Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Mbowe amesema katika saa 72 zijazo Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na Mimi nitakuwa Waziri mkuu

Chanzo: Mwananchi online

====

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ndani ya saa 72 zijazo, mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu anakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia anagombea ubunge jimbo la Hai, alitahadharisha kuwa kitendo chochote cha kuwazuia mawakala wao 80,160 nchi nzima wasiingie kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 28, kunaweza kubadili historia ya Tanzania.

Hivyo, aliisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vyombo vya Usalama, kuhakikisha hakuna jaribio lolote la kuwazuia mawakala wao kuingia kwenye vituo kusimamia upigaji kura na wao watakuwa tayari kukubali matokeo kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

"Uchaguzi huu sio kati ya Chadema na CCM wala uchaguzi huu sio kati ya Lissu na Magufuli (mgombea urais wa CCM) bali ni kati ya wanaopenda uhuru na haki na waliokandamiza uhuru na demokrasia," alisema Mbowe.

Mbowe amesema wamezunguka mikoa yote ya Tanzania na wananchi wapo tayari kufanya mabadiliko ya uongozi na kusisitiza kuwa kwa mwonekano na hamasa waliyoionyesha Watanzania, Lissu anakwenda kuwa Rais ndani ya saa 72 zijazo.

Hivyo, ameitaka NEC kuhakikisha uchaguzi huu hauvurugwi kwa namna yoyote kwa sababu gharama yake itakuwa kubwa na kusisitiza kuwa wako tayari kukubali kushindwa kama NEC na vyombo vingine vitahakikisha uchaguzi umekuwa wa wazi, huru na haki.
 
Mola Ejani Leonard

“When tension extend to violent armed conflicts, these types of situation can be seen. How we fight matters because it is very painful to see young people who are going to school die Akwilina this way. If you want to fight war, attack military targets and not civilians.”

CNA

Lissu You deserve power 100%
 
Ndio keshamaliza kuhesabu kura zake nchi ya jirani?? 😆😆😆😆😆😆

mugah di mathew aona unatest mitambo ya bvr tehetehee
Subiri utafrahii mwaka huu

J5 tutaendesha interview ya uDC na uRC unaombwa kuhudhuria bila kukosa
Sifa hitajika
Mtanzania
Miaka 23 -55
Akili timamu
Ujue kusoma English na kiswahili
 
Watanzania Leo Kuna jamaa yangu kaniambia yupo kwenye usimamizi wa uchaguzi

Sasa semina Yao ya siku mbili iliyoanza leo wamepewa 80000/=

Chakushanga maneno waliyoambiwa kwamba presha huku nje ipo kubwa sana kwaiyo ikiwezekana kuua wakala waue tu ili mradi Maghufuri ashinde.

Kwanza walitolewa wote ambao walifatiliwa habari zai zikaonekana zinavinasaba vya upinzani.

Jaman tuweni makini uchaguzi huu ni hatari sana Kuna watu wapo tayari kuwa ili Meko ashinde usimwamini mtu.

Haki huinua TAIFA
 
Mola Ejani Leonard

“When tension extend to violent armed conflicts, these types of situation can be seen. How we fight matters because it is very painful to see young people who are going to school die Akwilina this way. If you want to fight war, attack military targets and not civilians.”

CNA

Lissu You deserve power 100%
Kiingereza kina tabia mbaya Sana. Haikiwapendi wanaokipenda.
 
Watanzania Leo Kuna jamaa yangu kaniambia yupo kwenye usimamizi wa uchaguzi

Sasa semina Yao ya siku mbili iliyoanza leo wamepewa 80000/=

Chakushanga maneno waliyoambiwa kwamba presha huku nje ipo kubwa sana kwaiyo ikiwezekana kuua wakala waue tu ili mradi Maghufuri ashinde.

Kwanza walitolewa wote ambao walifatiliwa habari zai zikaonekana zinavinasaba vya upinzani.

Jaman tuweni makini uchaguzi huu ni hatari sana Kuna watu wapo tayari kuwa ili Meko ashinde usimwamini mtu.

Haki huinua TAIFA

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app

lenyu Kwanini mnapenda kujitisha na kutishana hivyo?
Tufate sheria na taratibu za uchaguzi
IGP amesema wako tayari kutulinda wananchi na mali zetu
 
Back
Top Bottom