Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Nilishaleta uzi humu, kama serikali ina struggle kukusanya kodi hadi inaamua kuleta tozo ambazo ni mzigo kwa wananchi huku ikijua fika wananchi tayari wanalemewa na mfumuko wa bei na vipato vyao vimebaki palepale au vimeendelea kupungua, kuna justification gani ya kuendelea kuagiza magari ya kifahari ya V8 kwa ajili ya viongozi na watawala?​
 
Jambo hili litatatuliwa na KATIBA mpya ya Warioba.

Viongozi wote wa chama tawala na upinzani Wana Maslahi nalo hivyo hawawezi kuligusa ipasavyo.

Ameeen.
 
Mimi siyo mpinzani lakini namuunga mkono kwa hili.Kusema kweli tozo za benki zinaudhi sana aisee.kwani kuweka hela bank ni makosa? kupitisha mshahara bank ni makosaz? mtu umelipia PAYE ,bank inaka service charge na bank inakata tozo.hapa nayeumia ni mfanyakazi.mfanyabiasha anaweza kuamua hela yake isipite bank and asiweke bank.
 

..ungelaumu viongozi wa serikali na Ccm wanaotumia bure ma-V8 na magari mengine ya kifahari ya serikali.

..kwasababu waliokopeshwa wanarejesha mikopo yao, ungeshauri serikali iwakopeshe viongozi ma-V8, badala ya kubeba mzigo wa kununua na kuhudumia utitiri wa magari ya serikali.
 
Mtaalam Mbowe
 
Unadhani kwa upande wake yeye amefanya vya kutosha?
 
Hoja nzuri.

Bt tuseme Kweli, Mnyika anaweza akasimama jukwaani na kumwambia mwananchi haya?

Ndugu wananchi, mmetozwa tozo, mmeminywa Kodi Kila Mahali, nichagueni niwawakilishe,

Nitapofika bungeni nitalipwa zaidi ya ml 12 Kwa mwezi, Nitakopeshwa gari ya ml 800 na ntailipa polepole ingawa najua wananchi wengi hapa wanamiliki BAISKELI. Pia wanakosa pesa za matibabu wakiugua.

Nikimaliza ubunge mtanilipa zaidi ya ml 200 kama Asante ya kuwatumikia.


Jambo hili ni la kimfumo. Tuwabane kwenye KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ameeen.
 
Maandamano si kitu ambacho ndio tunakihitaji bali ni moja wapo ya njia ya kuonesha hisia zetu, hivyo zipo njia zengine za kuonesha hisia zetu kama maandamano inashindikana kwa kuogopa virungu.
Is why tuko hapa. Kutoka hamuwezi sababu mmetishiwa virungu, na hili wameshalijua kwahiyo wanajua hamna namna zaid ya social media.
 
Ni kweli kuwa wananchi ni waoga ila siamini kama Chadema inaweza fanya jambo lolote la maana katika Taifa letu kwa sasa.

Chadema imeshindwa kufanya lolote ilipokuwa ya moto kwa sasa viongozi wake wakuu wamejichokea na kukata tamaa.
Mnaposema wananchi waoga huwa mnaama kwamba walitakiwa kufanya nini ili kuonesha kuwa sio waoga?
 
mbowe alinunua hio gari akiwa wazir kivuli lumumba inamazezeta kweli.
Mafuta ya kuweka kwenye gari hiyo yalitokana na POSHO alizolipwa na wananchi maskini Ili aendeshe magari hayo ya kifahari.

Tunataka mfumo imara kama uingereza, mbunge analipwa kama watumishi wengine wa Serikali,

Wanapanda treni za umma kama wananchi wengine, mbona enzi za Nyerere wabunge walipanda treni kwenda Dom bungeni?

Ni muda wa Kupata KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ameeeen.
 
Mtu anayetaabika halafu halalamiki wala kudai haki yake inafaa akejeliwe ili akili imkae sawa. Kwasabb hawa hawa wananchi wanaoumia ndiyo uchaguzi ukifika unakuta akili zinafubazwa na ubwabwa, kanga na kofia
Kwamba mtu anaamka kwake na kwenda kupiga kura kisa kapewa kofia?
 
Kusema kweli tukiwanyamazia hawa wenye dhamana sasa hivi watatuuzia humu ndani! kama wananunua mabasi 60 kwa fedha za udhulamati wa kodi zetu tutarajie nini zaidi? Tuseme inatosha!
 
Kwamba mtu anaamka kwake na kwenda kupiga kura kisa kapewa kofia?
Ndiyo na kandambili iliyokatika kipande kwa kuchanwa na gwambara. Kavaa tshirt na kofia yenye picha ya mwanamme/mwanamke mwenzake
 
Aliyechelewa kuongea ni bora sana kuliko aliyenyamaza kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…