Lissu kugombea uenyekiti anaonekana na mwenyekiti wake kama muasi.
Kwani uenyekiti chadema ni mali binafsi ya mbowe?Alitakiwa amwache atangulie haya yote yasingetokea.
Ikiwa LISSU anaweza kuwatendea watu waliookoa maisha yake vipi sisi asiotufahamu ?.
Kosa la Lisu ni kugombea uenyekiti?
Mbowe alitakiwa kusoma alama za nyakati na kuondoka kwa heshima.
Kwa nini kila anayegombea anakuwa adui kwake?
Alianza Chacha Wangwe akafuata zitto kabwe,wote hao waliundiwa zengwe na kufukuzwa. Kumbe walionewa sana, tatizo ni Mbowe mwenyewe kujinufaisha kupitia CDM.
Awamu hii wapambe na machawa walitaka kuleta story zao za usaliti,umma ukawagomea na sasa wanahaha kumnusuru sultani na aibu inayokuja lakini hawatofanikiwa.
Wangekuwa wanampenda badala ya kujali matumbo yao,wangemwambia ukweli akajiuzuru kwani hakubaliki hadi huku chini mashinani.