Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

Uchaguzi 2020 Mbowe: Ndani ya saa 72 nitakuwa Waziri Mkuu

IGP ni mmoja wa taasisi zilizo kwenye mpango wa kunajisi uchaguzi. Ccm ndio wana imani na IGP maana wanaweza kumtumia kulinda ushindi haramu.

Wewe na wagombea wako mnalindwa na nani?
 
Huyo anaongelea wasimamizi wa uchaguzi na anachosema ni ukweli mtupu
Ndani ya chumba uchaguzi kuna mawakala wa vyama 16 Huyo mmoja tu sijui wa chadema nani ahangaike naye.

Chadema mnaanza kuhaha.Safari hii ngoja watu wa Dar es salaam tuongoze mikoa mingine kuwanyima kura.Tumewachoka kwa mambo yenu ya kizushi na uongo yasiyoisha .Tarehe 28 October chadema mnafungashwa virago Dar es salaam for good
 
Mbowe amesema katika saa 72 zijazo Tundu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na Mimi nitakuwa Rais


Chanzo: Mwananchi online


==
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema ndani ya saa 72 zijazo, mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu anakwenda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo Jumapili Oktoba 25 katika mji mdogo wa Bomang'ombe wilaya ya Hai wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni huku akisema Mungu akipenda, yeye anakwenda kuwa Waziri mkuu.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia anagombea ubunge jimbo la Hai, alitahadharisha kuwa kitendo chochote cha kuwazuia mawakala wao 80,160 nchi nzima wasiingie kwenye vituo vya kupigia kura Oktoba 28, kunaweza kubadili historia ya Tanzania.

Hivyo, aliisihi Tume ya Taifa ya Uchaguzi na vyombo vya Usalama, kuhakikisha hakuna jaribio lolote la kuwazuia mawakala wao kuingia kwenye vituo kusimamia upigaji kura na wao watakuwa tayari kukubali matokeo kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki.

"Uchaguzi huu sio kati ya Chadema na CCM wala uchaguzi huu sio kati ya Lissu na Magufuli (mgombea urais wa CCM) bali ni kati ya wanaopenda uhuru na haki na waliokandamiza uhuru na demokrasia," alisema Mbowe.

Mbowe amesema wamezunguka mikoa yote ya Tanzania na wananchi wapo tayari kufanya mabadiliko ya uongozi na kusisitiza kuwa kwa mwonekano na hamasa waliyoionyesha Watanzania, Lissu anakwenda kuwa Rais ndani ya saa 72 zijazo.

Hivyo, ameitaka NEC kuhakikisha uchaguzi huu hauvurugwi kwa namna yoyote kwa sababu gharama yake itakuwa kubwa na kusisitiza kuwa wako tayari kukubali kushindwa kama NEC na vyombo vingine vitahakikisha uchaguzi umekuwa wa wazi, huru na haki.
Kabla ya uchaguzi, mwanasiasa kazi yake ni kuomba kura.

Hii kauli ya Mbowe, kama kweli kaitoa, inaweza kutafsirika kuwa Mbowe hahitaji kura za watu, kashapata uhakika wa kuwa Waziri Mkuu.

Hivyo, wengine ambao walitaka kumpigia kura wakasema huyu hahitaji kura zetu, kashapata uhakika wa kuwa Waziri Mkuu. Labda tuwapigie wanaozihitaji.

Nilimsema Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kusema wananchi wakipigia kura CCM au wasipopigia kura CCM, CCM itashinda tu.

Narudia kumsema Mbowe, kwa sababu hizo hizo.

Kabla ya uchaguzi, mwanasiasa kazi yake ni kuomba kura.

Masaa 72 yajayo ni mengi sana. Mbowe hawezi kujua atakuwa nani.

Inawezekana kabisa akawa mfungwa wa kisiasa.
 
Hivi mawakala ni walipwa shilingi ngapi kwa siku?

Ushindi ni sayansi na sayansi ni hesabu💥
Wanalipwa teuzii
Kwahiyo CHADEMA mnampango wa kuwa na teuzi zaidi 80,000 kwa mawakala wenu tuu?
Ndio ma D.C. 😆😆
Teuzi ni nyingi tunafyeka maDC,RC,DAS,RAS,RSO,mabalozi ,MaDED ,wakurugenzi wa mashirika ya umma,Wenyeviti wa taasisi za serikali nk

Nadhani unatakiwa taasisi ya urais isafishe vibaraka wa mafisadi zaidi ya 100K
 
Maalim Seif asema msimamo wake ni "JINO kwa JINO"
Zamani sana hii, sikua hata naelewa vizuri maana uchaguzi ila ndio lilikua chimbuko la neno ngunguri
GENTAMYCINE Ulikua wapi kipindi kile

download.jpeg
.....
 
Back
Top Bottom