Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

"tutachukua nchi saa 4 asubuhi" lowassa 2015 mpaka naandika hapa sasa hivi ni saa 5 mchana 2020 🤣🤣🤣🤣
 
Mwanasiasa ni kiumbe muongo na msahaulifu sana,

Hata kama Lissu ndo anaibuka mshindi, Mbowe hawezi kuwa Waziri Mkuu hata kwa sekunde mbili tu labda kama katiba itakuwa suspended mara tu Tundu Lisu kuapishwa.
 
Mbowe amesema katika saa 72 zijazo Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na Mimi nitakuwa Rais

Chanzo: Mwananchi online

====

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ndani ya saa 72 zijazo, mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu anakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia anagombea ubunge jimbo la Hai, alitahadharisha kuwa kitendo chochote cha kuwazuia mawakala wao 80,160 nchi nzima wasiingie kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 28, kunaweza kubadili historia ya Tanzania.

Hivyo, aliisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vyombo vya Usalama, kuhakikisha hakuna jaribio lolote la kuwazuia mawakala wao kuingia kwenye vituo kusimamia upigaji kura na wao watakuwa tayari kukubali matokeo kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

"Uchaguzi huu sio kati ya Chadema na CCM wala uchaguzi huu sio kati ya Lissu na Magufuli (mgombea urais wa CCM) bali ni kati ya wanaopenda uhuru na haki na waliokandamiza uhuru na demokrasia," alisema Mbowe.

Mbowe amesema wamezunguka mikoa yote ya Tanzania na wananchi wapo tayari kufanya mabadiliko ya uongozi na kusisitiza kuwa kwa mwonekano na hamasa waliyoionyesha Watanzania, Lissu anakwenda kuwa Rais ndani ya saa 72 zijazo.

Hivyo, ameitaka NEC kuhakikisha uchaguzi huu hauvurugwi kwa namna yoyote kwa sababu gharama yake itakuwa kubwa na kusisitiza kuwa wako tayari kukubali kushindwa kama NEC na vyombo vingine vitahakikisha uchaguzi umekuwa wa wazi, huru na haki.
Akimaliza kuota ataamka then maisha mengine yataendelea
 
Habari kama hii iko chini mno ya kiwango cha aina yoyote!

Hao mawakala waliotolewa nje na kunyimwa 8,000/ wao ni wapumbavu hawajui hata wafanye nini?

Hao wanaotoa hizo 8,000/ na kutoa maelekezo uliyoleta hapa, hivi wanazo akili kichwani?

Unapoweka taarifa hapa JF, jitahidi kidogo kujua kwamba wanaosoma habari yako wana uelewa mkubwa kukuzidi wewe.

PUMBAVU kabisa.

Watu kama nyinyi ndio mnaoharibu mwonekano wa vyama vya upinzani.
Elfu themanini sio nane.
 
Mbowe amesema katika saa 72 zijazo Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na Mimi nitakuwa Rais

Chanzo: Mwananchi online

====

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ndani ya saa 72 zijazo, mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu anakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia anagombea ubunge jimbo la Hai, alitahadharisha kuwa kitendo chochote cha kuwazuia mawakala wao 80,160 nchi nzima wasiingie kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 28, kunaweza kubadili historia ya Tanzania.

Hivyo, aliisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vyombo vya Usalama, kuhakikisha hakuna jaribio lolote la kuwazuia mawakala wao kuingia kwenye vituo kusimamia upigaji kura na wao watakuwa tayari kukubali matokeo kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

"Uchaguzi huu sio kati ya Chadema na CCM wala uchaguzi huu sio kati ya Lissu na Magufuli (mgombea urais wa CCM) bali ni kati ya wanaopenda uhuru na haki na waliokandamiza uhuru na demokrasia," alisema Mbowe.

Mbowe amesema wamezunguka mikoa yote ya Tanzania na wananchi wapo tayari kufanya mabadiliko ya uongozi na kusisitiza kuwa kwa mwonekano na hamasa waliyoionyesha Watanzania, Lissu anakwenda kuwa Rais ndani ya saa 72 zijazo.

Hivyo, ameitaka NEC kuhakikisha uchaguzi huu hauvurugwi kwa namna yoyote kwa sababu gharama yake itakuwa kubwa na kusisitiza kuwa wako tayari kukubali kushindwa kama NEC na vyombo vingine vitahakikisha uchaguzi umekuwa wa wazi, huru na haki.
Mbowe akumbuke Waziri Mkuu ni negotiated post kati ya Executive na Parliament.... siuwaziri wa kawaida wa mtu kuamua tu na mkewe au chama chake... Na sasa ndio ieleweke kauli ya Mama Samia aliposema "CCM lazima itaunda Serikali", alikuwa amepiga mahesabu ya kuwa na majority seats Bungeni.
 
na mna uchu balaa !

ila bahati mbaya sasa ikulu mtaitazama kwenye video nchi sio mke kwa unakabidhiwa tu
 
Aendelee kuota na makengeza yake hayo , nchiii tunakabidhi JPM kwa kura za kishindo

sent from HUAWEI
 
Kuna watu wanaongea utafikiri Tz ni ya kipekee sana kwa hiyo machafuko hayawezi kutokea na kwamba huko yanakotokea labda hawana mungu au ni wakosaji.Kumbe kuna waliokua na utulivu na (amani??) kuliko sisi lakin muda uliongea.
 
Tumkumbushe tu bwana Freeman Yeye sasa ni mtu huru kama Jina lake halafu pia Ili uwe waziri mkuu lazima uwe mbunge wa kuchaguliwa na wananachi
 
Mbowe amesema katika saa 72 zijazo Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na Mimi nitakuwa Waziri mkuu

Chanzo: Mwananchi online

====

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ndani ya saa 72 zijazo, mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu anakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia anagombea ubunge jimbo la Hai, alitahadharisha kuwa kitendo chochote cha kuwazuia mawakala wao 80,160 nchi nzima wasiingie kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 28, kunaweza kubadili historia ya Tanzania.

Hivyo, aliisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vyombo vya Usalama, kuhakikisha hakuna jaribio lolote la kuwazuia mawakala wao kuingia kwenye vituo kusimamia upigaji kura na wao watakuwa tayari kukubali matokeo kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

"Uchaguzi huu sio kati ya Chadema na CCM wala uchaguzi huu sio kati ya Lissu na Magufuli (mgombea urais wa CCM) bali ni kati ya wanaopenda uhuru na haki na waliokandamiza uhuru na demokrasia," alisema Mbowe.

Mbowe amesema wamezunguka mikoa yote ya Tanzania na wananchi wapo tayari kufanya mabadiliko ya uongozi na kusisitiza kuwa kwa mwonekano na hamasa waliyoionyesha Watanzania, Lissu anakwenda kuwa Rais ndani ya saa 72 zijazo.

Hivyo, ameitaka NEC kuhakikisha uchaguzi huu hauvurugwi kwa namna yoyote kwa sababu gharama yake itakuwa kubwa na kusisitiza kuwa wako tayari kukubali kushindwa kama NEC na vyombo vingine vitahakikisha uchaguzi umekuwa wa wazi, huru na haki.
Hivi ni mchawi gani aliyempigia ramli ya uchonganishi kijana alosto Mbowe? Ubunge kakosa na sasa anataka kulazimisha ujinga mwingine? Tumpige mawe huyu.
 
Uchaguzi sio porojo za Twitter na mihemko ya vijana ambao wengi sio wapiga kura..

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Back
Top Bottom