Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Nilishaleta uzi humu, kama serikali ina struggle kukusanya kodi hadi inaamua kuleta tozo ambazo ni mzigo kwa wananchi huku ikijua fika wananchi tayari wanalemewa na mfumuko wa bei na vipato vyao vimebaki palepale au vimeendelea kupungua, kuna justification gani ya kuendelea kuagiza magari ya kifahari ya V8 kwa ajili ya viongozi na watawala?​
 
Nilishaleta uzi humu, kama serikali ina struggle kukusanya kodi hadi inaamua kuleta tozo ambazo ni mzigo kwa wananchi huku ikijua fika wananchi tayari wanalemewa na mfumuko wa bei na vipato vyao vimebaki palepale au vimeendelea kupungua, kuna justification gani ya kuendelea kuagiza magari ya kifahari ya V8 kwa ajili ya viongozi na watawala?​
Jambo hili litatatuliwa na KATIBA mpya ya Warioba.

Viongozi wote wa chama tawala na upinzani Wana Maslahi nalo hivyo hawawezi kuligusa ipasavyo.

Ameeen.
 
Mimi siyo mpinzani lakini namuunga mkono kwa hili.Kusema kweli tozo za benki zinaudhi sana aisee.kwani kuweka hela bank ni makosa? kupitisha mshahara bank ni makosaz? mtu umelipia PAYE ,bank inaka service charge na bank inakata tozo.hapa nayeumia ni mfanyakazi.mfanyabiasha anaweza kuamua hela yake isipite bank and asiweke bank.
 
Najua Mbowe ni TAJIRI.

Ninachopinga ni Mbowe huyo huyo aliekopeshwa V8 akiwa Waziri mkuu KIVULI Kambi ya upinzani na wabunge wote wa upinzani waliyapokea bila kukataa.

Leo wanapata wapi mamlaka ya kuhoji magari ya mawaziri ya kifahari.

Jambo hili mwenye Uhalali wa kuhoji ni MWANANCHI anaekamuliwa.

Katika Katiba mpya tusiwaachie wanasiasa watusemee sababu yapo yanayowanufaisha hawawezi yasimamia.

Naichukia sana CCM naiombea IFE, bt pia Nawakosoa Upinzani Ili wakae Kwa mstari wanapopotoka.

Ameeeen.

..ungelaumu viongozi wa serikali na Ccm wanaotumia bure ma-V8 na magari mengine ya kifahari ya serikali.

..kwasababu waliokopeshwa wanarejesha mikopo yao, ungeshauri serikali iwakopeshe viongozi ma-V8, badala ya kubeba mzigo wa kununua na kuhudumia utitiri wa magari ya serikali.
 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.

Hizi hapa nukuu za Mbowe...

“Tunapowapa Watawala nafasi ya kuongoza maisha yetu na wanaamua bila kujali kinachotupata, hatupaswi kuwa waoga.

Kuna wakati nakwazika sana kwa kazi ninayofanya mnapokuwa waoga na hofu, halafu mnalalamika.

Hao wanaowatoza kodi hiyo wanakwenda kununua V8 ya Shilingi Milioni 450 au 500, mtu ambaye angekuwa nyumbani kwa mumewe au mkewe asingeweza kununua V8.

Lakini kwa kuwa kuna pesa ya Wajinga Watanzania wanaweza kununua gari la kumpa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Jaji kila mmoja.

Jiulizeni ni Wafanyabiashara wangapi ambao wana uwezo wa kuendesha magari mapya?

Magari mapya Nchi hii ni mali ya viongozi wa Serikali, na mnavyokaa kimya mambo haya ndiyo yanaendelea, mnatakiwa kuamka.

Kama mnataka kuibadilisa Nchi hii lazima tuache woga, lazima viongozi wa dini muongee.

Nilimwambia Rais Samia hii simulizi ya ‘amani’ ‘amani’ ‘amani’ ni kupoteza muda, simulizi sahihi ni haki haki haki.

Kuwepo na haki kwa watu wote litakuwa tafa bora la kuishi. Watanzania wameangalia uchaguzi wa Kenya kila mmoja ametamani, ulikuwa wa wazi hakuna mizengwe
Mtaalam Mbowe
 
Hii kauli ya Mbowe kwamba "nakwazika sana kuona wanakuwa waoga" inaonesha bado ana dhamira ya dhati kuleta mabadiliko nchi hii.

Kinachomkwamisha ni kukosekana kwa ushirikiano anaohitaji toka kwetu, tupo kama misukule ndio maana naye anajua hilo, japo ameshindwa kutumia hilo neno kwa heshima yake aliyonayo kwetu.

Naamini wale wajuaji wanaosema kila siku Mbowe amelamba asali ndio maana yupo kimya, sasa ni wakati wao kum-prove wrong Mbowe, simameni mhesabiwe kulinda haki zenu ili Mbowe awe pamoja nanyi.
Unadhani kwa upande wake yeye amefanya vya kutosha?
 
..ungelaumu viongozi wa serikali na Ccm wanaotumia bure ma-V8 na magari mengine ya kifahari ya serikali.

..kwasababu waliokopeshwa wanarejesha mikopo yao, ungeshauri serikali iwakopeshe viongozi ma-V8, badala ya kubeba mzigo wa kununua na kuhudumia utitiri wa magari ya serikali.
Hoja nzuri.

Bt tuseme Kweli, Mnyika anaweza akasimama jukwaani na kumwambia mwananchi haya?

Ndugu wananchi, mmetozwa tozo, mmeminywa Kodi Kila Mahali, nichagueni niwawakilishe,

Nitapofika bungeni nitalipwa zaidi ya ml 12 Kwa mwezi, Nitakopeshwa gari ya ml 800 na ntailipa polepole ingawa najua wananchi wengi hapa wanamiliki BAISKELI. Pia wanakosa pesa za matibabu wakiugua.

Nikimaliza ubunge mtanilipa zaidi ya ml 200 kama Asante ya kuwatumikia.


Jambo hili ni la kimfumo. Tuwabane kwenye KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ameeen.
 
Maandamano si kitu ambacho ndio tunakihitaji bali ni moja wapo ya njia ya kuonesha hisia zetu, hivyo zipo njia zengine za kuonesha hisia zetu kama maandamano inashindikana kwa kuogopa virungu.
Is why tuko hapa. Kutoka hamuwezi sababu mmetishiwa virungu, na hili wameshalijua kwahiyo wanajua hamna namna zaid ya social media.
 
Ni kweli kuwa wananchi ni waoga ila siamini kama Chadema inaweza fanya jambo lolote la maana katika Taifa letu kwa sasa.

Chadema imeshindwa kufanya lolote ilipokuwa ya moto kwa sasa viongozi wake wakuu wamejichokea na kukata tamaa.
Mnaposema wananchi waoga huwa mnaama kwamba walitakiwa kufanya nini ili kuonesha kuwa sio waoga?
 
mbowe alinunua hio gari akiwa wazir kivuli lumumba inamazezeta kweli.
Mafuta ya kuweka kwenye gari hiyo yalitokana na POSHO alizolipwa na wananchi maskini Ili aendeshe magari hayo ya kifahari.

Tunataka mfumo imara kama uingereza, mbunge analipwa kama watumishi wengine wa Serikali,

Wanapanda treni za umma kama wananchi wengine, mbona enzi za Nyerere wabunge walipanda treni kwenda Dom bungeni?

Ni muda wa Kupata KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Ameeeen.
 
Mtu anayetaabika halafu halalamiki wala kudai haki yake inafaa akejeliwe ili akili imkae sawa. Kwasabb hawa hawa wananchi wanaoumia ndiyo uchaguzi ukifika unakuta akili zinafubazwa na ubwabwa, kanga na kofia
Kwamba mtu anaamka kwake na kwenda kupiga kura kisa kapewa kofia?
 
Kusema kweli tukiwanyamazia hawa wenye dhamana sasa hivi watatuuzia humu ndani! kama wananunua mabasi 60 kwa fedha za udhulamati wa kodi zetu tutarajie nini zaidi? Tuseme inatosha!
 
Kwamba mtu anaamka kwake na kwenda kupiga kura kisa kapewa kofia?
Ndiyo na kandambili iliyokatika kipande kwa kuchanwa na gwambara. Kavaa tshirt na kofia yenye picha ya mwanamme/mwanamke mwenzake
 
Ni sawa, huo ni utajiri binafsi wa Mbowe.

Bt Mbowe kama taasisi, hawajawahi kupinga ununuzi wa mav8 Kwa Kodi za Wananchi, walikopeshwa na Mbowe kalitumia.

Tuliona pia POSHO za wabunge CDM waliungana na CCM wakitaka ziongezwe, bt wananchi tulitaka zishushwe.

Watuachie wananchi kuhoji bt wao walishindwa KUSIMAMIA.

KATIBA mpya ya Warioba ililiona Hilo ikatight maslah ya viongozi yaendane na kipato Cha wananchi.

Ameeeen.
Aliyechelewa kuongea ni bora sana kuliko aliyenyamaza kabisa
 
Back
Top Bottom