Alitakiwa amwache atangulie haya yote yasingetokea.
Una maana Tundu Lissu angetangulia/kufa..?
Haa haa🤔🤔🤔....
Naona roho ya mwana wa kuasi (ibilisi) ndani ya Freeman Mbowe na Team Mbowe kwa ujumla, inaanza kujidhihirisha wazi wazi sasa eti kwa sababu ya uenyekiti tu wa CHADEMA..!
Hivi Tundu Lissu kamkosea nini hasa kiasi cha kuchukia na kupagawa kiasi hiki? Kwa sababu ya uenyekiti tu au kuna kingine..??
Lakini la kuhusu uhai wa Tundu Lissu acheni kukufuru ndugu
Ngongo msije kujipalilia hukumu mbaya ya bure tu toka kwa Mungu Jehovah...
Kwa sababu mkono wa Bwana, Mungu wa majeshi, muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyopo hai na visivyo hai NDIYE ALIYEOKOA UHAI WA TUNDU LISSU. Sifa, heshima na utukufu ni zake milele..!
Hujiulizi ktk hali ya kawaida ni binadamu gani duniani amewahi kumwagiwa risasi 16 mwilini mwake akabaki hai na bila kuathirika hata kiakili? Hatuoni kuwa huu ni udhihirisho wa wa nguvu na uwezo wa Mungu peke yake ndiyo ulizuia kifo cha huyu bwana..?
Kama kuna watu wanaweza kuanza kukufuru kwa kujaribu kujitwalia heshima na utukufu wa Mungu ktk hili, Amini amini nasema, Yesu Kristo atawahukumu...!
Ikiwa LISSU anaweza kuwatendea watu waliookoa maisha yake vipi sisi asiotufahamu ?.
Kawatendea kitu gani kibaya jamani..?
Mbona mnalialia tu pasipo kunyoosha maneno..?
Kama ni ishu ya uenyekiti, si tumekubaliana kuwa HII NDIYO DEMOKRASIA kwa kila mtu kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi..?
Au kuna mengine tusiyoyajua ukiacha hili la uenyekiti..??
Kwanini tusiwe waungwana tu kwa kujieleza kwa wapiga kura na sanduku la kura liamue hiyo tarehe 21/1/2025..?
Mnaogopa nini kiasi cha kutamani mpate ushindi nje ya sanduku la kura..??