Mbowe na siasa zake za "I am the only negro incharge in here"

Si ulisema hakuna mgogoro unakuzwa na watu? Tena ukasema suluhu ni kupoteza muda? Sasa haya ya uliyoandika hapa ya Nini Tena?

..Mbowe amesema hana nongwa na Dr.Slaa na wenzake ndio maana nikasema hakuna mgogoro.

..sasa Adv.Mwabukusi naye aonyeshe utu uzima kwa kuacha kushambulia vyama vya upinzani na ku focus kwenye harakati zake.

..kuna mabandiko kadhaa hapa JF ya kumuasa Adv.Mwabukusi na wanaharakati kuepuka kuzua malumbano na wapinzani kwani kufanya hivyo kutampotezea muda na nguvu zake na kuharibu malengo ya harakati zake.

..hata sisi hapa siku nzima tunabishana wenyewe kwa wenyewe badala ya kuchochea moto wa Katiba Mpya na kulinda rasilimali zetu.
 
Mwabukusi hajataja jina la chama chochote, bali anazungumzia wanasiasa wenye akili za ubunge kuliko picha pana ya mabadiliko nchini. Na anachosema ni sahihi!
 

Si ulishasema hakuna mgogoro? Si tufanye haupo ndugu?
 
It seems bila Chadema mikutano ya sauti ya wantanzania haiwezi kufanyika.Kama ni hivyo basi Chama kiheshimiwe hadi hapa kilipofika.
 
Imagine jamaa ni mwenyekiti miaka 20+
Hana kiasi.
 
Mbowe ni mnafiki na mrafi iko ndo kinamharibia uzarendo wake wote, Ila Slaa,Mwabukusi na Mdude ni vichaa kabisa Ati wanaipa Serkali 30 days wao ka jesh vile😅
ACT siwazugumzii sina muda wa kuchambua Wapuuzi.
Binadamu ni Lisu tu., Kama Lisu hatokua kwenyekiti wa CDM basi wacha CCM itawale milele hatuwezi wapa nchi wanafik,vichaa na Wapuuzi.
 
Si ulishasema hakuna mgogoro? Si tufanye haupo ndugu?

..yaani mna mgogoro na Cdm badala ya kuwa na mgogoro na Ccm.

..Je, unaona hiyo ni sahihi, na mnazitendea haki harakati za kudai katiba?
 
Mbowe ni mpumbavu haswaa. Natamani Lissu apate Chama cha kweli afanye siasa za kweli.

Slaa + Lissu naamini ukombozi utapatikana
 
..kama Mbowe anaonekana hafai basi wajitokeze wengine wenye uwezo na mbinu mpya.

..kwanini nguvu kubwa inaelekeza kumlaumu Mbowe kuliko kudai katiba mpya?

..Nadhani tumepoteza muelekeo hivi karibuni.
Mkuu

Kuna sehemu mbili za watu. Kwanza, huenda CCM wanataka aondoke

Pili, kuna frustration miongoni mwa Wanachama wa Chama chake kwasababu nyingi , na nina waelewa;

1. Akiwa magereza harakati za kudai Katiba mpya ziliendelea tena bila uongozi wa juu. Kuna video inaonyesha watu huko vijijini wanaimba '' Samia muachie Mbowe kiongozi wetu siyo gaidi'' wakitokea katika mkutano wa kudai katiba. Watu walitumia kifungo cha Mbowe in positive way.

Kisutu watu walikuwa wanadai Katiba mpya wala si kumlilia Mbowe kwasababu waliamini Katiba ndio jibu la Wates.

2. Alipotoka akafanya fyongo ya kwenda Ikulu siku ile akijua SSH alitaka kuzima nguvu ya Katiba.
Ilikuwa kumbana Mbowe asiendelee na harakati SSH akipanga kumhujumu! Ikalipa kwa kupoteza muda

Maridhiano aliyoanzisha na SSH yakadhoofisha jitihada za kudai Katiba, wengi wakitaraji matokeo mazuri.

Watu walijua SSH na CCM hawana nia njema. Mbowe hakujifunza kwa JPM pale Mwanza alipoomba maridhiano

Mbowe alioonywa sana kwamba hii ni mbinu ya kupoteza muda, CCM haijawahi kuwa na nia njema

Baada ya kupoteza muda kama CCM walivyotaka, Mbowe anarudi kusema maridhiano yameshindika.

Kibaya zaidi anadai Katiba na Tume huru. Hivi Tume huru inapatikanaje bila Katiba mpya. haelezi

Kuna frustration, akiwa kiongozi wa Chama kikuu cha upinzani kilichoaminiwa kubeba agenda kama mbadala wa CCM amedhoofisha jitihada za kupatikana Katiba kwasababu ya kuwa ' compromised ' na maridhiano.

Kuibuka kwa kundi la Sauti ya Tanzania ni katika kuziba Ombwe la Upinzani ! nitty gritty.
 
All these points do nothing else than making Mbowe really great and important in Tanzanian politics. He’s the pioneer of katiba mpya movement and any words claiming that Mbowe has abandoned the katiba move make him look tactful and confusing to his political enemies, which is what any politician dreams to achieve.
 
Wakati wa JPM ukimtoa Lissu hamna mtu alimpa shida kama Mdude anaweza asiwe na mkakati lakini siyo mwoga kama Mbowe. Halafu usiniambie Mbowe ana mikakati wakati kwa miaka 30 anafeli.
 
Amekuwa na soft speech sana mwenyekiti sijui kipi kimemkuta? CCM wanahitaji nginjangija kama ya TL tofauti na hapo ni kupoteza muda tu.
Wajinga wanasema siyo siasa ni harakati. Ni watu wa ajabu.
 
Mbowe ni kiongozi mwenye akili sana hata Nelson Mandela aliiaacha siasa za vurugu na ANC ikaweza kutawala South Africa.
 
Daah yaan umemchakata Mbowe hadi basi.

Je ana mazuri yake pia? Tujuze
 
Daah yaan umemchakata Mbowe hadi basi.

Je ana mazuri yake pia? Tujuze

Mwamba tumeshamzoea na Speeches zake nzuri nzuri za hamasa. Ni kweli kipaji cha kuzungumza anacho, anavutia kusikiliza. Lakini utamu wa speeches zake hautupi katiba mpya, tume huru ya uchaguzi wala kuzuia bandari zetu kwenda kwa mwarabu. Tunataka chama kiunge mkono next level ya struggle ambayo ni mass action,

Miaka 20 ya kukaa kwenye uwenyekiti wewe unaongea tu, unaongea tu, unaongea tu. Sasa leo wananchi wanataka kuraise stake juu, beef up the ante, kubonyeza kitufe cha kuongeza joto kwa CCM, na katika kuwezesha hilo tunahitaji kushirikiana na Taasisi ya Chadema ambayo na sisi kuna jasho letu humo wewe unakuja na blahblah za oooh, hamkunishirikisha, ooooh sisi siyo pressure group, kama siyo pressure nyie ni nani, ni kundi la wacheza singeli na vigodoro au kitu gani?

Hii naivety ya Mwenyekiti ya namna ya kudeal na CCM inaturudisha nyuma sana.
 
Sauti ya watanzania ni genge la wahuni
 
Mbowe amekuwa nguzo ya CDM kwa mrefu sasa, na kila mafanikio ya chama yana nguvu yake kwasababu amekuwa imara.

Ila lazima tukubali nguvu na ari ya mabadiliko inaongezeka na Mbowe hayuko tena kwenye speed hiyo, zaidi kwa maoni yangu naona anakuwa kizuizi cha ukuaji na ari ya kuleta mabadiliko.

CDM bado wako kwenye 'zidumu fikra za mwenyekiti' mawazo mapya, ubunifu mpya unapungua kila siku. Kwa miaka 20 ya uongozi wa Mbowe, wanahitaji mtu mwingine wenye fikra mpya.
 
Hii mbaya sana, upinzani kwa ujumla inatakiwa wawe active mda wote ili Serikali isilale, lakini wako kimya sana.

Nakumbuka wakati wa Magu, Lissu alikuwa vocal kwenye kila jambo mpaka Magu akasikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…