Yeah aliahidi kustaafu uenyekiti 2023 nashangaa anajiandaa kugombea urais. Hata hizi ziara zinambrand yeye kuliko chadema. This guy atupishe awe mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ila sio active politics. We need changes mtu kama Lissu, Heche, au Golugwa awe mwenyekiti.
Unanichanganya sana mkuu 'zitto junior'.
Wewe ni mtu niliyekufahamu muda kitambo humu JF kutokana na maoni yako uliyochangia toka nikufahamu.
Nilikuelewa sana, sana nilipoanza hii safari ya kukufahamu humu, kwa umahiri wako wa maoni yanayoambatana na ushahidi sahihi wa maoni hayo. Tumepita kwa pamoja, na huyu Mwenyekiti wakati wa hali ngumu sana enzi za Magufuli, na sote tulimsifu alivyoweza kukisalimisha chama chenu kilivyokuwa kikipikwa kwenye tanuru lile.
Wakati wote huo, sikumbuki kama ilitokea nikawa na shaka yoyote juu ya msimamo uliokuwa ukikuongoza katika uamini wako.
Lakini alipoingia Samia na hadaa zake za "maridhiano" yaliyoonekana kumnasa Mwenyekiti, nikaona kwa mara ya kwanza ukigeuka nyuma (sijui kama uligeuka kuwa gunia la chumvi!).
Hivyo vi-maneno vichache nilivyo weka hapo nawe ukavijibu kama hivi ulivyojibu...
Ndani ya CCM kuna watu wenye uwezo na ujuzi mkubwa katika mambo ya kuchanganya watu. Mchungaji Msigwa kachanganywa na kuchanganyika. Kule mwenzake Sugu, ni kama hatujui kulitokea kitu gani, na sote tunajifanya kama tumesahau..., hizi ni kazi za CCM!
Sikutaka kutumia maneno mengi haya kueleza jambo ambalo pengine sikuliweka bayana lieleweke.
Lakini nimalize tu kwa kukuondoa shaka. Sina wasiwasi wowote na uwezo wa uelewa wako wa maswala kama haya, kama walivyo wengi wetu hata walioko kule ndani ya CCM, lakini wanaamua tu kutumikia maslahi zaidi kuliko huu ujumla wetu wa kiTanzania.
Hayo uliyo andika hapo juu, nitaendelea kuyatafakari kwa kina zaidi. naomba unisamehe kwa kuwa 'personal' kiasi hiki.