii.Ukiona unapiga siasa na watawala wako kimya jua unapoteza muda tu.Piga siasa hadi kesho usikie watawala wametuma jeshi lao kuzima na hapo ndio utajua kweli sindano zimewaingia
 
Dhambi mbaya anayoifanya Mbowe ni kuonyesha kumtenga Lissu waziwazi.
Amekuwa na soft speech sana mwenyekiti sijui kipi kimemkuta? CCM wanahitaji nginjangija kama ya TL tofauti na hapo ni kupoteza muda tu.
 
Shida ya Chadema na wafuasi wake ni ujuaji mwingi. Hamuwez itoa CCM madarakani kwa siasa za Mbowe na genge lake. Kama mnalengo la kupiga porojo sawa ila kama ni kuitoa CCM madarakani kwa siasa uchwara hizi msahau. CCM inajivunia uwepo wa siasa kama za Chadema
 
Chadema kimekuwa chama MFU kwa sababu ya mbowe na siasa zake za udini na ukabila
 
zitto junior JokaKuu Tindo Nguruvi3 Uzima Tele Pascal Mayalla brazaj Kalamu The Boy Wonder ....
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.
Kama ndiyo hivyo kulikuwa na sababu gani ya kubeza wengine kwa kuwaita ni pressure group? Kwanini kama viongozi wasingefanya mawasiliano na wakashauriana?
 
Wanaharakati huru wanaruhusiwa kufanya harakati zao za upatikanaji wa katiba mpya na kuzuia kuuzwa kwa bandari.
Wasitegemee mgongongo wa chama chochote cha siasa kuanzia sisiem hadi vyama vya upinzani.
Ccm wana rasimu yao wanayoiita katiba mbadala, wananchi wana rasimu ya Warioba inayohujumiwa.
Wanaharakati waje na ya kwao.
Kutegemea kuungwa mkono na upinzani mfano wa chadema ni sawa ila wakubali hilo sii jukwaa moja kwani kwa njia hiyo ccm wanaweza kueneza propaganda kuwa hii ni katiba ya chadema.
Kila kundi lipambane kutokea angle yao na ikifika mahali fulani ndipo nguvu ziunganishwe.
Kundi moja kutaka huruma za kundi jingine ni kuhujumu au kukwamisha dhamira njema ya upatikanaji katiba mpya.
Wanaharakati huru achaneni na mbowe na chadema, lakini katika masuala ya msingi ndipo iunganishwe nguvu.
Hili la kutuhumiana limeshaipa nguvu ccm kuhujumu harakati kwa kuzingatia kigezo cha kwamba watu hawa wanegawanyika na hivyo kuwatwanga ni rahisi maana hawana lugha moja.
 
Kuna jambo wengi hawawezi kulifafanua
The guy anatuchezea akili na vile wadanganyika wameruhusu basi safari ya ukombozi ni ndoto
Mkulu anafanya teuzi nje ya nchi, anavunja Katiba left right n center anatembea kila siku kwa shughuli hazieleweki opposition wapo kimya
Inafikirisha sana
 
Kama ndiyo hivyo kulikuwa na sababu gani ya kubeza wengine kwa kuwaita ni pressure group? Kwanini kama viongozi wasingefanya mawasiliano na wakashauriana?

..Kama Mbowe alisema hivyo basi atakuwa amekosea.

..Labda alikuwa anajibu kauli ya Adv.Mwabukusi kwamba vyama vya siasa ni magenge ya ubunge na ruzuku.

..Sasa ukiacha hiyo minyukano ambayo haina maana, hali ya mahudhurio na hamasa ktk mikutano ya hadhara haionyeshi kwamba huu ni wakati sahihi wa kuitisha maandamano.

..Tujifunze toka kule walikoitisha maandamano na wakafanikiwa. Je, hali yetu ya kisiasa inalingana nao?
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.
Mnaelimisha nini ambacho wananchi hawajui?Mnatofauti gani na CCM wanaosema swala la katiba wananchi wapewe elimu kwanza?
 
Mnaelimisha nini ambacho wananchi hawajui?Mnatofauti gani na CCM wanaosema swala la katiba wananchi wapewe elimu kwanza?

..maandamano ni zao la mikutano mikubwa yenye hamasa ya hadhara.
 
..maandamano ni zao la mikutano mikubwa yenye hamasa ya hadhara.
Huko walikopita wameacha hamasa gani?Operation wanazofanya akina Mbowe ni utapeli na uhujumu kodi za wananchi. Wananchi wamechoka na ccm na hakuna asiyejua ubaya wa ccm saizi.Kinachotakiwa ni mass action tu na sio kuendelea kuleta porojo. Swala l bandari halikuhitaji porojo zaidi ya Mbowe kuitisha maandamano nchi nzima. Huko Kenya mbona hatusikii porojo za kutoa elimu wanapokua na jambo lao?Bei ya unga imepanda,Odinga ye ni kuwaingiza wafuasi wake barabarani. Hakuna porojo kama za akina Mbowe huku
 

..kama hali ya hamasa imefika hapo basi yeyote yule anaweza kuitisha maandamano hakuna haja ya kumlalamikia au kumkoromea Mbowe au Chadema.
 
..suala la maandamano halipaswi kuharakishwa.

..wacha mikutano ifanyike kuelimisha wananchi, na wakishahamasika ndio maandamano yafanyike.

Hii hoja ya wacha wananchi waelimishwe kwanza ndiyo hoja hiyo hiyo Samia anaitumia kwenye katiba mpya kuwa "wacha wananchi waelimishwe kwanza".

Sikia elimu haina mwisho!. Ila kuendelea na mfumo huu wa sasa hata kwa mwaka mmoja mbele ni mzigo!. Thats why cheche zozote za kupeleka struggle to the next level lazima zisaidiwe, zilelewe, ziungwe mkono na ziwezeshwe. Siyo kurudia the same old politics ambazo Mbowe kazifanya kwa miaka zaidi ya 20 sasa na tuko palepale!.
Insanity is doing the same thing over and over again expecting different results!
 

..kama Mbowe anaonekana hafai basi wajitokeze wengine wenye uwezo na mbinu mpya.

..kwanini nguvu kubwa inaelekeza kumlaumu Mbowe kuliko kudai katiba mpya?

..Nadhani tumepoteza muelekeo hivi karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…