Mbowe: Sijipendekezi kwa Rais Samia, ninachotafuta ni haki

Sisi tunaomfuatilia tumeona anajipendekeza ASITUPANGIE TUNAYOONA
 
Atafute kwanza haki ndani ya Chadema ikishapatikana ndo atoke nje, sawa Mwenyekiti wa kudumu?
 
Kwani ukisema unajipendekeza nini kitabadilika?

Mheshimu sana mtu aliyepewa mamlaka na Mungu.Kujishusha sio ajabu ila kujitutumua kwa vimaneno vya ubabe uchwara ndilo jambo linawafedhehesha hawa chadema.
Alikuwepo "chuma" kila mtu alinyooshwa na wakawa kama vifaranga vya kuku.Sasa hivi wanatakiwa kuwa wastaarabu na waongee kwa staha
 
Ameanza kufanya vikao ili kuwahadaa wafuasi wake kwamba kwamba ruzuki zilitumika kufanya vikao nchi nzima.
 
Wakati huohuo Zitto Kabwe yupo bize kusaka teuzi viti 2 vya wabunge alivyobakiza rais .
 
Chuma sasa hivi anawanyooshea wapinzani wapi ?
 
Kwani mbowe ana elimu gani?
Hata akijipendekeza saaana labda awe mlinzi wa kufungua mlango ikuru
Wenye elimu wanajipendekeza kwa sababu nafasi za kutumikia nchi zinahitaji wasomi.
Ikulu ya Tanzania nayo inahitaji wasomi? Kwa umasikini huu tulionao, ni ngumu kusema nchi hii inaongozwa na wasomi. Wasomi hawa waliolelezwa na dhalimu wakatengeneza kibanda cha kujifukiza hapo muhimbili, badala ya kufanya vipimo ndani ya maabara?
 
Kwani mbowe ana elimu gani?
Hata akijipendekeza saaana labda awe mlinzi wa kufungua mlango ikuru
Wenye elimu wanajipendekeza kwa sababu nafasi za kutumikia nchi zinahitaji wasomi.
Kuna kusoma, kuna kueleimika na **** suala la akili.

Hivi unaweza kusema mtu kama marehemu, Ndugai au Kabudi, japo wamesoma, lakini wameelimika?

Kuna watu wamekaa miaka mingi madarasani wakikariri lakini wakatoka wakiwa watu wa hovyo, wasioelimika na wala hawana maarifa.
 
Kwani mbowe ana elimu gani?
Hata akijipendekeza saaana labda awe mlinzi wa kufungua mlango ikuru
Wenye elimu wanajipendekeza kwa sababu nafasi za kutumikia nchi zinahitaji wasomi.
Hakuna aliyeelimika anayejipendekeza kwa mtu.
 
Mbowe anazidi kuwabrainwash wafuasi wake sugu
Unapomzungumzia Freeman Aikaeli Mbowe, unapswa kuwa mtulivu. This is the only worthlistening political party leader in Tanzania. Her Excellency Samia Suluhu Hassan is as well a great Public Speaker.
 
Siyo majambazi, mafisadi na wachezea mifumo ya serikali tu wanaomjaribu rais Samia hata Chadema wanamjaribu.

Leo wametangaza maandamano ya kudai katiba mpya na tume huru yani wanataka rais aache kufocus na kukamilisha SGR ,Bwawa la nyerere ,ajira, viwanda ambavyo ndiyo hitaji la wananchi akaanze kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya katiba ambayo ni hitaji la wanasiasa tu?

Mbaya zaidi wanataka mchakato wa katiba uanze upyaaaaa na siyo pale ulipoishia zamani
 
Hawautaki mchakato wa Prof Kabudi na Polepole?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…