Muda wote alikuwa wapi mpaka anaongea sasa hivi au kaona kule kwenye bank kumemgusa mimi ndio maana siwaamini Wanasiasa wote wapo kimaslahi tofauti yao ni Moja mmoja yupo madarakani mwingine anasaka madaraka kwa kutumia matatizo ya wananchiMbowe ameshazungumza kuonesha msimamo wake, ajabu nyie bado mnaamini hisia zenu, hebu acheni kuishi kama mnatembea barabarani huku mnaota ndoto mchana wa jua kali, amkeni!.
jibu hiloUnaposema Chadema unakusudia hadi na wanachama na wapenzi wa chadema au viongozi tu wa Chadema?
Wewe unaongea hivyo kama Nani una nafasi gani hapo chadema2025 tutawatia adabu
Wewe unayewaza ujinga ndiye unayewaza hivyo ila wenye busara wanajua kaongea mambo ya msingi.Kama ni hivyo angeweza pia kuamua kukaa kimya tu badala ya kuhadaa watu ambao tayari wana shida na wanaumia, siyo vizuri kumkejeli mtu ambaye anataabika tayari!
Hatakama anazo 20 hajanunua kwa kodi zenu. Mnatakiwa muulize akiwa serikalini na kutumia kodi za kutembea kwa v8.Ndugu Mbowe anatumia gari aina Gani? Kabla hatujajadili V8 alonunua mwigu Kwa Kodi zetu!!
Tuanzie hapo.
Iitaridhisha kuona upinzani wa Mbowe upo imara ikiwa atailazimisha serikali kuruhusu mikutano ya kisiasa ambayo si ya kujificha mahala.Hii kauli ya Mbowe kwamba "nakwazika sana kuona wanakuwa waoga" inaonesha bado ana dhamira ya dhati kuleta mabadiliko nchi hii.
Kinachomkwamisha ni kukosekana kwa ushirikiano anaohitaji toka kwetu, tupo kama misukule ndio maana naye anajua hilo, japo ameshindwa kutumia hilo neno kwa heshima yake aliyonayo kwetu.
Naamini wale wajuaji wanaosema kila siku Mbowe amelamba asali ndio maana yupo kimya, sasa ni wakati wao kum-prove wrong Mbowe, simameni mhesabiwe kulinda haki zenu ili Mbowe awe pamoja nanyi.
Hoja nzuri.
Bt tuseme Kweli, Mnyika anaweza akasimama jukwaani na kumwambia mwananchi haya?
Ndugu wananchi, mmetozwa tozo, mmeminywa Kodi Kila Mahali, nichagueni niwawakilishe,
Nitapofika bungeni nitalipwa zaidi ya ml 12 Kwa mwezi, Nitakopeshwa gari ya ml 800 na ntailipa polepole ingawa najua wananchi wengi hapa wanamiliki BAISKELI. Pia wanakosa pesa za matibabu wakiugua.
Nikimaliza ubunge mtanilipa zaidi ya ml 200 kama Asante ya kuwatumikia.
Jambo hili ni la kimfumo. Tuwabane kwenye KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.
Ameeen.
Hata ccm tumeshangaa mwenyekiti wa chadema mwaka mzima kakaa kimya ,bora kaongea tu ,aongee angalau mara mbili Kwa mwaka.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.
Angekuwa ni mtumishi wa umma ndiyo kasema hivi! mngemfukuza kazi, mngemkamata na kumfungulia mashtaka ya utovu wa nidhamu, na bla bla nyingine!Anaongea nini huyo nae, atulie hakuna wa kumsikiliza.
Uchaguzi wa Kenya hauna mizengwe
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.
Hizi hapa nukuu za Mbowe...
“Tunapowapa Watawala nafasi ya kuongoza maisha yetu na wanaamua bila kujali kinachotupata, hatupaswi kuwa waoga.
Kuna wakati nakwazika sana kwa kazi ninayofanya mnapokuwa waoga na hofu, halafu mnalalamika.
Hao wanaowatoza kodi hiyo wanakwenda kununua V8 ya Shilingi Milioni 450 au 500, mtu ambaye angekuwa nyumbani kwa mumewe au mkewe asingeweza kununua V8.
Lakini kwa kuwa kuna pesa ya Wajinga Watanzania wanaweza kununua gari la kumpa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Jaji kila mmoja.
Jiulizeni ni Wafanyabiashara wangapi ambao wana uwezo wa kuendesha magari mapya?
Magari mapya Nchi hii ni mali ya viongozi wa Serikali, na mnavyokaa kimya mambo haya ndiyo yanaendelea, mnatakiwa kuamka.
Kama mnataka kuibadilisa Nchi hii lazima tuache woga, lazima viongozi wa dini muongee.
Nilimwambia Rais Samia hii simulizi ya ‘amani’ ‘amani’ ‘amani’ ni kupoteza muda, simulizi sahihi ni haki haki haki.
Kuwepo na haki kwa watu wote litakuwa tafa bora la kuishi. Watanzania wameangalia uchaguzi wa Kenya kila mmoja ametamani, ulikuwa wa wazi hakuna mizengwe
Ndugu Mbowe anatumia gari aina Gani? Kabla hatujajadili V8 alonunua mwigu Kwa Kodi zetu!!
Tuanzie hapo.
Mbowe ni tajiri kuanzia 1970s