Pre GE2025 Mbowe: Nitajiuzulu siasa 2025 endapo CCM itashinda angalau kiti kimoja tu cha jimbo mkoani Kilimanjaro

Pre GE2025 Mbowe: Nitajiuzulu siasa 2025 endapo CCM itashinda angalau kiti kimoja tu cha jimbo mkoani Kilimanjaro

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe ametangaza kujiuzulu kufanya siasa endapo Chama cha Mapinduzi (CCM) kitashinda angalau kiti kimoja tu cha jimbo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro wenye majimbo tisa (9) ya uchaguzi.

Mbowe ametangaza ahadi hiyo Julai 05.2024 wakati akizungumza na wakazi wa Maore, wilayani Same, mkoa wa Kilimanjaro kwenye muendelezo wa mikutano ya hadhara ya chama hicho inayolenga kufikia mikoa yote ya kanda ya Kaskazini ikiwa ni muendelezo wa 'oparesheni +255 Katiba mpya' ambapo amesema msingi wa kuweka ahadi hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mkoa wa Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini kwa ujumla wake CHADEMA imekuwa nguzo imara mara zote.

Ametolea mfano uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi) uliohusisha vyama vingine vitatu (3) wakati huo vya CUF, NCCR Mageuzi na NLD, vyama vya upinzani vilishinda majimbo saba (7) kati ya tisa (9) ya mkoa wa Kilimanjaro.

Ametaja majimbo yaliyochukuliwa na upinzania kuwa ni pamoja na Same Mashariki, Rombo, Vunjo, Moshi vijijini, Moshi mjini, Hai na Siha, huku CCM ikiambulia majimbo ya Mwanga na Same pekee, hivyo kutoa wito kwa wakazi wa Same na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla wake kujipanga sawasawa ili kurejesha heshima hiyo kwa kuhakikisha wanashinda sehemu zote kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu (2024) na uchaguzi mkuu mwakani (2025)

Kuhusu mkoa wa Arusha, Mbowe ameeleza kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CHADEMA iliibuka kidedea kwenye majimbo sita (6) kati ya saba (7) yaliyoko mkoani humo, ambapo CCM iliambulia jimbo moja (1) pekee ambalo ni la Ngorongoro, jambo ambalo amedai kuwa haoni dalili ya CCM kushinda tena kwenye jimbo hilo kwa kuwa wakazi wa Ngorongoro wameahidi kuipigia kura CHADEMA kutokana na kile alichodai kuwa shukrani ya chama tawala (CCM) na serikali yake baada ya kuchaguliwa ni kuwahamisha watu wa jamii ya Masai kutoka kwenye eneo lao la asili na kuwapeleka Msomera, wilayani Handeni, mkoani TangaAidha, kwa upande wa mkoa wa Tanga.

Mbowe amebainisha kuwa mkoa huo umekuwa ngome ya CCM kwa miaka mingi kwani katika majimbo 12 ya uchaguzi yaliyopo mkoani humo CCM ilikuwa inashinda majimbo yote, hata hivyo amedai kuwa kufuatia mikutano 72 aliyoifanya hivi karibuni kwenye mkoa huo tathmini ya CHADEMA inaonyesha kuwa majimbo pekee ambayo CCM inaweza kushinda ni matano (5) tu huku CHADEMA ikiwa na uhakika wa 'kunyakua' majimbo yote yaliyosalia ambayo ni saba (7).

Mbowe ametoa wito kwa wakazi wa Same, mkoa wa Kilimanjaro na kanda ya Kaskazini kwa ujumla wake kuhakikisha wanashinda chaguzi zote zijazo, yaani kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji baadaye mwaka huu (2024) na uchaguzi mkuu mwakani (2025) kuanzia kwenye viti vya Madiwani ili waweze kuunda Halmashauri, Wabunge na hatimaye nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile alichodai kuwa chama hicho kinaenda kuunda serikali baada ya uchaguzi mkuu wa mwakani (2025).

Screenshot 2024-07-06 at 15.05.07.png
 
Kila chama huwa kuna sehemu kinakuwa kinakubalika zaidi ndio maana utasikia hii ni ngombe ya chama fulani. Sasa huko ni ngombe ya chamba hicho.

Japo siikubali chadema ya sasa na viongozi wake akiwemo mbowe, ila acha kumlisha maneno.
 
Democratic nao wanamajimbo yao ,moja tu likimpigia mgombea wa republican hasa trump , sahau kuingia marakani democratic

Sembuse ,arusha kwahiyo sugu naye akitamka Kanda ya nyasa kuchukuliwa na ccm hatajimbo moja tayari kitakuwa chama wahehe ,wanyakyusa wabena au kikanda.....akili zenu maandazi hizo
 
Kila chama huwa kuna sehemu kinakuwa kinakubalika zaidi ndio maana utasikia hii ni ngombe ya chama fulani. Sasa huko ni ngombe ya chamba hicho.
Japo siikubali chadema ya sasa na viongozi wake akiwemo mbowe, ila acha kumlisha maneno.
Nilitaka kumpa hii fact kuwa kanda ya kaskazini ni ngome ya chadema na ndio sababu ya yeye kusema hivyo.

Shida ya hawa mazombie huwa juu ya shingo zao wamebeba maboga.
 
Ila mbowe mjanja sana kwa wanachadema wenzake 😂 kisa wameshaahidiwa kurudi bungeni ety ataachia uenyekiti ccm wakishinda jimbo moja Kilimanjaro 😂

Yn hapo kwa ufupi ni kwamba, jamaa bado yupo sana hapo kwenye kiti 😂
 
Ndiyo maana wachaga huwa hawakimbii chadema
 
Back
Top Bottom